Habari

Prof.Lipumba aba Msaada kwa Bolozi Seif Ali iddi

IMG_6508

Balozi Sefu Ali Iddi ambaye anaongoza zoezi la kukifanyia hujma Chama cha Wananchi CUF akishirikiana na Prof. Lipumba jana ametwishwa zigo zito na Prof. Lipumba katika kufanikisha njama za kukifanyia hujma Chama cha Wananchi CUF.

Zigo hilo alilotwishwa Balozi Sefu na Prof. Lipumba ni pamoja na kutakiwa kutoa ulinzi wa Vikosi vya SMZ, Mahitaji ya kila siku ya kundi hilo la Prof. Lipumba, Magari mawili ya Washawasha, na FFU gari 4.

Zigo hilo limekuja baada ya Prof. Lipumba kumwambia Balozi Sefu kwamba ni lazima waandaliwe mazingira mazuri ya usalama wa maisha yao na kumueleza kua sio jambo jepesi kwa sasa kufanya mavamizi katika Ofisi za Makao Makuu yaliopo Mtendeni kwa kile alichaodai Prof. Lipumba kua lolote linaweza kutokezea na kusababisha hata kupoteza maisha yao hasa kwa kuzingatia mazingira ya kisisasa ya sasa ya Visiwa hivyo.

Prof. Lipumba amemwambia Balozi Sefu kua Wazanzibari kwa sasa wana hasira kutokana na kuporwa kwa haki yao ya Uchaguzi wa tarehe 25 October hivyo ni lazima aandae mazingira rahisi zaidi ya kuwawezesha wao kufanya kile wanachokipanga pasi na kufikwa na matatizo. Katika kukazia hilo Prof. Lipumba amemtaka Balozi Sefu kuhakikisha kua anaandaa mazingira ya Vita ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vikosi vya SMZ dhidi ya Wananchi kabla ya wao kuvamia maeneo hayo. Jeshi la Polisi na Vikosi vya SMZ vifanye kazi ya kupambana na raia kabla ndipo wao baadae wafanye mavamizi na ulinzi mkali nyuma yao.

Katika hatua nyengine mambo sio shwari kwa upande wa kundi hilo la Prof. Lipumba hasa kwa Wakurugenzi walioteuliwa hivi karibuni na Prof. Lipumba.

Familia ya Nassor Sefu ambae ni mmoja wa Wakurugenzi hao imetuma mjumbe kutoka katika familia yao kuja kukieleza Chama cha Wananchi CUF kinachoongozwa na Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad kua familia hiyo haiko pamoja na Nassor Sefu na haiungi mkono mambo yanayofanywa na Mtoto wao huyo.

Wazazi wa Nassor Sefu wamesema kupitia mjumbe wao huyo aliekuja Makao Makuu akitokea Pemba kua tayari wameshamwambia Nassor Sefu kwamba hawako pamoja na yeye na hawatoshirikiana nae katika jambo lolote linalomuhusu. Wazazi hao wameenda mbali zaidi na kusema kua wamemwambia Nassor Sefu pia akifa atafute pa kuzikwa.

Haya yanajiri kipindi ambacho Chama cha Wananchi CUF kiko ukingoni kuishika Serikali jambo ambalo linawashangaza Watanzania wengi hasa Wazanzibari na kuamini kua kundi hilo linaloongozwa na Prof. Lipumba lilikua tawi la CCM lililojificha kwa mda mrefu ndani ya Chama cha Wananchi CUF.

Share: