Sauti:Hoja ya Mh.Jussa – Baraza la wawakilishi
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 23/01/2012 // Habari, Sauti // 10 Comments
Ripoti ya DW-SW
Shukurani za dhati kwa Ashakh




10 Comments on "Sauti:Hoja ya Mh.Jussa – Baraza la wawakilishi"
Tujaalie Mh.Shamhuna hatojiuzulu kwa khiari (ambapo kwa mahesabu naweza sema asilimia au probability ni 0.99 itakuwa hivi).Kwa mara ya kwanza tokea nizaliwe, naona chombo hiki kikisimamia haki za wanyonge, badala ya kushangilia siasa.
Natoa pongezi kwa wote waliosimama upande wa utetezi wa Zanzibar na watu wake pamoja na vizazi vijavyo.Nasubiria kwa hamu kubwa kuona kifungu cha 37 cha Baraza kumpigia kura ya kutokuwa na imani makamu wa raisi (Balozi Seif).
Matumaini yangu ni kuwa baraza litachukua uamuzi huo mgumu, ambao utawapa nafasi ya uwakilishi mzuri wa ubunge kwa wananchi wa jimboni kwa Mh.Balozi Seif.Ni wazi Balozi Seif hana nafasi ya kuwakilisha wananchi katika bunge, anachofanya si uungwana kabisa kula kueka maslahi mbele ya kupokea mishahara bila ya kuitumikia ipasavyo!.
Wasalaam,
mrfroasty
@ Mrfroasty (Ufundi)
Tafadhali ukipata muda soma kwa makini sana maoni ya Babuji chini ya makala ilowekwa na suha yenye kichwa cha habari :Ombi la eneo la bahari kuu lapingwa.
@Babuji,
Nimeyaona hayo maoni, sio mara ya kwanza kuwa urais wa Zanzibar unakuwa unapatikana kwa njia hizi za kunyofoa madaraka/rasilimali zetu kuzihamishia Bara.Mifano iko mingi inayoonesha makubaliano ya siri kati ya Tanganyika na mgombea urais Zanzibar.
Karume mkubwa – muungano
Jumbe – ASP
……………….
Karume mdogo – TRA/Kodi
Shein – Mafuta ???
P:S
**Nimeskip mifano ya marais wa kati hapo na vitu walivyovitoa muhanga kwa ajili ya maslahi yao binafsi.Huu ni usaliti, na inshallah mwaka huu iwe mwisho!
Ushauri wangu kwa wawakilishi ni kutuletea kura ya maoni na kadhia hii ya muungano, tumeshachoshwa (si leo, tokea miaka 48 iliopita muungano ulitakuwa usiwepo!).
Sawa,
Leo naona Wazalendo kama vile zile ndoto zetu zinasadifu. Jee tunataka ushindani au tunataka upinzani?
Tokea awali niliona nuru za baraza letu zikichomza. Wako waliokuwa wakiona giza kwa vile walikuwa wamevaa miwani nyeusi. Hata wale waliokuwa wakiponda GNU na vyombo vyake kwa kutegemea myanya ya udhaifu, wameparama na kuufyata kimya.
Hata Mh Asha Bakar anayajuwa hayo, sikwambii Mh Hamza. Kesi kama hizi ndio inazomlazimisha Waziri au kiongozi kujiuzulu. Hapa unakuwa na sababu za msingi kufanya hivyo. Sio mtu mwengine kafanya kosa, adhabu atwishwe mwengine.
Zanzibar na muelekeo wa siasa mpya, nani haamini?
Tuendelee kujifunza kupambanua.
alhamdulillah , sasa napata matumaini kua zaznibar yaweza kua kama hong kong ,
mana ukiondoa mas’hara katika kazi basi kila ulichokipanga huenda sawa
a.alaykum wazalendo.
Tusimlaumu sana Shamhuna kwani haya ni mazowea kajisahau kma yumo ndani ya serikali ya UMOJA viongozi wote walopita mambo ndio haya hujiamulia mwenyewe mtu na wakaufyata ustaarabu wetu tunaona anaumia Seif na CUF YAKE laiti ingelikua baraza zilopita miaka yote hiyo tusingefika hapa leo tungekua mbali lakini wapi MIAKA 50 sasa ndio kwanza tunaanza kutambaa tulikuwa chali apitae apite tu donge la mfukoni laingia SEIF akajenge ikuluye mtambwe sasa tunaona raha ya umoja wanachomoza sasa inayowauma ZANZIBAR.
NIMEPENDA HII KAULI WALOTOA WACHANGIAJI WA HOJA. NANUKUU;
HII HOJA ISITIZAMWE KISIASA NA WALA ISITIZAMWE KAMA KAITOA NAIBU KATIBU WA CUF BALI IMETOLEWA NA MH JUSSA MWAKILISHI WA WANANCHI WA ZANZIBAR.
HONGERENI INSH TUKIWA WAMOJA TUTASHINDA KUIKOMBOA ZANZIBAR NA WATU WAKE.
Jamani wako wapi wawakilishi wenye masimamo kama wa Jussa. Tungalipata 15 kama hao kutoka CCM na 15 kutoka CUF basi tungalikuwa mbali sasa hivi.
What I hav learn, ni kuwa kama Wazanzibar tukiamuwa jambo huwa tunalifanya kwa standard, na hili limethibitika now. Atlist we can see the light, na watu wajifunze pia kuwa uwezekano wa Watu kuichukia Serikali na Viongozi wao upo kama watakuwa hawasimamii yale ambayo Wananchi wanayataka. Ila na uwezekano wa Watu kuipenda Serikali na Viongozi wao nao upo pia kama Serikali itasimamia maslahi ya Watu wake.
Sasa tunaona mabadiliko, hili sio tena lile BLW lililopoteza heshima na kudharauliwa na Wazanzibar kwa kutosimamia vyema wajibu wao na kufanya maamuzi ya kisiasa ambayo siku zote yamekuwa hayana tija kwa Wazanzibar.
Sasa inathibitika kuwa yeyote atakaesimamia maslahi ya Waznz ataheshimika na yeyote atakaehujumu maslahi ya Waznz tutapambana nae na kumdharau.
Kwa spirit hii tunawaambia Wawakilishi wetu kuwa “THEY WILL NEVER WALK ALONE” kwani Wazanzibar tuliowachaguwa tupo pamoja nao.
Wazalendo wezangu,
Mimi nahisi huu ni wakati munasab wa BLW ku-propose motion ya kuvunja Muungano badala ya kungojea huu upuuzi wa Katiba.This is sending the wrong impression/signal ya kuwa naqama hii itwayo Muungano bado tumeridhika nayo. Mimi natafishika hata nikisikia lile jina Tanzania likitajwa ndani ya baraza letu.
Hii si Tanzania bali ni kiTanzi cha Nyerere kwa Wazanzibari kunin’ginia. Huku kusema mambo haya tuakhirishe mpaka katiba mpya, ni sawasawa na kukubali kukaa chini ya mavutu ya Wadanganyika, wakaendelea kutufusia mafuso ya ugali na mlenda. Sijuwi mpaka lini.
Iko methali ya Kiarabu isemayo ” Albaab liijik minhu riih, sidd aleihi wsatariih” Yani ” Mlango ulo wazi ukakuletea upepo wa dharba ufungilie mbali ujistarehee”
Nakupa heko ndugu yetu mzazibari mzaleno mheshimiwa Jusa . Nime msikia mzee moja wa akieleza alivyowasikia wazee wa umri kuliko yeye na wacha mungu.kwamba Zanzibar baada miaka arubaini ya maafa 1964 itanza kufurukuta na kuanza harakati za kurejesha tena dola yake. Na wato ongoza harakati za ukombozi ni vijana wake . Yarabi iwe mhishimiwa Jusa awe katika vijana hao. Amba na amini wako wengi. Amin, Amin.
NEXT STOP BARAZA LA USALAMA KUDAI KITCHTEU KIREJESHE WE MUNGANO SI HA LALI.
WAZANZIBARI WANA KILA YA SELF DETERMINATION.
HI NI FURSA YA DHAHABU YA KUDAI HAKI YETU UN. WASILALAMIKE WA TANGANYIKA WEMEANZA WAO KENDA HUKO BILA YA KUTUSHAURI NA SISI HANA HAJA KUWA SHAURI LWA LILO NA MASLHI YA NCHI YETU. ZANZIBARIS AWAKE.