Habari

MPANGO MPYA WA KUIHUJUMU CUF, UMESUKWA NA MASSAUN AKIZIDI KUMTUMIA LIPUMBA.

MPANGO MPYA WA KUIHUJUMU CUF, UMESUKWA NA MASSAUNI…AKIZIDI KUMTUMIA LIPUMBA….

Watawala wa dola ya Jamhuri waliokabidhi kazi maalumu kwa Kamati ya Kuimaliza CUF (KKC) kamati ambayo imeasisiwa kwa nguvu za dola kuu ili kukisambaratisha na kukiua Chama cha Wananchi CUF kwasababu ya ushindi wa Uchaguzi wa Zanzibar wa October 2015 na ushindi wa kura nyingi za UKAWA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao matokeo yake pia yalichakachuliwa. Kamati hiyo ambayo inajumuisha Viongozi wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali haramu ya Dr. Shein na Ofisi nyeti ikiwemo Ofisi ya Msajili, SMZ, M/kiti wa ADC pamoja na mipini Khalifa Suleimn, Mohd Habib Mnyaa na Nasssof Seif Amour ndio iliokua ikipanga yote yaliyotokea mwanzo hadi hapa tulipofika ili kuihalalisha Serikali haramu ya Dr. Ali Moh’d Shein na kuua UKAWA kwa lengo la kwamba CCM ipate ushind wa kura nyingi 2020. Yote hayo yamethibitishwa na Kibaraka Lipumba juzi katika kipindi cha mahojiano na Cloud FM pale alipotamka wazi kumpongeza Jecha Salim Jecha jambo ambalo lilianza kutokea tangu siku kundi la Kibaraka Lipumba lilipokuja uuvuruga Mkutano Mkuu pale kundi hilo lilipojitokeza wazi na kusema kua “Ni bora Jecha kulikoMaalim Seif”. Hii ilionyesha wazi kua Kibaraka Lipumba na kundi lake linaunga mkono uharamia wa Dr. Shein na linabariki uwepo wa Serikali haramu ya Dr. Shein.

Pamoja na yote hayo CUF Taasisi imeendelea kumsumbua Kibaraka Lipumba na Dola baada ya Maalim Seif kueka wazi njama zao zote za kukihujumu Chama cha Wananchi CUF tangia pale alipofanya Press Conference katika ukumbi wa Ramada mnamo tarehe 9/04/2017 ambapo Mkutano huo ulihudhuriwa na Vyombo vya Habari 72 vilivyopo nchini. Maali Seif katika mkutano huo alieleza wazi njama za kuitumia RITA kukihujumu Chama cha Wananchi CUF na kusema kua “Sasa hatutokubali kuvumilia tena mumeshatufikisha kwenye ukuta” kauli iliyowakosesa usingizi kundi la Kibaraka Lipumba na Dola wanayoitumikia.

Pia ziara za Katibu Mkuu-Maalim Seif zilizoanza hivi karibuni mjini Dare-es-salam zimekua pigo jengine kwa Dola na kundi hilo baada ya kundi la Kibaraka Lipumba na Dola kushindwa kufanya fujo na kuzuia ziara hizo kama walivyopanga hapo awali. Katika ziara hizo Maalim Seif alikutana na Mh. Edward Lowassa, Viongozi wa NLD na Baba Askofu Gwajima pamoja na wazee kutoka maeneo mbali mbali ambao waliungana na Maalim Seif katika ziara zake. Kitendo hicho cha Maalim Seif kuktana na Vingozi hao limekua pigo kwa kundi la Kibaraka Lipumba na Dola hasa kwa kile kinachodaiwa kua kundi hilo kwa kushirikiana na Dola lilipanga kumzuia Maalim Seif lakini wameshindwa kufanya hivyo.

Baada ya pigo hilo la Maalim Seif kufanya ziara zake Dare-es-salam na kuwazindua watu wa Mikoani jambo ambalo Kibaraka Lipumba na Genge lake mwanzo walilikejeli na kusema kua Maalim Seif hatofanya ziara hizo za kikiimarksha Chama na kushindwa kufanikisha mpango wao wa kumzuia, kundi hilo limejikuta likikesha katika vikao kupanga njama nyengine za kukihujumu Chama cha Wananchi CUF ili kukamilisha utumwa wa mabwana zao (Dola) ambapo katika kikao chao cha hivi karibuni kundi la Kibaraka Lipumba likisaidiana na Dola zote mbili chini ya Naibu Waziri wa Mambo ya ndani (Masauni) ambaye juzi ndie alieamrisha kughairishwa kwa Ziara ya M/kiti wa Kamati ya Uongozi Mh. Julius Mtatiro mkoani Tanga jambo ambalo alishindwa kujitetea alipobanwa na Wabunge Bungeni pamoja na Baloteli (Balozi Sefu Ali Iddi) sasa wamepanga kumtumia Kibaraka Lipumba kwenda Pemba.

Kibaraka Lipumba amepangiwa kwenda Pemba ambapo ameahidiwa kutataftiwa Wanachama wa CCM, ADC na Chama cha Wakulima kinachoongozwa na Said Soud na kuvishwa sare za CUF ili ionekane kua Kibaraka Lipumba amekutana na Wanachama wa Chama cha Waananchi CUF. Tukio hilo limepangwa kufanyika ndani ya ukumbi wa Makonyo ambapo Habibu Mnyaa na Khalifa Suleiman na Hamad Rashid ndio wasimamizi wakuu wa mpango huo.

Mkuu wa mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba pamoja na Ma-DC wote tayari wameshapewa maagizo na Dola ya kumtaftia watu Kibaraka Lipumba kutoka CCM, ADC na AFP katika maeneo mbali mbali kama vile Kangagani, Wawi, Mwambe, Mkanyageni, Mkoani na Chokocho pamoja kumuandalia ulinzi wa kutosha kutoka Uwanja wa ndege na mda wote wa shughuli hiyo.

Wakati Dola ikimtumia Kibaraka Lipumba na genge lake kukihujumu Chama cha Wananchi CUF hali ya Chama cha Wananchi CUF inazidi kuimarika siku hadi siku huku CCM ikizidi kua katika hali ngumu. Mabodi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM anaonekana kama vile hana msaada wowote ndani ya Chama hicho kwa kile kinachodaiwa kua hana jipya alilolifanya tangia aliposhika nafasi hiyo. Kitendo cha Dr. Ali Mohd Shein kususiwa fomu za uchaguzi katika mkoa wa Kusini kimezidi kukiweka katika hali ngumu Chama hicho na kuwakosesha usingizi Viongozi wa Chama hicho huku Dr. Shein akifadhaishwa na kushangazwa na hali hiyo.

Katika kukabiliana na njama zote hizo CUF-Chama cha Wananchi kinaamini kua kitazishinda njama zote zinaopangwa na Dola kupitia kibaraka wake Lipumba na mipini yake kama kilivyoshinda njama za Dola zilizotumika kipindi cha Mapalala na Vibaraka wengine wa CCM huku Wanachama wa Chama hicho upande wa Pemba wakisema kua wanamsubiri kwa hamu Kibaraka Lipumba na genge lake na kumuonya kwa kumwambia kua “Pemba Peremba ukenda na Joho utarudi na Kilemba”.
FB

Share: