Sauti:Mahojiano na M.Seif – Umoja wa kitaifa
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 28/07/2010 // Sauti // 23 Comments
Ikiwa zimebakia siku tatu kabla ya kufanyika kura ya maoni kuwauliza wazanzibari iwapo wanataka yawepo au la mabadiliko katika muundo wa serikali ambapo kutakuwa na serikali ya umoja wa kitaifa, kiongozi wa upinzani Maalim Seif Shariff Hamad amesema mchakato huo umewkua ukienda vizuri.
Hata hivyo Hamad alisema amefanya kazi kubwa ili kujenga mazingira ya hoja hiyo kuungwa mkono na wazanzibari wengi kwa kuwa na ridhaa nzito zaidi. akizungumza na mwandishi wetu wa zanzibar Ally Saleh alisema angetamani kura za ndio zifikie thuluthi mbili ili kumaliza tatizo la mgawanyiko wa kisiasa wa wazanzibari.






23 Comments on "Sauti:Mahojiano na M.Seif – Umoja wa kitaifa"
Hii ndio zamira yao na wanalijuwa kabisa kuwa watu wana shida na ndio maana wakioneshwa pesa kidogo tu.basi akili inamchemka na mapigo ya moyo yanakwenda mbio.inafika saaanyengine mtu unashinda hata mlo mmoja kwa siku nzima .jee akionesshwa pesa za kunywa sheerbati na juwa lilivo kali hana budi kuuza kipande chake.Mimi naamini kuna watu ni wazanzibar lakini hata ukimuuliza waziri wa afya ni nani basi hata hamjuwi.
Ok ndugu mwananchi tiya kura yako ya NDIO upate kujihisi kama na wewe binaadam.nnakuwombeni mutie kura ya ndio halafu subirini muda mdogo tu mutaona matunda ya faida yake .naamini kuna watu wataliya machozi kwa kupoteza muda wote bure.kwa hivo kazi kwako. mwananchi wengi wetu tumeijuwa nchi yetu vipi hasa ilivo teseka bada ya kuwa wakimbizi na ndio maana tunasema weka ya ndio.
WEKA NDIO
Kwa maoni yangu napenda kuwapongeza kwa wale wote wanaotoa fedha ili kuwahadaa wazanzibari watie kura ya hapana.
Nadhani ukiangalia kwa undani utakuta hao wanaotoa fedha kuwapa baadhi ya wazanzibari ili kutia kura ya hapana ni wale wanaoungana mkono na viongozi wa Tanganyika waliosema kua zanzibar sio nnchi ili wathibitishe usemi wao na kuifanya zanzibar ni mkoa ili waendelee kuitawala na kuinyang’anya zaid hadhi yake na mamlaka yake.
Kwa Ushauri wangu na kwa vile hali ya kiuchumi,umasikini na ugumu wa kimaisha visiwani zanzibar!
Mzanzibari yeyote atakae pata bahati ya kupewa pesa na mtu wa aina yeyote ili aweke kura ya hapana katika serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar! Pesa achukue na azile bila wasiwasi wowote, hio ni haki yake ni mali ya wazanzibari.
Baada ya hapo kura ya ndio ni siri yake na hakuna atakae tambua kua kaweka ndio au hapana. Kwani mzanzibari yeyote anafahamu wazanzibari walipofikishwa na serikali ya tanganyika na ilioko madarakani kwa muda huu mpaka hii leo.
WEKA KURA YA NDIO.
Nawasilisha
InshaAllah Wazanzibar tuungane, pamoja na kuwa kuna madai ya baadhi ya watu kuunga ambao wanashindwa kujitokeza kusema HAPANA lakini wanagumia the so called ‘Sauti ya Kisonge’ Kwa Mzazamo wangu tayari watu hawa kwa uwezo wa Allah inaonekana wameshindwa kabisa na ndio maana wanashindwa kujitokeza. InshaAllah sala na dua za pamoja ziendelee na Mwenyezi Mungu atatupa ushindi wa kuza za NDIYO kwa zaidi ya asilimia 79%. Tuachane kabisa na hao Wadanganyifu, na hawana uwezo wowote hao mbela ya Allah! Wanatapatapa, na mara nyingi ukiona mgonjwa anatapa tapa basi ndio hata tena lake ndio yuko katika safari ya sakaratul mauti. Kwa hivyo, binafsi nahisi tushikamane hao watasambaratika wenyewe tarhe 31 July kwa uwezo wa Allah! Yaa Allah..Yaa Allah …Yaa Allah! Wewe ndio Mola Wetu! Wewe ndio Moal wa Kila Kitu! Wewe ndio Tunaekutegemea! Wewe ndio Tuaekuabudu! Wewe ndio Unaejua ya Dhahiri na Siri! Wewe ndio Muongozaji na Mtendaji! Wewe ndio Unaposema Liwe, Huwa au Unaposema Lisewe, Haliwi kwa Idhini yako! YAA ALLAH TUNAKUOMBA KWA KILA JINA LAKO TUKUFU ULILOJIITA UIFANYE SAUTI YETU YA NDIO KATIKA KURA HII YA MAONI IWE NI KAULI YA WAZANZIBARI WOTE NA YOYOTE ATAKAYE KWENDA KINYUME NA SAUTI YA KURA YA NDIO IZIME KAULI HIYO KWA CHINI YA WALIOCHINI ILI TUDUMISHE UMOJA, MAPENZI NA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WANAADAMU WAKO WA ZANZIBAR …AMINI AMINI!
dah!inshallah allah atusalim salama ikiwa watu wanafikia kutumia fedha kuwarubuni watu wapige kura ya hapana hiyo ni kuliko hatari na inatisha kwa hakika,ni ubaya wa kupindukia haiwezekani watu wafikie mpaka kutumia fedha bure bure yarabi tunusuru hapa inaonesha kuna jambo kubwa limekusudiwa.itabidi tumuelekee allah kwa visimamo vya usiku tumuombe sana atunusuru na shari ilokusudiwa, na yoyote alokuwa haitakii mema zanzibar basi allah atampa la kumpa.
demokrasia kweli kama alivyozungumza maalim mtu anayo haki ya kukubali au kupinga lakini kwanini watu watumie fedha kuwashawishi wengine kupinga, twambieni mnakusudia nini khasa? hawa watu watakua wametumwa kuja kutuvuruga na hiyo hoja waliokuja nayo ya kuwatisha watu si ya msingi kabisa na haiingii akilini eti kura ya ndio ikatupeleke serikali moja,hapana ndio kuikubali serikali moja kwani ndio sera ya chama tawala na kwa maana hiyo kura ya ndio inaonekana kuogopewa sana kwa vile ni biashara ilokuwa haijakamilika(unfinished bussiness)kwa miaka yote tuloiwekea mikakati ya kuitia mkononi na sasa dakika za mwisho zanzibar inaelekea kutuponyoka hawa watu msifikiri watatuacha hivi hivi lakini kwa uwezo wa allah inshallah atatuokoa amin.
watu wanapomuelekea Mungu basi haitakiwi kujifanya wengine ndio watabiri, au kua wanajua sana. kwakua watu wanatanguliza sala chakuomba ni dua zetu zipokelewe na kila anaekwenda kinyume na dua zile basi arudi yeye ki nyume nyume….kwani bwana ukwelitu hujalia wewe bado?maana sisi wenziwe tumo kilioni miaka mingi, ulikuwepo wapi wewe hata usilie kwa dhiki,shida, njaa, maradhi, uonevu, chuki, ubinafsi, dharau, ubaguzi ,na mengi mengine?au wewe sio mzanzibari mwenzetu? maana hata hizi kompyuta mpaka leo watu wengine hawana majumbani mwao na hawapati kuona mambo kama haya ambayo wewe unaona….kwa hivyo mimi nakushangaa kuwambia watu watalia ….ni sawa sawa na kupepea mwiku. labda wewe unaposho kubwa unapata somewhere so u can not feel joto la wazanzibari ni aibu mtu kama wewe kusema hivyo,mimi nafikiria ni chuki au ni choyo kinachokuchoma moyo……wazanzibari nendeni waacheni wakosefu wa imani na nchi yao hawawezekani hao
SALAM ALEIKUM
NAPENDA KUMPONGEZA MAALIM KWA MAHIJIANO HAYA NAMTAKIA KILA LAKHERI KATIKA KURA YA MAONI WAFANIKIWE HIYO ASLIMIA WANAYO ITAKA INSHAAAL
KITU CHENGINE KILINICHO NIFURAHISHA KATIKA MAHOJIANO HAYA KUNA SOMO KUBWA KALITOA MAALIM KATIKA MAHOJIANO HAYA , NALO NI MAANA HALISI YA DEMOKRAS MIMI NADHANI TUJICHUKULIE HILI SOMO KWAHAPA KATIKA MTANDAO WETU MZURI WA MAZALENDO,
INAPOTOKEA MTU KUWA KINYUME NAHOJA ILIYOTOWA TUWENAWYE KWAKARIBU SANA NA SIO KUMBEZA NA KUMDHARAU ,KWANI HIYO PIA NIHAKI YAKE KIDOMOKRASI
NADHANI HAPA UONGOZI WA MZALENDO INGEPATA SOMO TOSHA KUPITIA KWA MAHOJIANO HAYA KWA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD NINI MAANA HALISI YA DEMOKRASI, HASA RAFIKI ZANGU KINA
@ MZEE OLE
@ MRFOASTY
@ ASHAKH
NAKUTAKIENI KAZI NJEMA
MR BANDA MWENYEWE
NAOBMA NISIJE KUTAFSIRIWA VIBAYA MIE MSIMAMO WANGU KW KURA YA MAONAI NI NDIO NDIO NDIO
ASANTENI
watu wote wanajitahidi kuweka mazingara safi ya mandhari yawazanzibari lakini watu wajiulize kabla hayajawekwa hayo mazingara ni nini cha muhimu tunahitaji kwanza ili kupata piece of mind{elimu, matibabu, kazi, barabara,na ile heshima yetu n.k]jee tunayo hayo?hatuyapati ila tupige kura ya ndio
@Banda,
Demokrasia ya kupigania sera ya CCM “Serekali mbili kuelekea moja = (Zanzibar kuwa mkoa wa pwani)”.Ni bora ukaniita mie dikteta au kheri uniambie mwanzoni kama unapigania tumbo tunaweza fahamiana vizuri.
You can do better than that….
usingizi wangu ulikuwa wa mapande mapande hii habar ya watu kutumia fedha kwa kweli imenishtua sana na kama maalim alivyosema hii ni hatari,hapo hatari ina maana kubwa mie sitoamini kuwa wazanzibari wenyewe wataikataa serikali ya pamoja kama wapo watakaopinga itakuwa ni kidogo watu washakua wamaji kwa hali inavyokwenda hivi sasa lakini hatari yenyewe pasije pakapitapita hila na mbinu ya kuja kufanyiwa dhulma kwenye matokeo. maana unashindwa khasa kujua nia za watu vifuani mwao, wengi wa viongozi wanadhihirisha kuunga mkono lakini hatuwajui katika nafsi zao wako vipi,na huku wanakwenda mbio za chinichini mpaka kufikia kutoa fedha kwa watu. hapa kuna siri iliofichika lakini wakae wakifahamu yoyote atakaeshiriki kuihujumu zanzibar na watu wake atakua amebeba dhulma kubwa na hatma yake itakuwa mbaya mbele ya Allah. watu wanaweza wakala hizo pesa hiyo itakuwa bahashishi yao kwa kusuguliwa roho zao lakini wakitoka hapo watie kura ya ndio kwa kuinusuru zanzibar na inshallah Allah atakuwa pamoja nasi amin.
@ Banda,usiwe na wasiwasi tuko pamoja ndugu.
Tatizo ni lugha kushindwa kuitafsiri demokrasia maana yake. Leo hii unaweza ukatoa maana halisi yademokrasia na ikasibu. Ikazishinda zile zote zilizotolewa kabla yake.
Tukija kwenye maelezo ya Maalim kiasi umpongeze kwa sababu hakusema pumba. Kama vile wewe ulivyokuwa hukusema pumba hakuna aliyekudharau. Wala usikiri kwa sababu ya kumpongeza, unaweza kumpinga na watu wakaridhia. Mfano juzi, taymia pamoja na mimi tulipinga hotuba yake aliposema, kuna mengine mengi tatayapigia kura ya maoni. Hakuna alichukua hoja tuliyoitoa na waziwazi tulimpinga Maalim.
Ubaya ni namna ya upingaji na hoja zako zako. Hapo Maalim amesema pamoja na kuwa wapingaji wa kura ya maoni nihaki yao kupinga, watafute njia za kupingia.
banda na ashakh basi tena haifai hivyo kurudia mambo ya nyuma,hapa tutizame la usononi kwetu linalotukabil ndo jambo la muhimu.
WALE WOTE WANAOBEZA MSIMAMO WACHAMA CHETU CHA CCM KHUSUSAN WATU WAKISONGE NAWALE WAFADHILI WAO AMBAO WENGINE WANA NYADHIFA KUBWA NDANI YA CHAMA NA SERIKALI WAWE TAYARI KUYAPOKEA MABADILIKO YA KISIASA 31 JULY INSHAALLAH. NAWAFAHAM KEJELI ZAO JUU YAWAKUU WETU WA CCM TUNAZIFAHAM NAWAO TUNAWAFAHAM NACHAMA KITACHUKUA HATUA ZAKINIDHAMU MARA TU BAADA YA MATOKEO YAKURA YAMAONI.
mkifanya hivyo tutafurahi sana ili tuthibitishe kama CCM pia ipo kwa ajili ya Zanzbiar si Tanganyika tu. inshaAllah kher siku ya Jumamosi.
Ni juzi tu, nilisema hakuna ubaya kupinga hii serikali ya umoja wa kitaifa. Lakini iwe kwa nia njema. Nikasema kwamba ingekuwa vizuri, hawa wanao pinga na wao wakatupa sababu zao za msingi, moja, mbili, tatu… ikisha na sisi tuka tafakari.
Kusema wana siasa wetu ambao wanapinga hawaja tufanyia haki kwa hili. Tulitegemea wao kama wana siasa ni watu wanaona mbali, kwa hiyo ndio inakuwa dira yetu kwenye maamuzi makubwa makubwa kama haya. Mimi leo ukinipa katiba, basi nitadodosa tu ama nitasoma tu kama kasuku.
Kama mtu hakupewa jukwaa, kwanini asiseme mimi kama mtu fulani, napingana na hili wazo na sababu zangu ni hizi. Nani atamlaani kwa hilo? Kwa hiyo si kweli kama hawa watu hawaja pewa majukwaa. Tumesha sikia wawakilishi wengi wakisema kuwa wao wanaunga mkono, lakini wanaogopa wasije kukosa kura, akaa wewe kweli muwakilishi? Au unajali tonge yako tu. UK kuna MP mmoja wa conservative David Davis, kuna wakati mmoja alikuwa anapingana na hoja fulani na kwasababu chama chake hakikuwa wazi kwa hilo, basi aliamua kujiuzulu Ubunge wake, baada ya mwezi mmoja uchaguzi ukafanywa, akarudi tena kwa wapiga kura wake wa jimbo. Na wao kwasababu walikuwa pamoja na yeye kwa maamuzi yake, wakamrejesha. kwa hiyo sasa hivi ni mbunge japo kuwa apepotezeza uwaziri kivuli wakati wakiwa upidhani na sasa hivi wameingia serikali amebakia kama mbunge tu. Tukiweka maslahi ya nchi na watu wake ambao ni sisi basi inshallah tutafanikiwa.
Nampenda Maalim Seif na siasa zake. Mara nyingi anapoingia kwenye uchaguzi, hupendelea kupata asilimia nzuri. Ili aweze kuwa na sauti pale anapo amua kitu. Na kwa hili tayari tuna uhakika wa kupita japo kwa asilimia ndogo, lakini nalo tayari kashaanza kuliangalia vizuri. anayo sema ni kweli, kuwa kupata asilimia 52% bado tatizo hatuja litatua. Kinadharia sasa hivi tunaweza kuona hali imekuwa shuari kwasababu ya maridhiano. Lakini ukweli hasa wa mambo upo kwenye kura ya maoni. Siku ya Jumamosi tuna mambo mawili matatu ya kuangalia. Moja ni ZEC, jee hawa watu wamekubali kujibadilisha na kulinda haki za watu. Kama kura ya ndio itakuwa ipo juu kwa asilimia hiyo asemayo Maalim Seif na mimi naomba ifike 80%, basi hapo tutaanza kujenga matumaini na kwa uchaguzi ujao. Kufanikiwa kufanya uchaguzi ulio hutu na haki, ndio kusema maridhiano yamefanikiwa na hapo ndipo tutakapo weza kujenga serikali iliyo safi ya umoja wa kitaifa.
Nakumbuka kwenye uchaguzi wa 1995 Maalim Seif kwenye kampeni zake alikuwa akisema kuwa kama atapata ridhaa ya kuingia serikalini kama Rais wa Zanzibar, basi yupo tayari kufanya kazi na mzanzibari yeyote, la muhimu ni mchapa kazi. Kulikuwa na fununu za hapa na pale mmoja ambaye angeweza kufanya naye kazi ni Said Bakari Jecha. Huyu alikuwa Shein Mwengine wa miaka ile. akitokezea mtu na kusema eti anataka kuingia serikalini kwa mlango wa nyuma, huyo ni mwandawaimu.
@mrfroasty @banda
hata mm nakuunga mkono ndugu banda maana ktk mtandano imezoeleka mawazo yafanane tu na yasipingane na wengine lazima uhuru wa demokrasia uwepo kila mmoja ana upeo wake wa kufikiri na kuchambua, kwa mfano mm jana nilitoa mawazo tofauti na wenza ngu lkn nikasakamwa sana na mr froasty pamoja na wengine na kuambiwa maneno ya kejeli na fedhuli kwamba mm ni mtangayika nimetumwa tu.. sasa kwa kweli hali kama hii ahileti picha nzuri .. mtu akitoa mawazo yake aheshimiwe au kama kuna mtu ana hoja tofauti na yy atoe na sio kumshambulia. ashante tuko pamoja hata mm naunga mkono kura ya NDIO NDIO NDIO KWA ZAZNIBAR YETU IFANIKIWE.
Hawa watu wanaogawa vijisenti wasiwarushe roho. Wanachokifanya ni kutapatapa roho wameona kuwa wananchi walio wengi wamefahamu maana ya kura hiyo na uwezekano wa kupita ni mkubwa.
Sijui watagawa pesa kiasi gani hata wawatosheleze raia wote. Hapa tutahadhari na kubambikiwa pesa feki. Mbinu zao ni dhaifu ni sawa na kutia sindano katika bahari ya Hindi.
Inshaallah kura itapita.
Mimi naona hao kwanza sio wazalendo wala hawaumwi na hii nchi na ndio maana wanahitaji kwa gharama zozote watu walipinge na kupigia kura ya hapana ili lao lifanikie. Lakini kwa maoni yangu ikiwa wewe ni mtu mwenye akili timamu na mwenye kuendeshwa na utu uzima wako baadala ya kusukumwa kama mtoto au kuendeshwa kwa remoti, nina uhakika hutokubali kuuza utu na haki yako kwa vijisenti ambavyo havikufikishi wala havikuhakikishii hata kula yako ya siku mbili. Jiulize wewe, yawaje mtu kama huyu atoe mpaka fedha zake akupe wewe ati nenda katie hapana, lazima ujiulize, ni kwa nini siku zote hajakupa akakwambia kuwa nakusaidia kama kweli ana imani na mapenzi nawe. Huko ni sawa na mtu kuja kumchumbia mwanao akiazima joho la kifahari na gari la kifahari ili tu umkubalie kumpa mwanao, kama utakuwa na akili timamu basi hutokuwa tayari kwa hilo. Ni kumuuza mwanao kwa ganda la njugu huko, thamini na jitukuze kwa hali yako.
Jamani, nakuamsheni waislamu na wananchi wenzangu:
Kwanza huko ni sawa na kukubali kuhongwa, hakuna kitu cha bure bure, jua kuwa kama alivyotumia fedha yake kukununua wewe na wewe ukakubali kununuliwa basi hata ukimridhia anajua kuwa atakukamua tena wewe wewe ili arejeshe fedha zake, ndugu yangu, huko ni kutumiwa mgongo wako kuvuukia bahari wakati ukizamishwa wewe muokowaji.
Kwa upande wa pili, nakutanabahisha nikiamini kuwa miongoni mwa munaopokea hivyo vijisenti ni waislamu, nasi tumetakiwa katika kitabu chetu kukumbushana, M/Mungu anasema, amemlaani mtoa rushwa, mpokeaji na mwenye kuchangia kati ya wawili hao, elewa kuwa kumbe hio hasara sio kwa hapa duniani tu lakini mpaka mbele ya hakki, tahadhar, maisha hayana garantii.
Na mwisho ikiwa umeshapokea na pengine kushatia kharamu mwilini mwako, kuwa mjasiri kama ndugu zetu wa kule kina yahe- Pemba, walipolishwa mahela na kina Mbaatia na Mrema wakitumai kuwa watawanunua wapemba na kuwapa majimbo, kinyume chake mtu hata ile kura yake mwenyewe mpokeaji wa lile nofu haikupatikana, Usikubali kuuza haki yako na kudhaalilisha utu wako. Hao wote wanaopiga kampeni hiyo hata hawajuulikani vyama vyao si CUF, si CCM bali ni popo hao.Kwa sababu kama vyama ndio vinavyowahamasisha, na viongozi hao hao walitamka hadharani, leo wanawapitia tena wafuasi wao wakiwa na kauli nyengine jueni kuwa munaongozwa naa wanafiki, na wanafiki ni wabaya kuliko wauwaji, kama ni kweli wana hoja kwa nini wasitamke hadharani. Mimi ningalikuwa kiongozi basi hao kwanza ningaliwavua uongozi na hata uwanachama, na baadae nikawatia katika kundi la wachochezi na kuwafunza siasa na uongozi ni nini. Tunataka kiongozi ambae anaweza na anajiamini kusimama popote na kutoa msimamo wake kwa anaowaongoza, awe muwazi sio ndumi la kuwili, watu kama hawa hata wakati wa Mtume walikuwako na ndio mpaka M/mungu akawataja kwenye quran kuwa wakiwa na wewe Muhammad husema sisi ni waumin wa Uislam na wakiwa na makafir wenzao husema hakika sisi tuko pamoja nanyi isipokuwa wale tunawacheza shere tu. OGOPA MNAFIKI HATA KAMA NI MZAZI WAKO-HAFAI
MTAZAMO WANGU NA MSHTUKO WANGU
Mimi nishaingiya wasi wasi wa kubadilishiwa box la ndio likawa siyo na siyo likawa ndio wezangu hapo mushapaona kwani hawa ccm sio. mimi mtoto wa muwakilishi lakini kwahili lililo fikiya hata baba yangu analiunga mkono na akisema kila leo kuwa yeye yake ni NDIO na wanawe wake wote waweke NDIO . lakini CCM matapeli wanakulana wenyewe kwa wenyewe seuze wewe mgeni. tujitahazari na sana kwa CCM vigogo
nAPENDA NIMTAHADHARISHE KIONGOZI ATAEPATA RIDHAA YA KUONGOZA KUWA NDANI YA KUNDI L KONDOO , WAMO PIA NA MBWA MWITU. HAWA VIONGOZI TULIONAO SASA AMBAO AMEWATEUA MWENYEWE RAIS KARUME NDIO HAWA HAWA WANAOMDHALILISHA NA KUMPINGA KWA GHARAMA ZOTE. NI DHAHIRI KUMBE MENGI ANGALIWEZA KUYAFANYA KARUME LAKINI KUTOKANA UTIMBAKWIRI WA WATU WAKE MWENYEWE WALIOKUWA WAKIMRAMBA KICHOGO WAMEMREJESHA NYUMA SANA, SASA HAPA IWE NI SEIF AU SHEIN HILI NI SOMO KWAO. IKIWA KWELI WANATAKA KUIBADILISHA ZNZ NA WAZANZIBAR KIMAENDELEO BASI WAWE MAKINI SANA KATIKA KUCHAGUA NANI AWE WAZIRI , KATIBU MKUU NA HATA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA. NINGALIKUWA NI KAMA MIMI SASA HIVI NINGALIKITUMIA SANA KIPINDI HIKI KUJUA NI NANI NITAWEZA KUFANYA NAE KAZI NA TUKAWA NA LENGO MOJA NA NANI NI KIBARAKA, AKICHEMKA KATIKA UTEUZI KWA KUWEKA MBELE MASLAHI YA KICHAMA KULIKO NCHI BASI KITAKACHOTOKEA ASIJE AKAMLAUMU MTU.
PILI KARUME TAYARI AMESHAJIFUNZA KWA MAKOSA ALIYOYAFANYA, SASA KAMA KWELI ANATAKA KUTUNZA HESHIMA YAKE INAYOPOROMOSHWA NA WALE ALIOKUWA AKIDHANI NI WENZAKE, BASI INABIDI AKAZE KAMBA KUHAKIKISHA UCHAGUZI UNAENDA WA HAKI ILI AMANI IPATIKANE. SOTE TUNAHUBIRI NENO LA AMANI LAKINI AKIKUJIA ADUI NA PANGA WEWE HUTOMPA MKONO BALI UTATAFUTA LAKO, NI KUSEMA IKIWA HIVI SASA YATARI MAZOWEZI YANAYOFANYWA YANAASHIRIA FAULU, RUSHWA, MIKUTANO YA SIRI SIRI , VIGENGE BASI NI WAZI KUWA YALE TUNAYOYAHUBIRI YAKO MBALI. kIONGOZI MMOJA ALISEMA TUKISHINDWA KIPINDI HIKI KUENDESHA UCHAGUZI KWA NJIA YA SALAMA NA AMANI BNASI TUJUE KUWA ZNZ ITAKUMBWA NA MACHAFUKO AMBAYO HAYAJAWAHI KUTOKEA. mUNGU ATUEPUSHE NAYO.
@Manyamba, Banda
Ujumbe umefika inshallah wazalendo tutajitahid…
Maasalaam,
mrfroasty
nasema tena matokeo ya hiyo mnayo iita kura ya maoni ambayo mimi siijuwi faida yake weeeegi wemepiga hapana lakini CCM wanaikubali ipitishwe kama tume ya nyalali vile ndio nikasema siioni fida yake na kama hamuamini subirini mwaka 2010 asanteni sana
@ Kijini
Mara kadhaa umekuwa ukiandika maoni ambayo ni ambiguos. Hayako wazi wala hayafahamiki. hebu jaribu kutueleza angalau nasisi wenzio tukuelewe.
Katika maoni yako inaonekana mpaka leo hujasikia au hujafahamu kuwa Zanzibar kuna kura ya maoni. Nakariri:
“..hiyo mnayo iita kura ya maoni ambayo mimi siijuwi faida yake..”
Sasa sijuwi ninani mwenye uwezo wa kukufahamisha kuwa hii inaitwa “kura ya maoni”. Pia faida zake ni kadhaa wa kadhaa.
Unaposema:
” weeeegi wemepiga hapana..”
Kwani imeshapigwa? Ninavyofahamu nikuwa kura ya maoni itapigwa siku ya Jumamosi tarehe 31/07/10. Labda mwenzetu unajuwa mengi zaidi,hebu twambie ilipigwa lini?
Unaposema:
“..lakini CCM wanaikubali ipitishwe kama tume ya nyalali..”
Kwani hii kura ya maoni itapigwana wana-CCM peke yao au ni Wazanzibar wote kwa jumla? Isiwe umechanganyikiwa, ukafikiri ni ule uteuzi wa wagombea ubunge na uwakilishi ndani ya CCM!! Tume ya Nyalali kila mmoja anafahamu, kwa maneno ya Mchonga nikuwa 20% walikubali, na 80% walikataa. Iweje hapa ufananishe hii kura ya maoni na Tume ya Nyalali?
Unasema:
“..kama hamuamini subirini mwaka 2010 asanteni sana”
Kijini uko dhahiri, hivi sasa tukokwenye huo mwaka 2010. Sasahili onyo lako linamnasaba gani na mwaka huo wa 2010? Hebu andika kitu wengi wafahamu. Lengo la kutoa maoni katika mzalendo ni kwa ajili ya kuuzndia umma. Ikiwa utabanabana kama hivihiyofaida itakuwa haipatikai.