Sauti:Zanzibar kubadili katiba kuunda serikali ya Umoja wa K
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 02/08/2010 // Sauti // 5 Comments
Baraza la wawakilishi Zanzibar linatarajiwa kukutana kuibadili katiba baada ya kura ya maoni kuunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa visiwani humo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.
Katika kura ya maoni iliyofaywa Visiwani Zanzibar, huko Tanzania, mwishoni mwa wiki kuwauliza wananchi kama wanataka katiba ya nchi yao ibadilishwe ili kuweko serekali ya Umoja wa taifa baada ya uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba mwaka huu, asilimia 66.4 ya wapiga kura walisema wanaunga mkono jambo hilo, na waliobakia walisema hawataki.
Hiyo ina maana Baraza la Wawakilishi visiwani humo litakutana kuibadilisha katiba ya Zanzibar ili kuweka njia wazi ya kuweko serikali ya Umoja wa taifa, huenda sana baina ya vyama vya CCM na CUF.
Othman Miraji alizungumza na mkuu wa upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hamad Rashid Mohammed, ambaye yumo katika uongozi wa Chama cha CUF.
Pia alizungumza na Harun Suleiman, waziri wa elimu wa Zanzibar, na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama tawala cha CCM.
Sikiliza mahojiano baina ya DW na Hamad Rashid Mohammed:
Sikiliza mahojiano baina ya DW na Harun Suleiman:
Repoti ya Salma Said,





5 Comments on "Sauti:Zanzibar kubadili katiba kuunda serikali ya Umoja wa K"
HAPA HAMAD RASHID YEYE AMEJIBU KIUNGWANA KABISA KAMA YEYE HAWEZI KUSEMA NANI ATASHINDA. LAKINI KWA MJOMBA WANGU HARUNI JAJE KANA MBILI VANO, YEYE ANASEMA CCM ITASHINDA, ALIPOULIZWA SUALA LA PILI JEE IKIWA CUF ITASHINDA CCM ITAKUBALI? AMEBAKIA NA KIGUGUMIZI,, EE HARUNI WE WCHA ZAKO HIZO MAMBO SASA YAMESHABADILIKA UKISHINDWA UTAKUBALI TU UKITAKA USITAKE.
MMOJA HUMU ALISEMA JOGOO AKIWIKA ASIWIKE ASUBUHI ITAINGIA TU.
Kwaomtu: haruni hawezi kusema au kulijibu hilo swali.kwani anaomuda kidogo wakuiba kwani wanalijuwa vema swalihilo jibu lake .sasa kazi ilio bakiya ni kuiba tu tayari washaujuwa mwisho wao wa kuganduka madarakani .panguwa panguwa inakuja .mtaiona ndoto ya jiwe.
NDIOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
A/A
@kwao mtu : tafadhali punguza maskhara unapotowa maoni ,hayo mambo unayondika ni kuwakejeli wa makunduchi na kuukejli ulimi wao ,ili kujenga zanzibar mpya lazima tuheshimiane
Mjomba wako haruna amesema kwa mujibu wa miongozo ya chama chake na kili yake inavyomtuma.kama utataka kuzungumzia kimakunduchi basi kiandike kama kinavyozungumzw
JAJE KANA MBILI VANO????????????????
kwa kweli sio mambo yote yatakayobadilika baada ya serikali ya mseto lakini nna kiswali kidogo.
hivi ZFA ni chama kinachofanya uchaguzi au ufalme?
kwa wale wasiojua maana ya ZFA ni
Z.zanzibar
F.football
A.assosiation.
nimeuliza hivi kwa sababu sina kumbukumbu za kufanya uchaguzi hivi karibuni
jee serikali iko wapi mda wote mpaka soka yetu imepotea ?
karibia miaka 10 sasa znz tumetoka kwenye midani ya soka kisingizio kikubwa hatumo fifa hilo mimi nalipinga kwani miaka ya 80 soka ilikuwa inatisha znz bila ya fifa.
wanzazibar mna litazama vipi suala hili ?
mimi kimtazamo wangu mdogo lawama zote nazitupa kwa serikali wewe unamtizamo je ?
Mimi naomba niekwe sawa hapa waungwana kuhusu haya marekebicho ya katiba.ikiwa makamo wapili wa Rais ambaye atatoka katika chama kilicho shinda nafasi ya Urais atakuwa ndie mshauri wa Rais na Shuhuli za serekali zote pamoja na shuhuli za Baraza la Uwakilishi? huyu makamo wakwanza ambaye ccm tayari wamesha jipangia ktk mawazo yao na mazingaombwe yao kuwa atatoka cuf kazi zake zitakuwa zipi Katika kuwahudumikia wananchi wa Zanzibar? Au ndio ccm wanataka kufanya ujanja wa kujikumbizia badaraka?