Habari

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 26 April, 1964.

Ameandika Mohamed Aliy

Mtazamo wangu kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, 26 April, 1964.

Tanganyika na Zanzibar, tumerudi nyuma, badala ya kwenda mbele kama nchi mbili huru zilizokuwa na lengo la kujenga ustawi wa watu wake na kuenzi uhuru uliopatikana kwa gharama kubwa.

Muungano umezima KIU ya Wazanzibar kuona wanakuwa huru, badala yake Muungano katika kila hatua umeonekana kuhatarisha Uhuru wa mshirika mmoja wa Muungano “Zanzibar”, Zanzibar imejikuta ikilazimishwa kusalimisha kila kilicho chake kupitia kiini macho cha “Muungano”

Muungano umerudisha nyuma juhudi za kujenga demokrasia ya kweli kwa kuruhusu Viongozi wa Tanganyika kuzima majaribio ya Wazanzibari kuchagua Viongozi wanaowataka kwa kuingilia chaguzi ati kwa kisingizio cha kulinda Muungano. Chaguzi zote kuanzia ule wa 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 zinatupa ushahidi wa wazi.

Vyovyote iwavyo, fikra za miaka 53 iliyopita haziwezi kutumika kuzima juhudi za kizazi kipya, Muungano utaendelea kuhojiwa, na hatimae mbinyo unaoendelea kufanywa na watawala kwa kisingizo cha kulinda Muungano utazidi kuwaunganisha raia wa Tanganyika na Zanzibar.

Zanzibar itarudi katika nafasi yake,
Demokrasia itatuunganisha kuamua aina ya mahusiano tunayoyataka nje ya Muungano huu tulionao sasa

#ZANZIBARKWANZA

Share: