Habari

Mgogoro wa kisiasa zanzibar lazima utatuliwe

Na Mohamed Nur

Mgogoro wa kisiasa Zanzibar uliopandikizwa makusudi na viongozi wenye uchu wa madaraka wasiojali maamuzi ya watu, wenye tamaa ya kubaki kwenye madaraka pasi na uwezo wala uthubutu wa kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi ni lazima utatuliwe.

Lakini Wazanzibari walio watulivu, wavumilivu na wapevu sana katika medani ya kisiasa haipaswi kudhihakiwa katika utatuzi huo. Makala ya Deus, ambayo ime “hint” haja ya utatuzi wa mgogoro huo inapaswa kutambuliwa kama hatua nzuri ya kuwaelimisha wananchi. Pamoja na uzuri huo kumtaja JK kama mpatanishi ni fikra yake, ambayo tunaweza pia kuivumilia ila lazima tuikunjue kidogo kitaarifa.

JK kuwa msuluhishi ni dhihaka kwa Wazanzibari, ambao wamedhalilishwa mno na migogoro mingi yakutengeneza makusudi. Mtengenezaji ni mtawala, yule mwenye majeshi, anaeyaamuru yafanye nini wapi.

Ni JK huyu aliesema katika bunge 2005 kuwa ataushughulikia mgogoro wa Zanzibar. Akaitisha vikao Bagamoyo kwa miezi isiopungua 14. Akiwa Mwenyekiti wa CCM kazi yote iliyofanywa na viongozi wa CCM na CUF kwa kutumia fedha za wananchi maskini wa Tanzania, ikadharauliwa. Kikao cha Butiama kikakataa proporsal ya timu ya mazungumzo. Very simple!

Ni Wazanzibari wenyewe waliokaa chini, wakatafakari na kuona hebu iwe basi. Lakini pamoja na maridhianao yaliosimamiwa na Maalim Seif na Mhe. Karume, akiwa Rais wa Zanzibar, na kupelekea Serikali ya Umoja wa Kitaifa 2010 – 2015 JK ameshindwa kusimamia kustawi kwa serikali hiyo ama kustawi kwa maridhiano baina ya wananchi wa Zanzibar. Kila alama iliyochomoza kuonesha kuwa maridhiano Zanzibar yanaelekea kuchafuka ilionekana wazi na vyombo vya dola. Amiri wa vyombo hivyo, JK, hakuchukua hatua yeyote. Mimi naamini kuwa Maalim Seif hakuachia tu kuwa amirijeshi, JK, anapashwa habari na vyombo vyake naamini Maalim atakuwa amemjuilisha JK ama kwa maandishi au uso kwa macho. JK ameshindwa kuzuia kuvurugika kwa Maridhiano Zanzibar.

Huyu HAFAWI HATAKUKARIBIA MEZA YA MAZUNGUMZO.

Katika miaka yake kumi JK ameondoka mgogoro wa kisiasa Zanzibar ukiwa ni mbaya zaidi ama sawa na mwanzo alipoingia. AMESHINDWA. Au hakutaka makusudi akiwa ana nyenzo zote na amri. Ameshindwa akijua kuwa Wazanzibari wengi toka pande zote mbili zinazovutana wamechoka na migogoro. Wazanzibari hao wakamchagua kinara wa MARIDIANO, Maalim Seif, kuwa Rais wa Zanzibar ili aendeleze spirit ya Maridhiano. Alas!! JK alikuwepo, bado ana nguvu na amri, akamimina majeshi kuzuia demokrasia.

JK kuwa mpatanishi ni kumtukuza na kumpa nishani ya ushujaa kwa jambo ambalo alisimama kidete kulipinga badala ya kulijenga. Hiyo itakuwa ni DHIHAKA kwa Wananchi wa Zanzibar. Itakuwa dhihaka kwa demokrasia ya kweli.

FB

Share: