MSIMAMO WANGU NI KURA YA NDIO-SPIKA KIFICHO

Written by  //  18/07/2010  //  Habari  //  28 Comments

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho.
  • Spika atoa kauli yake ya NDIO kwenye Kongamano la MUWAZA

Salma Said, Zanzibar

WAKATI wajumbe wengi wa Baraza la Wawakilishi wakiogopa kutangaza misimamo yao juu ya kura ya maoni, Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ametangaza msimamo wake kuwa atapiga kura ya ndio ili kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

“Mimi mkiniuliza nifanyeje nitasema weka ndio julai 31 katika kura ya maoni” alisema Spika huku akicheka na kupigiwa makofi wa vigeregere vya pongezi.Msimamo wa Spika iunakuja siku moja baada ya Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume kurudia kauli yake ya kuwataka wananchi wa Unguja na Pemba kupiga kura ya ndio ifikapo Julai 31 mwaka huu ili kutoa nafasi ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo ndio inayoonekana njia sahihi ya kumaliza migogoro ya kisiasa.

Juzi Rais Karume aliwaambia wananchi wa Gombani ya Kale Kisiwani Pemba kwamba atawashangaa wananchi wa kisiwa hicho ambao kwa miaka kadhaa wamekuwa katika migogoro ya kisiasa iwapo watakataa kupiga kura ya ndio ili kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itawashirikisha vyama vya siasa katika serikali hiyo.

Mbali na Rais Karume mgombea wa urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein naye aliwataka wananchi wa Pemba kuunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa kwa kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura ya ndio ili kumaliza matatizo ya kisiasa yaliopo na Zanzibar kuondokana na siasa za chuki na uhasama.

Baadhi wa wajumbe wa baraza la wawakilishi hasa kutoka chama cha CCM wamekuwa na khofu ya kutangaza misimamo yao wakiogopa kunyimwa kura katika majimbo wanayotoka.
“Si kama tunakataa umoja lakini kuna ugumu wake kuungana na CUF ni jambo kubwa lakini jengine wananchi wetu hawataki serikali ya umoja wa kitaifa na inakuwa vigumu sisi wawakilishi kwenda majimboni kusema suala hilo na ndio ukatuona tumekaa kimya kila mmoja anaogopa kutangaza msimamo wake” alisema mwakilishi mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa jimbo la Tumbatu CCM, Haji Omar Kheri alikiri baadhi ya wawakilishi wanaogopa lakini alisema yeye binafsi amekuwa mstari wa mbele katika kuwataka wananchi wajitokeze katika kura ya maoni bila ya khofu.

“Mimi ni mwakilishi wa jimbo la Tumbatu CCM na ninapofanya mikutano katika jimbo langu nawambia wananchi wangu tieni kura ya ndio kwa sababu hili ni agizo la chama chetu sasa hao wanaoogopa sijui wanaogopa nini” alisema Kheri.

Akizungumza katika kongamano la kura ya maoni na umuhimu wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar katika ukumbi wa Baiytul Yamini Malindi Mkoa wa Mjini Unguja, Spika Kificho alitoa historia ya Zanzibar na migogoro iliyotokea huko nyuma hadi sasa.

Alisema mbali ya chaguzi nyingi zinazofanyika tokea kabla ya mapinduzi na baada ya mapinduzi lakini amani na utulivu unaotokana na chaguzi hizo haujapatikana hadi sasa jambo ambalo limewasukuma viongozi wa kisiasa kuwa na utashi wa kisiasa wa kutaka maridhiano.

Kificho alikuwa akichangia mada ya majukumu ya waandishi wa habari katika kura ya maoni na serikali ya umoja wa kitaifa iliyowasilishwa na mwandishi wa habari mwandamizi, Salim Said Salim ambapo alisema waandishi wana jukumu kubwa katika kuhakikisha nchi inakuwa salama.

Salim alisema waandishi wanapaswa kuandika ukweli juu ya suala zima la kura ya maoni na kutosita kuwafichua wale wote wenye nia mbaya na wenye kuweka vizingiti katika suala hilo ili kuiepusha nchi kuingia katika janga la vita huku akitoa mifano ya nchi zilizoingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi nyengine za Afrika.

Mwandishi huyo akizitaja nchi ambazo zimewahi kukubwa na migogoro ya kivita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ni pamoja na Rwanda, Burundi na Somalia na matukio ya Kenya yaliotokea wakati wa uchaguzi mkuu ambapo mamia ya watu walipoteza maisha na wengine kuhama nchi yao kutokana na uchochezi wa wanasiasa na waandishi wa habari.

Akiwasilisha mada ya faida ya serikali ya umoja wa kitaifa, Mwanasheria Mwandamizi, Salim Tawfiq alisema wazanzibari wanapaswa kuzingatia walipotoka na hapa walipo na kutotoa mwanya wa kutorejeshwa nyuma ambapo migogoro ya kisiasa ilikuwa imeshamiri na kudumaza maendeleo nchini.

Tawfik alisema serikali ya umoja itaundwa kwa makusudi ya kuleta utulivu kutokana na migogoro ya kisiasa iliopo katika wakati maalumu na itaundwa kwa sababu wahusika wanataka kuondokana na mivutano.
Mwanasheria huyo amesema serikali ya umoja inatokana na mkataba ambapo pende mbili zinazovutana lazima zikubaliane na serikali itokane na makubaliano hayo ambapo haitagemei kabisa nguvu ya kisiasa ya mmoja katika wanaovutana.

Alisema iwapo kura ya maoni itapitishwa, itaudnwa kwa maelekezo ya katiba na taratibu za kupitisha marekebisho ya katiba itabidi zifuatwe ambapo vyomvyote iwavyo serikali ya umoja lazima iwe kama wahusika walivyokubaliana.

28 Comments on "MSIMAMO WANGU NI KURA YA NDIO-SPIKA KIFICHO"

  1. binamu 18/07/2010 kwa 3:41 um ·

    MIMI NAPATA KIGUGUMIZI SANA NINAPOWASIKIA WANASIASA NA WATU WALIOPEWA JUKUMU LA KUSIMAMIA SHERIA ETI LEO WANAKUWA NA LUGHA TAMU, WANAJIFANYA MAULAMAA NA WATU WENYE HURUMA SANA AU KUITAKIA MEMA NCHI HII. WAJUWE TU ADHABU YA MNAFIKI KWA MWENYEZIMUNGU NI KALI KULIKO HATA YA MUUWAJI AU KAFIRI.
    INASHANGAZA MTU KAMA KIFICHO, MTU MZIMA, MSOMI, ALIHAJI/ALHAJI, MWENYE MASHAHADA KIBAO YA SHERIA MPAKA KUFIKIA KUKABIDHIWA RUNGU LA DOLA, AMBAPO ALIKUWA AKILITUMIA RUNGU HILO HILO KUWAGONGA NAA KUWADHULUMU WAISLAMU WENZAKE KAMA KWAMBA HAJUI KAMA KUNA KUFA NA KUHUKUMIWA. LEO ANAJIFANYA KUELEZEA HISTORIA YA ZANZIBAR, CHAGUZI ZA ZANZIBAR, MATESO YA WAZANZIBAR NK. NI NANI ALIEKUWA AKIYASIMAMIA HAYA KAMA SI YEYE, AMESAHAU PALE ALIPOKUWA AKIWADHULUMU WAWAKILISHI WA UPINZANI KWA KUWANYIMA HAKI ZAO NA ZA JAMII WANAOWAWAKILISHA, KUWAFANYIA VISA MPAKA KUFIKIA KUWATOA NJE YA BARAZA NA WAKATI MWENGINE MPAKA KUWAFUNGIA VIKAO, LEO HII KAWA ANAIHURUMIA NCHI, MNAFIKI MKUBWA, ANATAFUTA MAZINGIRA YA KUJIPATIA MAFAO NA KIBARUA CHENGINE BAADA YA UCHAGUZI TU HAWANA LOLOTE. KAULI KAMA HIZO WANAZOZITOA ZILITAKIWA ZISIKIKE KWA WATU WENGINE AU ASIKIKE YEYE AKIWASHUTUMU WATAWALA WENGINE WALIOKUWA WAKIFANYA DHULMA HIZO. LEO AKISEMA HAYO TUMUHUKUMU NANI, BASI TUMPE RUNGU LAKE AJIPIGE NALO KWA SABABU MWIBA UNAPOCHOMEA NDIPO UNAPOTOKEA. WAJUE KUWA ISHI MPAKA UOTE MVI ZA KIJANI LAKINI MAUTI YANAKUSUBIRI NA KILA CHEMBE YA OVU ULIYOTENDA UTAULIZWA NA UTAWAJIBIKA NAYO, WALA HAWATOKUSAIDIA KITU HAO ULIOKUWA UKIWAPINGIA KIFUA HUKU UKIDHULUMU WENGINE KWA KUTAFUTA RADHI ZA UKUBWA NA MAISHA YA DUNIA.
    EWE MOLA, TUDHIHIRISHIE NA UWAFEDHEHESHE WANAFIKI NA WALE WOTE WANAOJIVISHA NGOZI ZA KONDOO ILHALI NI MBWA MWITU.
    YA RABBI TUNAKUOMBA UWALIPE HAPA HAPA DUNIANI NA AKHERA IENDE HESABU, WADHALILIKE NA WAHASIRIKE KUANZIA DUNIANI HADI SIKU YA MALIPO.
    WALA TAZIDI DHWALIMINA ILA DHALALA, WALA TAZIDI DHWALIMINA ILA TABARA, WALA TAZIDI DHWALIMINA ILA KHASARA.
    WABILLAHI TAWFIQ

    • Taymiya 19/07/2010 kwa 11:42 mu ·

      Ustadh wangu binamu.
      Najuwa unamachungu sana na yaliopita hapa Zanzibar, lakini nahisi na ukweli hasa hayajakufika wewe kama yaliomfika Bilal Bin Rabah. Bilal Radhiya llah Anhu, alipata misukouko mikubwa kutoka kwa wale waliommiliki kipindi cha Ujahilia. Lakini walewale waliokuwa wakimtesa mfano Abuu Sufyaan mara tu aliposilim Bilal alikuwandie wa mwanzo kumkumbatia.

      Sasa ikiwa hawa watu wanaonesha wameshakubali kuishi kwa umoja basi cha msingi tuwaombee duwa ili hiyo tarehe 31 July Allah akitufikisha tuone hizo kauli zao, hapo ndipo hayo yaliojificha kwnye nafsi zao yatakapodhihiri.

      Ujuwe tu “kila binaadamu ni mwenye kukosea na mbora wa yule ambae amekosea basi ni yule aliyetubia makosa yake[na huwezi kutubia mpaka ukiri]” Hayo ni kwa mujibu wa Hadithi ya Mtume Muhammad amani ya Allah iwe juu yake.

  2. mkarafuu 18/07/2010 kwa 5:05 um ·

    Asalam.

    @Binamu,ndugu yangu hebu nipe hukumu ambayo ungali muhukumu huyu spika kama angalisema msimamo wake ni HAPANA,ungalimwita vipi ikiwa NDIO nimnafiq?.

    Jamani tuzifunzeni kuwa wastahamilivu,na kushukuru pia, kwani Tumeona viongozi wengi wa CCM hadi leo wameshinwa kutoa misimamo yao juu ya hili, sasa akitokea mmoja akiwatayari kuonyensha msimamo wake hasa ikiwa ni NDIO basi tumpongezeni.

    Lengo la hayo maridhiano ambayo tunaojinata kua kuyasapati ni kuitakia mema zanzibar basi lengo moja wapo ni kusameheana na kusahau yalopita,tunataka kuanza sasa kushirikiana na kujenga nchi yetu.

    Ukimuona mtu alikua mbaya na baadae akauona ubaya wake basi huyo tusimuone mnafiq,kwani hata huyo Rais Amani alikua huko huko na alikuja na kasi ya ubaguzi,kama munana kumbuka aliulizwa siku moja na waandishi mwanzo tu alipoingia madarakani.

    SWALI:Kwanini hukuwachagua wapemba kwenye baraza lako la mawaziri? JIBU: Siwezi kuwachagua watu ambao mimi hawakunichagua wakati wa kura.,lakini leo tunamuona ndio kinara wa umoja na muanzilishi pia wa umoja huo anaouhubiri.

    Wito wangu kwa ngugu zangu wa kizanzibari tusau yalopita na tuangalie mbele tuendako kwa lengo la kuikomboa Zanzibar na Umasikini na kuirudishia heshima ZAnzibar kama nchi nyengine duniani.

    Nakupongeze Mh,Kificho kwa kuonyesha msimamo wako na hata hivyo tuliona jitihada zako barazani katika kuusapoti umoja huu,matumaini yetu hutokua mnafiq.

    AHSANTENI.

  3. kwaomtu 18/07/2010 kwa 5:20 um ·

    MIMI SITOKUJA KUSHANGAA NIKISIKIA HII KURA ATI IMEKATALIWA. NYINYI MUNAWAJUWA SISIEM? MUMESHAKAA NAO MUKAWANUSA HARUFU ZAO? JEE MUMESHAWAHI KUKWANGA NAO? BASI SHAURI ZENU, NAWAAMBIYA HAWA MARA HII WATAMLAZA MTU MLALO WA KIFO CHA MENDE, HAWA JAMAA HAWAAMINIKI HATA DAKIKA MOJA MBELE YA WAVU WA MADARAKA.

    HIVI KURA MUNATIYA MAWAKALA WATU WANAIBA JEE HII INAYOSHUGHULIKIWA NA TUME A 2 Z. SISIEM WAO HAWASHINDWI NA ARGUMENT YA KUJILINDA SI WATASEMA WANAHESHIMU MAAMUZI YA RAIA WALIO WENGI WAMEKATAA TU. NYINYI MAKAFU HEBU SOMENI WAKATI NA TAREKHE ZAKE, MUMESHASAHAU UCHAGUZI WA 1995, PALE VIONGOZI WA SISIEM WALIPOSEMA HAWAITAMBUI TUME YA UCHAGUZI WALIOICHAGUWA WENYEWE NA WAKASEMA PIA UCHAGUZI UREJEWE, MBONA WALIPOTANGAZWA MSHINDI WALIKUJA JUU UPESI NA KUNADI TUME NDIO MUAMUZI WA MWISHO NA WAO WANAHESHIMU MAAMUZI YA TUME.

    TAREHE 31 JULY HAIKO MBALI TUSIANDIKIE MANENO, LAKINI ….

  4. Mshauri 18/07/2010 kwa 5:36 um ·

    haya tuyaache tuyaone yanavokwenda. mie sidhani kana kuna aneweza hata kutabiri iyo kura itakuaje. jawabu la kura hii lipo bara litakuja baada ya wananchi kupigwa na jua kupanga foleni kupiga hio kura. amini usiamina jawabu la ndio au sio liko bara.

  5. salma 18/07/2010 kwa 6:16 um ·

    Asalamu Alaykum.

    Jamani tusiitane wanafik wala kuitana majina mabaya katika hili kila mmoja na matazamo wake lakini tukubaliane kwamba tumetoka mbali na sasa tunataka kutandika misingi ya maridhiano kwa hivyo lazima tujipe moyo na kuvumiliana kama aliavyosema mwenzangu hapo juu.
    katika hili hakuna mshindi kila mmoja anapaswa mbele katika kusukuma maendeleo yetu kwa maana hiyo tusivunjane moyo bali tuwe wavumilivu kwa kila mmoja ambaye hajafahamu basi aelimishwe zaidi kuliko kubezwa, ni wajibu wetu kusaidiana katika kuweka mazingira mazuri zaidi ya kukubalika kwa kura ya maoni kwanza mambo mengine yote yatakuja baadae inshallah hakuna lisilowezekana iwapo dhamira na utashi wa kisiasa utakuwepo.

  6. spark 18/07/2010 kwa 6:33 um ·

    YULE UNOMUITA MNAFIQ UJUE KWA HIVI SASA NDIO YUKO MADARAKANI,NA ENDAPO AKIKUTILIA SHAKA WEWE MPIZANI, ANAWEZA KUONA KUMBE HATA WEWE SIO KWAMBA UNATAKA KUSEMA NDIO KWASABABU YA MAPEZI YA NCHI YAKO BALI UNATAKA IWE NDIO ILI UIINGIZWE MADARAKANI TU KWA MASLAHI BINAFSI. SIO AJABU HATA YEYE AKABADILI MSIMAMO NA KUPIGA YA HAPANA. KAMA HUTOKUWA NA MOYO WA KUSAMEHE UJUE HATA HAYO MARIDHIANO HAYATOFIKIWA, TUACHE JAZBA KUAZA KUWAITA WATU WANAFIQ KWA KUTOA MISIMAMO YAO TENA YA BUSARA HASA KATIKA HIZI DAKIKA ZA LALA SALAMA.

  7. kwaomtu 18/07/2010 kwa 6:36 um ·

    SALMA KIPENZI CHETU KWA SISIEM HAKUNA CHA KUSTAHMILI TENA, HAO NYINYI MUKO HAPOHAPO ZANZIBAR NA HAMUJAWAJUA TU TABIYA ZAO! HEEHE! AMA KWELI ASIYESIKIA LA MKUU.. JAMANI MIMI NILIKUWA NIKO FIFTY FIFTY NA HAWA SISIEM JUU YA HAYA MAONI WALIYOYAPIKA. HAPA AMANI ALIWEKA MTEGO, YAANI IKIWA BILALI ATAUKWAA UGOMBEYAJI WA URAISI KUPIA SISIEM BASI ENGELIJITAHIDI NA KUSIMAMIA KIDETE UCHAGUZI UWE WA HALALI NA LAKINI ZAIDI KURA YA MAONI INGELIIFANIKISHA ILI KUMUWEKEA KIZINGITI CHA KUPAMBANA NA WAPINZANI NDANI YA SERIKALI YAKE.

    LAKINI SASA WAKATI ALIYEPATA NI SHEHA WAKE BASI ITAKAYOBAKIA NI MANENO YA MSISITIZO TU KUWALAGHAI MAKAFU, LAKINI HAPO HAPAWI KITU,KWENYE KURA YA MAONI WAZANZIBAR HASA KAFU WATAPIGWA KIFO CHA MENDE WASIWEZE TENA KUINUKA KWA AJILI YA UCHAGUZI, NA WAKIINUKA BASI WATAKUTANA NA MAMBA ATAWALA HUKU ANALIA.

    MIMI NASUBIRI USHAHIDI TU, NAIPENDA ZANZIBAR LAKINI…

  8. Junior 18/07/2010 kwa 6:38 um ·

    SALAAM WAZALENDO,

    Kwa upande wngu nahisi ni vyema kabisa kuunga mkono maandishi ya MKARAFUU kua tusahau yaliopita na tugange yajayo, M/Mungu amesema “kisasi ni haki” tena akweka mipaka yake kua pua kwa pua, sikio kwa sikio n.k ila Mungu hyu hyu amesema kusamehe n bora zaid na huwezi kumuhukkumu Binaadam mwenzio kabla hajafa huwezi jua km ametubia na Allah almighty amemkubalia. Nampongeza Kificho kwa uamuzi wake ikiwa kweli rohoni yuko hivyo.
    MUNGU IBARIKI ZENJI NA WATU WAKE.
    EIMEN.

  9. mfurukutwa 18/07/2010 kwa 6:47 um ·

    @KwaoMtu:
    Inaonekana kuwa wasiwasi wako upo kwenye magubegube ya CCM ambayo yanajengwa na historia ya chaguzi zilizopita! Nahisi uondoe wasiwasi juu ya kura ya maoni. Ingekuwa bora ukampongeza Bw. Kificho kwa kauli yake. Hata kama yeye ataamua abadilishe msimamo wake basi kura watu watapiga na SUK itaundwa. Vyenginevyo nisingekupinga ikiwa ungeonyesha kuwa una wasiwasi juu ya matokeo ya uchaguzi mkuu; kwa hili CCM wapo smart na washalivalia njuga, na mara hii watalikamilisha kwa njia za kitaalam na ustaarab zaidi!

  10. Salmin Kiluwa 18/07/2010 kwa 7:50 um ·

    Nashindwa kuwafahamu ndugu zangu. Mtu asiposema mnafiki. Leo Mwenye Ez Mungu kampa fahamu ya kujuwa kwamba huku ndio kwenye kheri mnamwita mnafiki. Jee tutakwenda hivi? Hii ni Zanzibar nyengine sasa na mabadiliko hayaji ghafla. Hawa watu wana mambo mengi likiwemo lile la woga wao wasipoteze mafao kwa wananchi wao. Hivyo wapeni time kidogo lakini wakiingia katika upande ulionyooka basi wapokeeni kwa mikono miwili musiwanyanyase, na inshaallah Mwenye Ez Mungu atawasaidia (AMIN)
    Kiluwa

  11. mtu kwao 18/07/2010 kwa 8:59 um ·

    A.aalaykum Mimi naona serikali ya umoja haijaundwa mnaa za kuwaambia wanafiq kwa maana hiyo hamuwaamini kwaninimnataka kukaa nao pamoja hao wanafiq!si bora kila mtu awe kivyale vyake..Mimi nilikua nataka ndio kwa Hali hii ninayoiyona kwa nyie ndugu zetu vichwa ngumu sitii Tena natia hapana msije mkaja kupaka ikulu mava ha ha ha ha

  12. muhimu 18/07/2010 kwa 9:03 um ·

    ahh nyie ndo mumekuja kuomba uoo mseto tukakubalieni tupige kura ya maoni leo nyie nyie munakuja kusema watu wanafik sasa ndugu zangu hasa munataka nini au tuwe tunakuja kuwalisha kwa vijiko kila siku asubuhi majumbani kwenu kial tunalojitahid baya kwenuu sijui tuafanye nini sasa

  13. zenjiboy 19/07/2010 kwa 12:00 mu ·

    hahahaaa, muhimu kwa kujidai! Hebu twambie ndani ya CCM wewe unapata nini? cheo chako ni kipi?

    Jamani nakuombeni tuwe na hikma wakati mwengine. Hii imezidi, kila kitu unafik, basi Mh Kificho aseme nini ili leo aonekane mtu. Watu hawahukumiwi kwa yaliyopita. Hata Dk Amani na Maalim Seif wenyewe walisema tusahau yaliyopita tujenge Zanzibar mpya, na huu ndio msingi wa maridhiano na hiyo kura ya maoni yenyewe. Sasa kama leo mtu anajitahidi kutoa msimamo wake, tena spika ambae atakuwa ufunguo kwa wale wawakilishi wa CCM walio woga anasema hivi tunamwita mnafiki kwa sababu tu alikuwa sehemu ya yaliyopita. Basi kama ni hvyo inabidi CCM wote akiwemo Rais Amani wapige kampeni ya HAPANA, jee hiyo itakuwa nzuri Bw/Bibi kwaomtu. Mbona kila siku tunamlaumu Dr Bialal kwa ukimya wake juu ya swala hili?

    Naomba pia tusiwahukumu CCM sasa hivi kama wataiba kura ya maoni na hata ya uchaguzi mkuu. Ni kweli tukiangalia historia hawaaminiki, ni kweli kama bara hawako tayari, lakini mambo yanakwenda kwa mipango ya Allah tu hakuna wa kumpinga.

    • muhimu 19/07/2010 kwa 5:49 um ·

      kwani nyie cuf nyote muna vyeoo ndani ya chama chenu ?

  14. al-akhi 19/07/2010 kwa 12:06 mu ·

    @ wachangiaji
    Mapungufu yapo kwa kila binadamu na kukosa ni sehemu ya ubinadamu pia.Kila mmoja ni shahidi wa huko Zanzibar inatoka,hakuna ambaye hakuguswa na hayo yaliyotokea,awe mfuasi wa chama au vyenginevyo.Bila shaka mambo huzidiana na wako ambao wanaguswa zaidi kwa majeraha au ulemavu walioupata.Hayo yatabaki kuwa sehemu ya historia.Wa kusamehe asamehe na yule aliyekosa aombe msamaha huu ndio wakati.Ni vyema basi tutumie nafasi hii kutoa michango ya kuelekeza zaidi namna ya kujenga zaidi badala ya kila wakati kujivunja moyo kwa kudhani kuwa haiwezekani.Ni suala la uamuzi tu,tunaweza.
    NAMI NA UUNGANA NA WENYE KURA KWA KUWAOMBA PIGENI NDIO JULAI 31.

  15. popobawa 19/07/2010 kwa 1:20 mu ·

    Haya tayari Mh. Kificho ametoka mafichoni na kuingia uwanjani wazi wazi kuungana na wazanzibari wengine. Nyinyi akina Nahodha bado ndio mnakimbilia huko msituni alikotoka Kificho. Muulizeni amegundua nini katika maficho hayo?

  16. binamu 19/07/2010 kwa 1:53 mu ·

    UNAJUA SIKU ZOTE UKITAFUNWA NA NYOKA UKIONA UNYASI TU UNASHTUKA, NAKUBALIANA NA YOTE YALIYOSEMWA NA WALIOTANGULIA HAPO, ILA HISTORIA INAONYESHA HATA FIRAUNA ALIPOIONA AHADI IMESHAMKABILI SI NAE ALIJIFANYA KUTAKA KUMKUBALI MUSSA? JEE ALIKUWA MUISLAMU NAE, TUNATAKIWA TUKISHAFANYA MAKKOSA NA KUTANABBAHI BASI HARAKA TURUDI KWA KUTUBU NA SIO TU KUSEMA NIMETUBU LAKINI UJUTIE KWA ULOYAAFANYA NA KUDHAMIRIAA KUTOREJEA, HAWA WATU NI KWA SABABU TU WAANAONA SASA YANAWAAACHA NDIO NAO WANAJIFANYA KUYAWACHA. HATA HIVYO KWA KUWA SISI TUMEITWA INSI BINNISYANI KWAMBA TUMENASABISHWA NA KUSAHAU, BASI UKWELI WA TOBA YAO TUTAUONA KAATIKA HIZI CHAGUZI ZINAZOFATA. MIMI KWA IMANI YANGU NA KHOFU YANGU AMA NISEME MACHUNU YA MAADONDA YANGU NITAWAAMINI TU NA KUWASAMEHE ENDAPO NITAAGUNDUA KUWA WAMEFANYISHA CHAGUZI ZOTE MBILI KWA HAKI NA AMANI, NA WALA NISIELEWEKE KUWA NI LAZIMA KKISHINDE CHAMA FULANI, BAHATI MIMI SI MWANACHAAMA WA CHAMA CHOCHOTE, CHAMA CHANGU MIMI NI HAKI, UMOJA, USAWA NA MAENDELEO.
    WENGINE HUSSEMA NAHNU SAMI’NA WA’SWAANA NAA WENGINE HUSEMA SAMI’NA WA’ATWAANA, YAANI TUMESIKIA NA LAKINI TUTAASI/HATUTATEKELEZA NA WENGINE TUMESIKIA NA TUTATEKELEZA, HAPPO NDIPO PALIPO NA KIPIMO CHA MNAFIKI.
    MUNGU IBARIKI ZANZIBAR.

  17. brenda 19/07/2010 kwa 4:12 mu ·

    Ingelikua M/Mungu alitaka engeliwafanya watu wote wakawa kitu kimoja na wote wakawa waislam,lakini kawafanya watu rangi, makabila,dini, sura, tabia mbali mbali, ili mupate kutambuana, ana hikma zake aliposema ili mupate kutambuana, namshughulikia mgonjwa mmoja mwenye asili ya kipolish, bibi huyu alichukuliwa na wajerumani alipokua na miaka 19 kwenda germany kufanya kazi yenye kipato kidogo au siku nyengine bure, chakula kilikua cha shida, na hali ilikua ya ubaguzi sana. huo ulikua ni utawala wa Hitler na watu wengi nafikiri wanaelewa story yake.kulikua na watoto walemavu kibao kutokana na mabomu na vita. basi mtawala yule aliwaona kama uchafu mkubwa kwenye taifa lake, aliwatangazia watoto wote walemavu wapelekwe kuonana na daktari fulani, matokezeo yake mamia ya watoto walitiwa ndani wakaaambiwa wavuliwe nguo wakogeshwe kwanza, kumbe walifunguliwa mifereji ya gesi na kuuliwa hapo hapo bibi huyu akishuhudia, na wanaume wengine pia na wao waliuliwa kama hivo.maasi juu ya maasi.lakini matokezeo yake Hitler yuko wapi?. hata kaburi hana. hapa mashujaa hukumbukkwa kwa maua, mizinga, gwaride yeye hata siku aliyokufa haijulikani, hivo anaetaka kutubu wakati ndio huu, lakini ajute kwa aliyoyafanya, kisha atubu kweli kweli, sio kwa ajili yeyey ni bendera. huenda tukapata salama na utulivu. kusameheana ni uzuri, tujifunze kusamehe halafu tusahau [forget and forgive}[ ramadhani inakuja thawabu juu ya thawabu]ili tugange lijalo, vovote vile kilichoandikwa hakifutiki, tumuachie Mungu

  18. mtu kwao 19/07/2010 kwa 8:19 mu ·

    Asalaam alaaykum ….mimi sioni haja ya kuomba mtu samahani kwani kafanya nini kukaa madarakani ndio kosa mbona seif alikua waziri kiongozi aliwazulumu watu wa unguja haki zao aliwafukuza kazi na kuwakata mishahara na kuwanyima kwenda kusoma nje na aliwapa nafasi wapemba je? Aliomba radhi tusiangalie upande mmoja jamani na kubagua wewe unaemwambia mwenzio mnafiki wewe umetakasika huna dhambi au wewe mtume hatukujui?acheni blaa blaa chagieni mada acheni kuegemea upande mmoja

    • mrfroasty 19/07/2010 kwa 8:33 mu ·

      @mtu kwao
      Tuletee ushahidi wa watu kufukuzwa makazini katika uongozi wa Seif.That will be very interesting…

      Aidha ukitaka ushahidi wa watu waliofukuzwa makazini katika uongozi wa Salmin, huu hapa chini:

      1.Dr.Muchi – Alikuwa kiongozi wa project ya Malaria na Mnazi mmoja.Alisumbuliwa wakati wa Salmin, hadi CUF wakamfuata na kumuingiza kwenye siasa.
      2.Baba angu mimi personally amefukuzwa kazi, kisa na mkasa hakijulikani amekosa hata pension.
      3.Babu Duni amekosa haki zake zote nadhani…
      4…..orodha ndefu

      Kila la kheri na kutuletea ushahidi huo wa Seif kufukuza watu makazini.

    • zenjiboy 19/07/2010 kwa 8:51 mu ·

      @mtu kwao
      Nami naungana mkono na mrfroasty,
      Tuletee majina ya watu waliofukuzwa kazi wakati Maalim Seif ni Waziri Kiongozi. Naomba orodha iwe na:
      1. Jina, 2. Idara aliyokuwa akifanya kazi, 3. Tarehe aliyofukuzwa kazi, 4. Sababu iliyoelezwa ndani ya barua yake.

      Nadhani wakati wa Salmini wewe mwenyewe ni shahidi wa watu kufukuzwa kazi na wanafunzi kufukuzwa skuli pamoja na wengine kunyimwa nafasi za kwenda kusoma. Naamini humu ndani ya mtandao angalau asilimia 50 ya wasomaji wameathirika kwa namna moja au nyengine na kadhia za Salmin, na Bilali na master mind wao Shamhuna.

      Tukija katika mada, tunaomba msimamo wa Dr Bilali na Nahodha, tuna hamu tuwajue msimamo wao hadaharani wasipite chini kwa chini kupakaza sumu tu!

  19. Mznz 19/07/2010 kwa 10:33 mu ·

    ALLAH HUMA ANTA SALAM WAMINKA SALAM TABAARAKTA YA DHALJALAAL WAL-IKRAM

  20. Mznz 19/07/2010 kwa 10:34 mu ·

    INNAA LILLAH WAINNA ILAYHI RAAJIWUUN

  21. Mznz 19/07/2010 kwa 10:36 mu ·

    Ni msiba kumbe hivi ndivo Wazanzibari walivogawanyikaaa!!! mama miaaaa!!! huu msibaaaa tena sio mdogo.

  22. Heart 19/07/2010 kwa 1:29 um ·

    mimi sipo kabisa kuchangia mada ya hapo juu, ila kwa maneno machache nawapongeza viongozi wote wanaoweka hadharani kuunga mkono kura ya NDIO kwa SUT kwani ni hawa hawa kule nyuma walikataa na kupinga umoja huu. Hongereni kwani sasa Zanzibar kumepambazuka.

    Sasa niende kwenye makusudio yangu, Niliona mada moja hapo juu baada ya hii YA MHS Spika nilipofungua Mtandao huu ilikuwa na kichwa cha habari SIRI YA MAALIM SEIF NA AMANI IMEFICHUKA KUTOKANA NA MAKUBALIANO YAO YA GHAFLA walitaka kushitakiwa mahakama ya kimataifa kule Hague Uholanzi.

    Nilipotaka kuingia kwa undani ilipotea ghafla na sikuiona tena na nikambiwa habari hii haipo mtandaoni. Jee wataalamu hii habari ilikuwepo mukaifuta au kuna tatizo la kiufundi limejitokeza? Naomba jibu Administrater.

  23. stonetown 19/07/2010 kwa 2:45 um ·

    @Heart
    Assalamu alaykum.

    http://www.mzalendo.net/?s=SIRI+YA+MAALIM+SEIF+NA+AMANI+IMEFICHUKA

  24. Heart 20/07/2010 kwa 6:48 um ·

    W’msalaam.

    Ahsante sana Stonetonwn nimeisoma habari hii, nashukuru kwa ushirikiano wako.

Comments are now closed for this article.