Habari

Risasi na mabomu yarindima Kangagani usiku huu

Kuna taarifa za kuaminika kuwa milio ya risasi na mabomu imekuwa ikisikika huko Kangagani Pemba. Hali hii imewafanya wakaazi wa Kangagani usiku huu kuyakimbia majumba yao na kukimbilia misituni kupata manusura.

Chanzo cha hali hii ni wananchi kukataa kutajwa jina la Dr Shein kwenye khutba ya Ijumaa.

Tokea mchana wakati wa swala ya Ijumaa hali imekuwa tete kwa wakati wa Kangagani ambapo waliswali Ijumaa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi huku mkuu wa mkoa wa kaskazini na mkuu ya wete wote wakihudhuria.

Wiki iliyopita vijana 7 wamekamatwa na polisi hadi leo hii bado wako mahabusu.

Bado haijajulikanwa ni watu wangapi wameumia kwenye mashambulizi haya, lakini inasemekana majeruhi ni wengi. Pia haijulikani hadi sasa ni watu wangapi wamekamatwa.

Share: