Yaliyowakuta wapemba wakiwa safarini

Written by  //  02/12/2009  //  Mengineyo  //  2 Comments

Ilikuwa ni siku ya ijumaakuu ya mwaka 2006 wakati nikiwa katika mjzungoko ya kujitafutia rizki halali, jua lilikuwa linazama tena katika kijiji kiitwacho masuguru bagamoyo mkoa wa pwani kamasikosei ni kijiji alikotokea mh. rais Kikwete..

Nikiwa na mwenzangu jina hemed. Tulipoona jua limetua na tulikuwa mifukoni tuna pesa ambazo ndio msingi wa mihangaiko yetu tuliona nibora kuomba hifadhi kwa serikali ya kijiji hicho tusije tukaporwa.

Tuliripoti kwa mtendaji wa kijiji hicho alitupa chakula pia alitusaidia simu kwani zetu hazikuwa nachaji ili tuwasiliane na jamaa zetu pemba.Diwani huyu alikuwa mkarim sana alitupa na jamvi la kujipumzishia.yote haya ilikuwa baada ya kujieleza na kuridhika kuwa tulikuwa ni wasafiri tuliohitaji msaada.

Amakweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Kwani ghafla kibao kiligeuka.Ghafla alikuja diwani wa kijiji kwa jina moja la Mapipi
Diwani Mapipi nae alituhoji kama mwenzake na kuridhishwa na maelezo yetu ila mwisho alituuliza kwani nyinyi ni watu wawapi ? tukajibu PEMBA loooo pale alibadilika utu aliuvua akavaa unyama.

Siamini kama dunia inawaja kama bw huyu. Alitoa simu yake na kupiga, ehe hapo ni polisi bagamoyo? sawa mimi ni diwani Maplpl hapa kijijini tumekamata majambazi wawili na wananchi tumewadhibiti njooni haraka. Akapiga simu nyengine kama hiyo polisi chaljnze.sisi tupo pekeyetu kwenye jamvi alotupa mtendaji na wao wawli wamesimama hapakuwa na mtu mwengine.

Mtendaji hakuridhiswa na kitendo hicho kwani walitupiana maneno.Kwanini unawafanyia hivi hawa vijana wasiokuwa nahatia?aliukiza mtehdaji, akamjibu waache tuwakomeshe.

Hatimae gari aina ya landrover liliingia kwa kasi likitokea polisi chalinze likiwa na wapiganaji wasiopungua 10 wakiongozwa na ocs ambae pia alikuwa dereva wa gari hilo, wote wakiwa na submachinegun, wanakijiji walishtuka kuna nini? wakiuliza hao majambazi wako wapi? mapipi akajibu hawa hapa kidole upande wetu.

Alokufa MUNGU amrehem, simamajuu hapo tulisalimiwa kwa vibao mateke ngumi matako ya bunduki, ama mapipi sitomsahau zoezi liliendele kwa madakika kadhaa. mwisho tulifungwa kamba ya kitani mikono nyuma hadi polisi chalinze mwendo wa saa 4 usiku.

Amakweki dhulma ipo, kwani tulipotiwa mapokezi tu ocs alitoa amri kwa askari wa zamu akisema wape ile file ya wame .hapo wame ulifanyika ujabazi kuvamiwa lori na kuporwa mapesa na vitu vya thamani siku chache zilopita lakini wavamizi hawakupatikana, hivyo tukapachikwa sisi kesi hiyo.

Makubwa yalitukuta jee ni yapi hayoo? angaza macho kwenye makala ijayo nikupe yalotufika kituo cha polisi chalinze,polisi bagamoyo, mahakama ya mkoa bagamoyo na jela ya kigongoni mkoa wa pwani. YOKA

Tulisota mahabusu ya chalinze kwa siku 4 . hapo nilishuhudia mambo ya ajabu mlo wa hapo ni ugali wa sembe kwa supu ya dagaa kavu kauzu looo.

. jamaazetu walikuja kutoka dar kutaka kutuchulia dhamana walidunda wallambuli kutununulia chips kuku na maji safi. chaajabu mifupa tuliyo itupa wenzetu tuliowakuta waliiwania na kuisaga kwa meno alau nawao wawe wamekula kuku.looo

jambo jengine ni kuchaanganywa na watoto walikuwemo watoto wawili wenye umri mmoja miaka 11 na mmwmengine 7 hawa walikuwa na kesi ya kuvunja kioo cha gari niliwahoji ilikuwaje wakasema walikuwa wanapiga ndege kwa manati loooo.

Maisha ya hapo chalinze yalikuwa magumu sana hasa kwa wale wasio na watu wa kuwashughulikia. mimi nilikuwa na pesa 2330000 kamasijasahau na mwenzangu 180000 ambazo tulizisalimishakituoni na kuandikwa kwenye kitabu cha mahabusu PPR. ambazo siku ya kupelekwa mahakamani tulipewa na hapo hapo kuzichukua ocs na ikawa yamle sikuziona mpaka leo loooo.

Baada siku 4 siku ya jumaane tulipigwa pingu chini ya ulinzi mkali hadi kituo cha polisi bagamoyo. wkati tumo gari i tuliomba msaada wa kupigiwa simu binadam wote si wabaya, tulipata na no ambayo nilikuwa nayo kichwani ambayo huenda tukapata msaada wa adhabu hii ilikuwa ni ya mbunge mmoja wa cuf ambae pia ni waziri kivuli wa wizara fulani sipendi kumtaja kwani aliyapuuza yote niliyo mueleza juu ya yaliyotufika na kwa wakati huo yeye alikuwa yuko dar nilimueleza yeye kwa vile nilikuana karibu sana kwenye mambo ya chama.

Wapili nilimpigia rafikiyangu wa karibu sanaa sh Salim awadh omar ambae nashkuru MUNGU niliona msaada wke kwani hakusita kumpigia kamanda wa mkoa kwa wakati huo mzee Mbirikira.

Kamanda alitaka kujua wakati alipompigia simu ocs alipewa maelezo kuwa ni watuhumiwa wa kesi ya uvamizi hapo wame darajani.
Kamanda alitoa agizo kuwa tufanyiwe IP yaani gwaride la utambulisho
kama hatukutambuliwa tuachiwee loooo gwaride lilifanywa na hatukuacchiwa kesi yakwanza ilikuwa ni kumwaga misumari na kuliteka lori na kupora sh milioni 7 simu moja ya mkononi na pea moja ya sendols.

Kesi hii ya kwanza inadhamana na wakati huo wenzetu wlikuwepo kila tunapopelekwa kikosi hiki kiliongoza na bw Mahfoudh khamis .

tulilazwa mahabusi ya polis bagamoyo hee hapo ni balaa,kwa akili yangu ya ufundi nilikipima chumba hicho kilikuwa na urefu ft 10 kwa upupana wa ft 6. niliamini wadudu kama kunguni na chawa walikuwa labda wanamiminwa kwa vipolona mbu wlikuwa waingia na kutoka vile kama ndege za kivita mbu ambao wasifa ya kutoogopa kufa kwa kupigwa kofi wanapotua mwilini ni wakupangusa.

adhabu kama hii sijapata kuiona marazote ambazo nilwahi kuwekwa hapo kwetu. kulipokucha tulipelekwa mahakamani na sasakushindiliwa ji kesi liitwalo WIZI WA KUTUMIA BUNDUKI looooo maskini kwa uzoefu wangu hii ni kesi ya tatu kwa ukubwa ikiongozwa na uhaini na mauaji.binadam hatujali kama tumeumbwa..
kile kikosi chetu kilibwaga manyanga chini na walibakia kumwaga machozi kesi haina dhamana sisi haoo tunapelekwa rumande jela iitwa kigongoni ambayo iko nje kabisa ya mji wa bagamoyo .

makubwa tuliyaona hapokigongoni hapo si duniani wala si akhera katika sehem ya tatu ya mkasa huu ninakupeni hayo ya huko kigongoni tega jicho mwanaukumbi ujue kama nchi hii dhulma zinafanywa kwa wsio na hatia.

Chanzo:Story hii imetolewa na Shk.Rajab..pengine tutakuleteeni jinsi inavyoendelea

2 Comments on "Yaliyowakuta wapemba wakiwa safarini"

  1. Bigfather 02/12/2009 kwa 9:19 um ·

    Poleni sana , hilo ndio tatizo la watu kuchagua viongozi ambao hawakusoma ukiunganisha na kuajiri askari polisi ambao hawakusoma , kwahio maamuzi yao huwa yanatoka ndani ya vichwa vyao.

  2. ommykiss 02/12/2009 kwa 11:26 um ·

    Kwanza nakupa pole sana kwa matatizo haya makubwa yaliokukuteni. mimi hapa sioni kama tatizo ni kua polisi hawakusoma ila hapa umepita ubaguzi kwa kuwa hawa ni wazanzibari basi tutawaonesha kilichomtoa kanga manyoya.
    Tafadhali usisite kutumalizia hichi kisa japo kama kinaumiza moyo ila sisi wengine tunakichukulia hichi kama ni funzo kwa kujua vipi tuweze kuishi na hawa watu wenye chuki na utaifa wetu.

Comments are now closed for this article.