Habari

Mgogoro wa kukata umeme ni hoja ya kitaifa, Wazanzibar tuungane

Kutofautiana kimitazamo au kuwa na maoni tofauti ni kawaida ya binaadamu. Faida yake kuu ni kuongeza ushindani baina ya pande zinazotofautiana muhimu zaidi pale yanapofikiwa makubaliano.

Kwanza ni mpongeze Dr Shein kwa msimamo wake juu ya mgogoro wa kutaka kukatiwa umeme Zanzibar. Dr Shein katika taarifa yake ni nyepesi sana kuifahamu. Ukianzia lugha aliyotumia hadi body language ili kamilika, nampongeza kwa hili.

Magufuli angekuwa kiongozi makini na kama alivyosema Tanesco sio taasisi ya kisiasa alikuwa aiwacha Tanesco nje ya uwanja wa siasa. Sasa hivi tayari ameishaitumbukiza kwenye siasa.

Wazanzibar tunahitaji kujenga hoja za pamoja kwenye mgogoro huu. Hili ni suala la kitaifa. Tuanze kubainisha baada ya hoja za kivyama na hoja za kinchi

Mgogoro wa ulipaji umeme ni suala la miaka mingi sana. Hii ilitokana na dhana zilezile za Kikoloni walizo nazo mabwana zetu.

Zanzibar kwa decades ilikuwa ikizalisha umeme kwa generator zake wenyewe. Hadi ilipofika miaka ya 80 kuongezeka mahitaji ya utumiaji nishati hii ndio wazo la kununua umeme kutoka Tanganyika likazaliwa. Wakati suala la nishati halikuwa katika orodha ya mambo ya muungano.

Bila ya shaka kwa vile ni suala la kibiashara baina ya nchi mbili, Zanzibar na Tanganyika kulikuwa na mikataba ya kibiashara. Hapo sitokwenda mbele zaidi

Kwa umri wangu, makubaliano haya ya kibiashara yamekuwa yakivunja na kila upande. Zanzibar kwamba imekuwa hailipi vile inavyotakiwa. Tanganyika nayo inashindwa kutoa good service na value for money. Wakati huohuo wamekuwa wakiiadhibu Zanzibar kwa kuiuzia bei ya juu.

Hoja hizi mara kadhaa zimepigiwa kelele. Nakumbuka hata kwenye majukwaa ya Chama cha Wananchi CUF ikizungunzwa kwamba Tanganyika inaiuzia umeme Zanzibar kwa malipo ya dola.

Mwanzo Tanganyika ikizalisha umeme kwa kutumia maji (hydropower), sasa hivi wanazilisha umeme kwa kutumia gas, ambayo ni ya Muungano, vipi hapo?

Hivyo basi mgogoro huu umechochewa na dhana ya wakamue uwatawale. Ni wakati Wazanzibar kuwa kitu kimoja, kujenga hoja za pamoja kudai haki zetu. Na pale tunapodaiwa tubebe deni hilo kwa pamoja.

Tuje na hoja katika kipindi hichi kifupi zenye muelekeo wa muda mfupi pia zenye muelekeo wa muda mrefu.

Tukubali ZECO imekuwa ikiwapatia umeme Wazanzibar kwa bei rahisi ikilinganishwa na Tanganyika kwenyewe unakotoka.

Share: