Habari

MKUTANO MKUU & UCHAGUZI WAKE [ZAWA UK]

Kwa niaba ya Zanzibar Welfare Association UK, napenda kuwatanabahaisha Wazanzibari wote wanaoishi UK kuwa ZAWA UK imo katika matayarisho ya kufanya mkutano wake mkuu katika mwezi wa MAY mwaka huu, tarehe na mahala pa kufanyika mkutano huo mtajuulishwa.

Yatakayo zungumiwa siku hiyo ni mafanikio yaliyopatikana, matatizo tunayokabiliana nayo, matumizi ya fedha kutoka mwaka 2011-2012.

Pia kutafanyika uchaguzi mkuu wa Jumuiya ambazo nafasi zote 15 zitakuwa wazi, kuanzia Mwenyetiki hadi wajumbe wa Jumuiya.

Kama Mwenyekiti ninaemaliza muda wangu kwenye muula huu nawaomba Wazanzibari wenzangu kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huu na kugombania nafasi zote zilizopo. Pia kufika kwenu ndipo kutapofanya ZAWA UK izidi kusonga mbele.

Ahsanteni.

Hassan Khamis

Share: