1138am:Matokeo ya kura ya maoni (official results)
Kwa mujibu wa habari kutoka Zanzibar hivi sasa matokeo ya kura ya maoni yameshotolewa ni kama ifuatavyo:
Asilimia 66.4% wamepiga kura ya NDIO
Asilimia 33.6% wamepiga kura ya HAPANA.
Kila la kheri Zanzibar Mpya!
Report:
0830am:
Unguja majimbo yaliosema HAPANA ni MAKUNDUCHI, CHWAKA, MUYUNI, KWAHANI, DOLE, CHAANI, UZINI, DONGE kwa ujumla majimbo 8 tuu yamekataa na majimbo 42 yote ya Unguja na Pemba nzima yamesema NDIO.Matokeo rasmi kuanza kutolewa na Tume leo saa nne asubuhi.
Zanzibar yasema NDIO, HONGERA WAZALENDO!
Mahojiano ya Ally Saleh na Ali Rashid
Mahojiano ya Ally Saleh na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Salum,Kassim
- Maalim Seif apiga kura ya Maoni na kusema: “Zanzibar Daima!” (Picha kutoka FB ya Ghassany)
- M.Seif akipiga kura ya NDIO (Picha kutoka FB ya Ghassany)
- Wananchi wakijipanga kusubiri kupiga kura (Picha kutoka FB ya Ghassany)
- Dk.Karume akitia kura ya NDIO (Picha na Ramadhan Othman Ikulu.)
- Dk.Karume – kura ya NDIO (Picha na Ramadhan Othman Ikulu.)
Picha zote kutoka FB ya Ghassany
Tangazo:
Kwa waliopo nyumbani tunaomba tupeane update ya kinachojiri nyumbani kufuatia Kura ya Maoni leo hii.Tafadhali acha habari hizo kama ni maoni, au kama huna internet access unaweza tuma ujumbe wa sms kwa namba 0031 684440925
Shukurani kwa ushirikiano wenu
P:S
**Tunaomba tetezi sisichapishwe kwenye machapaisho mapya kurahisisha watu kuona habari za Kura ya maoni kwenye chapisho hili ambalo litakuwa la mwanzo kwa wekeend nzima hadi mchakato huu ukimalizika.
Sikiliza repoti ya Ally Saleh,
Maoni ya wazalendo:
Je unakubali kuwepo kwa muundo mpya wa serikali mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2010? Total Voters: 1.617
Loading ...
Shukurani za dhati
Shukurani za dhati kwa wazalendo walioshiriki katika kutupasha habari.MZALENDO inatoa shukurani za dhati ziende kwa
- Ally Saleh,
- Salma Said,
- Shk Hassan,
- Mh.Jussa,
- Ghassany,
- Dr.Yussuf,
- Ramadhani Othman,
- Muddy
- Na wote ambao hatujawaorodhesha hapa, hio ni orodha ya haraka haraka wazalendo wote waliotupasha na kutupa update za tukio lilivyokwenda.
Inshallah kheri tusubiri kesho kupata matokeo rasmi ya ZEC.
MZALENDO.net
Changelog:
*Tumeongeza picha za M.Seif baada ya kupiga kura
**Tumeongeza mahojiano ya Salum,Kassim
**Mahojiano na Ali Rashid
**Ujumbe wa sms kutoka Zanzibar
**Tumeongeza picha za Dk.Karume
**Matokeo ya Tumekuja







Ikiwa sasa hivi ni saa 4:45 za usiku Wazanzibar wanatarajia kuandika Historia mpya ya kuleta mabadiliko katika visiwa hivyo pamoja na nchi kwa ujumla.
Wengi miongoni mwao hawakulala usiku kucha kufikiria jinsi gani wanaweza kuitumia siku hii adhimu katika maisha yao.
Ni wazi kuwa dua zao walizoziomba jaana katika viwanja Muumba wa mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo ndani yake amezikubali na matokeo mazuri yanakuja usoni.
Kwa mawazo yangu ikiwa wamemuomba Muumba wa mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo ndani yake basi bila ya shaka yoyote maombi yao yamekubalika.
Uchaguzi mwema kila la kheir Zanzibar.
Amiin
Mmbaleni.
Asalaam alaykum.
Kusema ukweli nna furaha sana kuona nchi yetu zanzibar inaelekea katika demokrasia ya kweli na pia kuitoa katika nakama na fitna za kihafidhina.
Ingawa naamini wengi wa wazanzibari halisi (wenye uchungu hasa na zanzibar) watapiga kura ya ndio lakini bado wasiwasi wangu upo na unabaki kwa hawa wanakisonge!!, je ni hasira za kutopitishwa kwa ‘mgombea wao’ ama wametumwa ili kuharibu mambo?.
Inshallah Allah hatosimama na yeyote mwenye nia mbaya na nchi yetu ya zanzibar, na ni yeye Allah pekee ndiye mwenye kujua lipi la kumfanya hasidi huyo anaetaka kutubakisha ama kuturejesha kule kule kwenye mifarakano na uhasama.
Allah ibariki Zanzibar, na wanyime nguvu na uwezo mahasidi wote wa Zanzibar….amiin.
wana mzalendo tupeni yanayojiri nyumbani kila hatua maana huku siye hatuna njia nyingine ya kuyapata. na kwa hakika leo wengi wetu htutaweknda makazini ili kuskiliza ya nyumbani. Allahumma Hdina…
Hamad
CPH
@Mseto,
Kiilivyo kamati nzima ya MZALENDO ni wanaishi nje ya Zanzibar.Lakini wazalendo watatupa data kamili kwenye chapisho hili inshallah.
Namba ya simu iliotolewa hapo juu ni namba ya simu inayotumika na MZALENDO, unaweza tuma sms kutupasha habari hakutakuwa na majibu ya sms.Kwa maana ya kuwa habari itakuwa imesomwa na kuchapishwa hapa MZALENDO, lakini uongozi hautokuwa bizzi kujibu sms zote.Tunaomba samahani kwa hilo la kutokujibu sms.
Email pia inaweza tumika kama kawaida admin@mzalendo.net, ashakh@mzalendo.net, stonetown@mzalendo.net na taymia@mzalendo.net.
Kila la kheri
Tunamshukuru Mungu, Kura ya maoni imeendelea kupigwa kwa amani, inaenda kwa spidi ya kuridhisha kabisa. Mpangilio wa watu umewekwa kwa alfabet. Watu wengi wamehudhuria. Matarajio ni kuwa ifikapo saa kumi jioni, watu watakuwa wamemalizika vituoni. Inshallah tuome kheri. Tuna matarajio makubwa ya kura ya NDIO kupata ushindi mkubwa kwa sababu hotuba ya Amani Karume ya juzi imechangia sana kuwabadilisha hata baadhi ya wale wanaopinga NDIO katika mwenendo mzima wa kura ya maoni.
Unajua bwana hata kama mtu anafanya ibada sana lkn hatakiwi kujipa 100% yakuingia peponi bali ajipe 50%. Amesema mtume (saw) kua “atakae sema kau yeye ni mtu wa peponi basi huyo ni mtu wa motoni” (jam’ussahiih). Nasema hivi si kwa sababu naiombea mabaya zanzibar la bali nakhofia mambo yakigeuka watu wasije kuchanganyikiwa. Na inshallah mungu tunakomba kura Ya ndio ipite na iwe ni ufunguo wa kundokana na matatizo zanzibar aamiin. Onyo pia kura ya ndio ikishinda watu washereheke kwa njia nzuri na wala wasichupe mipaka hakika mungu hawapendi wanaochupa mipaka. Nasema hivi kwani mungu anasema( إنالإنسان خلقهلوعا)
habari za punde tu ninazowaletea ni kuwa katika sehemu ambazo mimezitembelea kama vile mwanakwerekwe, kiembesamaki, jang’ombe, tomondo na mpendae nimeshuhudia watu wakipiga kura kwa hali ya utulivu mkubwa na haraka.
Ikiwa na uchaguzi Mkuu wa October 2010 utakuwa kama huu wa leo basi Zanzibar itakuwa imeendesha uchaguzi katika hali ya juu kushinda uchaguzi waliofanya Uengereza.
Ingawaje huu wa maoni umepata baraka za vyama vyote pamoja na taasisi zote ziliopo hapa Zanzibar, imani ya wananchi walio wengi bado ipo na matumaini ya NDIO kupiti kwa zaidi ya asilimia 70.
Hata hivyo baadhi ya watu wa sehemu za Jang’ombe bado wanatilia shakha na baadhi ya watu kufanya hujma za kushtukiza kwenye baadhi ya sehemu au mali za watu. Hivyo wanaiomba serikali kupitia vyombo vya ulinzi viimarishe ulinzi wao mara baada ya kura hii kupigwa na ulinzi uzidishe zaidi hadi wakati sheria hii itakapopitishwa hapo tarehe 9 Agosti 2010.
Tunawaalika katika karamu ya Mseto wetu.
Assalaam Alaykum, Waungwana.
Leo ni siku ya historia katika Visiwa vyetu. Wananchi wanajitokeza kwa maelfu kuamua hatima ya nchi yao. Mimi nimeshapiga KURA YA NDIO! Sijui nyinyi wenzangu!
Mohammed Khelef Ghassany
Maalim Seif amepiga kura yake muda mfupi ulopita na akasema “Zanzibar Daima!” alipoulizwa na waandishi wa habari ‘comments’ zake baada ya kupiga kura. Alisema ameridhika kwamba zoezi linakwenda vyema na kwamba ana matumaini kila Mzanzibari atapiga kura ya NDIO kwani hawataki kurudi kwenye migogoro iliyopita
Mohammed Khelef Ghassany Kuna tatizo kidogo katika kituo cha Mtopepo. Majina yamepanguka (yamepanguliwa?). Watu wanahangaika. Lakini hili halijaondosha ukweli kwamba hali inakwenda vizuri katika maeneo mengine. Kwenye picha hii watu wanaangalia majina yao ili wakapige kura
A/aleykum asilimia kubwa sana kesho ni siku kuu Kwa – Wazanzibari kwamujibu wa mambo yanavyo kwanda heko wazanzibari , sisi wengine hatukupata kushirikiana na nyinnyi kivitendo kwasababu tuko nje ya nchi lakini roho zetu ziko pamoja na nyinyi wenzetu .
pigeni kura kwa amani na salama .
M/MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA WATU WAKE .
Ismail Jussa:
So proud and happy. I have just cast my ‘YES’ vote at Vikokotoni polling station in Stone Town constituency. Voting is going very smoothly, with the level of efficiency never seen before. You find smile on the face of every Zanzibari. O! Allah we thank you for guiding us towards restoring the lost glory of our great nation, Zanzibar
Ismail Jussa Voting has closed at 4:00 pm and now only those people already in queus will finish voting before counting begins.
Kura ya maoni yafanyika Zanzibar
Kura ya maoni inafanyika Zanzibar hii leo, ambayo inalenga kubadili katiba na kuruhusu uundwaji wa serikali za kuwagawana madaraka.
Zaidi ya wapiga kura laki nne walioandikishwa rasmi wanatarajiwa kupiga kura zao.
Chama tawala CCM na chama kikubwa cha upinzani CUF, vyote vinaunga mkono kura hiyo, ambayo inanuiwa kumaliza ghasia zilizokumba uchaguzi wa siku za nyuma visiwani Zanzibar.
Zanzibar ina utawala wake wa ndani chini ya serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikiwa kura hiyo ya maoni itapitishwa, Zanzibar kwa mara ya kwanza itashuhudia mfumo mpya wa serikali ambapo kutakuwa na rais na makamu wake wawili.
Makamu wa kwanza wa rais atatoka chama ambacho kitashika nafasi ya pili katika uchaguzi na wa pili atatoka chama kilichoibuka mshindi.
Pia baraza la mawaziri chini ya mfumo huo mpya litakuwa ni la kugawana madaraka.
Mwandishi wa BBC aliyeko Zanzibar anasema matokeo ya kura hiyo ya maoni yanatarajiwa kutangazwa katika muda wa siku moja.
Baraza la wawakilishi
Baada ya wiki moja, baraza la wawakilishi nalo litakutana ili kufanya marekebisho ya katiba kulingana na matokeo ya kura hiyo ya maoni.
Zanzibar ambayo inaundwa na visiwa vya Unguja na Pemba ilitangaza uhuru wake tarehe 12 January, mwaka wa 1964 baada ya mapinduzi yaliyomwaga damu yaliyomaliza karne kadhaa za utawala wa kisultani wa Waarabu.
Baada ya miezi mitatu Zanzibar ilijiunga na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini ikabaki na utawala wa kijimbo, rais, katiba na bendera yake.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mapema miaka ya tisini, visiwa hivyo vimekuwa vikishuhudia mapambano makali kati ya chama tawala CCM na chama kikuu cha upinzani cha CUF, haswa wakati wa uchaguzi.
Chanzo:BBC
thanks mrfroasty, ingawa picha waliyoweka BBC Swahili haiendani na habari yenyewe. Sasa hivi hatuko katika ugomvi kwa hiyo hawakutakiwa kuweka picha ya kupigana marungu. Wangeweka pich kama hizi za mzalendo inegependeza zaidi
Both President Amani Karume and CUF’s Maalim Seif Sharif Hamad told reporters immediately after casting their ballots that they were satisfied with the way the referendum is conducted and the peaceful and orderly environment in which it takes place. They expressed their hope and optimism that the majority of Zanzibaris will vote ‘YES’ to pave the way for new political culture.
HideIsmail Jussa For those who would like to follow the results of the referendum online as they trickle in from the constituencies’ tallying centres, here is the ZEC site (Kwa wale watakaopendelea kufuatilia matokeo ya kura ya maoni kadiri yanavyoingia kutoka vituo vya majumlisho vya kila jimbo), ZEC imeweka mtandao maalum:
Zanzibar Referendum — 31 July 2010
referendum.zec.go.tz
Zanzibar Referendum (31 Jully 2010)
HIVI SHENI YEYE HAITAKI SERIKALI YA PAMOJA? MBONA HAKUNA HABARI KUWA KAPIGA KURA. TUNAOMBA MUTUPATIE KKITUO ALICHOPIGIA KURA SHENI, SASA HICHI KICHEKESHO KWELI YAANI KUMBE HATA KURA HANA HALAFU ANATAKA APIGIWE KURA!!
AMA HAYA MAAJABU YA HISTORIA.
Dr Shein hakuandikwa kuwa mpiga kura wa Zanzibar kwa maana hiyo hawezi kupiga kura hii kwa mujibu wa sheria. Utata wake wa kuchaguliwa nadhani ushaelezwa siku nyingi. Hata hivyo bora yeye ambae hapigi lakini anawaambia watu wapige NDIO kuliko wenye haki ya kupiga wanaohimiza watu wapige HAPANA. Tuangalie kura ya maoni kwanza. Simfagilii Dr Shein il namtetea kwa hili. Tukija katika kura ya October tutampa Maalim tunaempenda zaidi.
InshaAllah kesho tutaamka tukiwa na nuru katika nchi yetu. Tufurahi na tusherehekee lakini tusimkufuru Allah.
“ZEC imeweka mtandao maalum:
referendum.zec.go.tz”
Nimejaribu huo mtandao wa zec aliouweka Dr. Yusuf lakini bila mafanikio, nimejaribu kuweka
.GOV.tz pia sikufanikiwa. Kama kuna aliepata kuingia naomba atujulishe vya kufanya.
Natanguliza shukrani.
Kiungo sahihi ni:
http://referendum.zec.go.tz/
Note:
Hakikisha hutumii www
http://referendum.zec.go.tz/
copy hiyo link na paste. Usiweke www.
Kwa sasa hakuna taarifa lakini tunatarajia wataweka.
Ismail Jussa: BREAKING NEWS: I have just received results from Bububu School polling station and it is 70% YES.
@Jussa,
Bismillahi, matokeo hayo yazidi kwa vituo vingine inshallah
J
Matokeo ya Kituo cha Tumekuja
Matokeo yasio rasmi kutoka Kituo cha Tumekuja
Matokeo ya tumekuja school waliotakiwa kupiga 350, wamepiga 267, kura ndio 231, hapana 33, zilizoharibika 3.
Tumekuja number, wapiga kura 350. wamepiga kura 250 ndio 219, hapana 26, zilizoharibika 5.
Chumba 3, walitakiwa kupiga kura 350, waliopiga 345, ndio 209, hapana 30, ziliharibika 6.
Kituo number4, waliotakiwa kupiga 356, waliopiga kura 252, ndio 224, hapana 26, zilizoharibika.
Kura zote zilizotakiwa kupigwa 1406
Waliojitokeza 1014
NDIO 883
Hapana 115
Zilizoharibika 16.
@Stonetown
Shukran
Matokeo ya kura Kengeja Pemba:
NDIO 1438
HAPANA 223
ZILIZOHARIBIKA 35
Ujumbe wa sms kutoka kwa Mudy Salum
Eehh Mungu Ibariki nchi yetu Zanzibar!
Matokeo rasmi yanategemea kutangazwa leo kuanzia saa mbili usiku huu EAT.
Kila la kheri Wazalendo wote.
Habari tulizopokea ni njema sana.
Tunaitakia kila la kheri zanzibar mpya na iwe ya mafanikio kwa rehma za Allah,kila hasidi Mungu atamshinda iwe zanzibar ya wenye kupendana isiwe ya wenye kuchukiana
Mungu ibariki zanzibar na wabariki wazanzibari popote walipo wenye kuitakia kheri zanzibar
BREAKING NEWS kisonge kura 2200 na wapenda nchiyao 300000 walonuna 97800
Habari nilizo zipata majimbo matano NDIO imeshinda mpaka mda huu, nayo ni Mwanakwerekwe, bubu, dole, kikwajuni, kiembe samaki..inshallah kheri
Ujumbe umepolewa kwa sms
Shukurani za dhati kwa wazalendo walioshiriki katika kutupasha habari.MZALENDO inatoa shukurani za dhati kwa Mwandishi Ally Saleh, Salma Said, Shk Hassan, Mh.Jussa, Ghassany, Dr.Yussuf, Muddy na wazalendo wote waliotupasha na kutupa update za tukio lilivyokwenda.
Inshallah kheri tusubiri kesho kupata matokeo rasmi ya ZEC.
MZALENDO.net
Baada ya matokeo ya majimbo 28 ya Unguja ni kama hivi:
YES 92,094
NO 71,958
MAJIMBO YALIOSEMA NO: MAKUNDUCHI, CHWAKA, MUYUNI
KWAHANI, DOLE
CHAANI
inatarajiwa majimbo yote ya Pemba yatasema YES na tofauti ya kura
itazidi kupanuka.
mnukio wa 60-70 percent upo. Uwezekano wa 80 percent pia upo
Edited following correction below:
Kwa hesabu zangu za kudonoa hapo 71958*100/(92094+71958) ~56% yasema NDIO.Wazalendo Unguja pekee asilimia 56% imesema NDIO!
Naweza pata usingizi maridadi kabisa
Kila la kheri na usiku mwema
mrfroasty
Samahani sana nilitaka kukusahihisha kidogo jinsi ulivyofanya hiyo asilimia. Sahihi itakuwa kwa Majimbo ya 28 ya Unguja ni 92094/(71958+92094) =56.13707849 na waliosema hapana itakua = 43.86292151
Kwa mahisabu yangu ya haraka haraka nategemea Pemba watasema ndio kwa asilimia 82 na watakaosema hapana watakua asilimia sio zaidi ya asilimia 12.00. Kwa maana hiyo NDIO itakua imeshinda kwa asilimia 68.53653117% Inshaallah. Mimi niko Germany lakini nafuatilia kwa karibu kama nyinyi.
Kila la kheri na usiku mwema
Thanks,
Uko right hapo, naomba samahani hio asilimia nimeigonga kwenye calculator kwa haraka.Ni asilimia 56.14% imesema NDIO na asilimia 43.86% imesema HAPANA kama ulivyoeleza.
mrfroasty,
Wamtambwe umenitangulia hata na mimi nilikuwa katika hesabu hapa nikaja na hiyo ya 56.13%.
Nimejaribu kucheza na hesabu kidogo, kwa mujibu wa matokeo tuliyonayo ya majimbo 28 ina maana kuna majimbo manne ya Unguja bado. Nimefanya makisio kwamba takriban wapiga kura 50.000 hawakupiga kura na nimewapa HAPANA watu 800 kila jimbo la Pemba na watu 2.000 kila jimbo la Unguja kati ya yaliyobaki. Hesabu ya Unguja imezingatia kuwa majimbo pinzani ya Wilaya ya Kusini tayari yameshatoa matokeo yao ya kupinga kwa ushindi mwembamba na Dole la Wilaya ya Kati. Baada ya kuzingatia haya nimepata hesabu ya wastani wa 69.73%. Kwa hali inavyokwenda natarajia ushindi wa asilimia 68 kama aliyotoa Wamtambwe hadi 74% kulingana na kiasi gani watu wameshiriki katika zoezi hili na kura zilizoharibika ni ngapi. Mimi naomba Mungu tupate hii ya 74% au zaidi.
Zanzibar inaelekea kuwa njema, lakini hatukaribishi kila mtu. ‘ile atakae aje’ basi tena
Maajabu ya matokeo haya:
Haroun anataka serikali ya umoja lakini jimbo lake halitaki
Nahonda yeye umoja hautaki lakini watu wa jimbo lake wanautaka.
0830am:Latest:
Unguja majimbo yaliosema HAPANA ni MAKUNDUCHI, CHWAKA, MUYUNI, KWAHANI, DOLE, CHAANI, UZI, DONGE kwa ujumla majimbo 8 tuu yamekataa na majimbo 42 yote ya Unguja na Pemba nzima yamesema NDIO.Matokeo rasmi kutolewa na kuanza kutolewa leo saa nne asubuhi
Zanzibar yasema NDIO, HONGERA WAZALENDO!
asalam alaykum!
wanaukumbi wazanzibari wazalendo kumekuchaaaaaaaaa na makucha yake nikiandika khabari hii nikiwa nimejawa na furaha kwa mujibu wa vyanzo vyangu ni kwamba jimbo la donge na uzini pia yamekataa na kupelekekea kutimia majimbo manane kwa unguja kusema hapana lakini napata tena faraja kwa ndugu zetu wa pemba kusema ndio kwa majimbo yote na kutudhihirishia ushindi kwa ndio. katika majimbo yote hamsini manane yamesema hapana lakini arbaini na mbili yamesema ndio.alhamdulihhhhhhhhh ALLAH NA ASHUKURIWE KWA KUSALI SALATIL SHUKRA KWA KILA MZANZIBAR MUISLAM.SISI KWETU TUNA MSEMO UNASEMA WENGI WAPEEEEEEEEEE.
Inshallah matokeo yawe hivyo tusemavyo baina ya 70% mpaka 80%. Kwa hali hii 75% ni ya uhakika, kwa hiyo kwa kiasi fulani tumefanikiwa. Tumefanikiwa kwa maana ya kuwa tumekubali makosa yetu. Leo hapafanyiki kitu, ni sherehe mtindo mmoja na huwezi kuwazuwia kwa vyovyote vile. Alhamdullah mambo yamekuja wakati mzuri mwezi wa shaaban na baada ya siku kumi ni Ramadhani, kwa hiyo ni miezi ya ibdada na yenye barka kubwa kubwa, sina maana mengine sio ya ibada, laa hasha…
Ninacho jiuliza, tumejipanga vipi kuanzia jumatutu 2, august 2010? Hatuna muda wa kuchezea, tumepoteza miaka takriban 57 tokea 1963 mpaka 2010. Kwa hiyo mwaka huu tunavunja jungu kwa kheri kabisa, tunakutana tena kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukubalia dua zetu tulizo omba Maisara na misikitini, ikisha tunaiingia Ramdahani, tukimaliza tunakwenda tena kwenye uchaguzi kwa mbwembwe kabisa.
Mara hii tusikaribishe watu kuja kuleta ufisadi ndani ya Zanzibar. Nadhani mumemsikiliza Bwana Mohd Said kwenye Youtube akifafanuwa juu ya kitabu cha Zanzibar…
Zanzibar Daima
haya mambo ya kutangaza matokeo usiku saa nne sijuwi si mazuri. Kama kura zishajulikana ni kupewa mambo moto moto, wasije wakaja vidudu watu wakaja kutuchafulia mambo na uzoefu unatuonesha hivyo….
@Kassim,
Data ya Saa nne usiku ilikuwa ni kosa langu la uchapishaji, nilikuwa sijaamka vizuri.Matokeo ni kuanzia saa nne asubuhi.
P:S
Chapisho lisharekebishwa
Wazalendo nimepata hii habari, hebu isomeni.
Initial results of a referendum in Tanzania’s Indian Ocean archipelago of Zanzibar on Saturday showed that 75.4 percent of voters gave yes vote to the formation of government of national unity in Zanzibar after the general elections in October.
Chairman of Zanzibar Electoral Commission Khatib Mwinyi Chande announced the result of five out of 50 constituencies in Unguja and Pemba, the sister islands of Zanzibar, after the completion of casting ballots in the referendum, which took place on Saturday.
Chande said in the five constituencies, 4,978 voters, equal to 75.4 percent, gave yes vote, and 1,622 people, equal to 24.6 percent, said no. All the five constituencies so far announced are in Unguja.
Chande said more results are expected to be announced on Sunday starting at 10 a.m. local time (0700 GMT), which would be followed by the announcement of the final results.
Thousands of people in Zanzibar voted in the referendum, marking a high turnout. Voters included President of Zanzibar Amani Abeid Karume, Zanzibar Chief Minister Shamsi Vuai Nahodha, the opposition party the Civic United Front (CUF)’s Secretary General Seif Sharif Hamad and the running mate of president of Tanzania, Mohd Gharib Bilal, who is the current Tanzanian vice president.
Karume said the vote went on in an atmosphere of peace and harmony, indicating the hope of prevailing peace and tranquility in the coming general elections.
Under the proposed structure of a government of national unity likely to be formed after the next elections, if a ruling Revolutionary Party of Tanzania Chama Cha Mapinduzi (CCM) candidate wins the presidency, CUF’s Hamad would become first vice president.
Source: Xinhua
HAYA JAMANI ANZENI KUKAA WATATU WATATU, MSETO UMEIVA, UNANUKIAA HARUFU NZURI ZA VIKAANGO NA SPICES ZA ZANZIBAR. TUNAMSUBIRI MPISHI BW. MWINCHANDE, MPAKUAJI NI MIMI MWENYEWE. JAMANI TUNAOMB MUJIPANGE KWA HISANI YENU.
MAASHALLA! MSETO WA KIPEE, UMEIVAA NA UNANUKIA, AA! WAPISHI HASWA WALIKUWA NI WENYEWE WAZANZIBAR NA WALAJI NI WENYEWE WAZANZIBAR. ALLAH AWABAARIK NA AWALIPE KHERI NA AWALISHE RIZKI HII YA MSETO IWATIE NGUVU, IJENGEKE MIILI YENU KWA MSETO HUU IWE NA NGUVU YA KUMSHINDA ADUI YEOTE YULE ATAKAEKUJA KUINGIZA HASAD NDANI YA NYOYO ZENU.
UWE NI MSETO WENYE FANAKA NA UTAKAOJENGA DAMU ITAKAYOSAMBAA NDANI YA MIILI YENU NA KUWAJAZA AKILI YA KUENDELEZA VISIWA VYENU. UWE NI MSETO MUTAKAOULA NA KUWAKUMBUKA NDUGU, JAMAA, MAJIRANI, YATIMA,MASIKINI NA FUKARA.
NA MWISHO NIWAKUMBUSHE TU MTUME MUHAMMAD AMANI IWE JUU YAKE ANASEMA UTAKAPOKULA BASI LIGAWE TUMBO LAKO KATIKA SEHEMU TATU. NAMI NAWAAMBIYA MUTAKAPO ANZA KUULA MSETO MUJIANDAE NA KUYAGAWA MATUMBO YENU SEHEMU TATU. YA KWANZA NI KWA AJILI YA UHUO MSETO, YA 2 NI KWA AJILI YA MAJI NA YA 3 NI KWA AJILI YA HEWA. PIA TUSIJE TUKAULA MPAKA TUKAVIMBIWA NA PIA TUSIJE TUKAFANYA ISRAF.
ALLAHUMMA AHDINAA BIFADHLIKA FIYMAN HADAYT.
@ kwaomtu
kwa hakika wazanzibari washajitayarisha na kugawa matumbo yao sehemu tatu kama ulivyoagiza na walaji wote wa mseto huu watagawa matumbo yao katika sedhemu tatu zifuatazo
1- zanzibar
2-tanganyika na
3- muungano
natumai walaji hawatafanya israf ishallah
ZEC iko kwenye mchakato wa kuhesabu kura jimbo moja baada ya moja habari ziko kwenye radio.Tuvute subra baada ya nusu inshallah matokeo yatakuwa tayari.
Kila la kheri
BREAKING NEWS KURA NDIO IMESHINDA NA MATANGAZO YASHAFUNGWA REDIONI LIVE KUTOKA BWAWANI SALAMA HALL. MSETO UMEIVAAAAA
kura ya maoni
hongereni wanzanzibar kwa ndioooooooooooo hata sisi huku tunatia kura zetu hapa
Assalaam allaykum wanaukumbi kwanza kabisa Alhamdulillah kwa Allah kututakabalia dua zetu na InshaAllah huu ndo utakua mwanzo wa Zanzibar njema na mpya kuna mengi ya kujadiliwa huko usoni lakini kwa sasa tufurahie ushindi ulopatikana zanzibar oyeeeee!wazanzibari oyeeee! hapa simu zinamiminika tu kutoka home sijui niipokee ya nani niiwache ya nani inshaAllah kheri kubwa itapatikana Amin.
NDIO NDIO NDIO
Tumeshinda natowa shukurani kwa Wazanzibari wenzangu wote walio shiriki katika zoezi la kupiga kura na wale ambao hawaja jitokeza kupiga kura kwa udhuru.
Pongezi kwenu mlio chaguwa ndio na hapana kura tayari imekwisha kamilika msindi kasha julikana na tuwacheni uhasama kwa sasa Wazanzibar tuwe wamoja kwa kuya tokomeza matatizo yaliyo tukumba kwenye miaka ya nyuma wakati serikali ya umoja wa kitaifa ikifanya kazi.
Hongereni zec kwa kutufanyia taratibu nzuri za uchaguzi kwa hali ya juu.
PEMBA+UNGUJA=ZANZIBAR ITAKAYO FUTA SHIDA ZA MIAKA ILOPITA.
Mungu tujalie Zanzibar ilio njema na amani amin
BREAKING NEWS
KURA YA NDIO IMESHINDA KWA ASILIMIA ZAIDI YA 66% HONGERA ZANZIBAR MPYA
AS duwa imefanya kazi.sasa ufisadi wote umekwisha.maana ukipiga simu nyumbani kila siku utapokeya habari mbaya.lakini leo aaa mtu anaanza na kucheka. daa amakweli sasa mambo barrdi jinaamizi linaanza kuwondoka kidogokidogo.
watu wana furaha utafikiri skuku
salama kwa wote waliotiya hapana. sasa mambo yameshakwisha hatuna ugomvi na nyinyi tukaeni pamoja tufunguwe ukurasa mmpya.sasa jahazi limevuka kwenye mawimbi makubwa linaelekeya kwenye maji shwari.
Alhamdulillah, Mwenyezi Mungu katuwepeshia hili na atuwepeshie na mengine waja wake.
Zanzibar oyee. Hongera Wazanzibari, Hongera ZEC kwa kazi nzuri lakin msije kugeuka mlevi kusifiwa… Hongera Dr Karume, Hongera Maalim Seif.
Shukran za dhati kwa uongozi wa mzalendo.net na wapasha habari wote kwa kwenda sambamba na shughlui yote. Nadhani ZEC wanaweza kutuamini kama tunaweza kuwasaidia kazi ya kutoa live results hapo october
Nakutakieni Eid njema – kull aamun waantum bikheir. Hint: Idd hii watu wasile pilau wala biriani, ni mseto tu!!!!!!! Wakisonge watakula dona manake hawautaki, hahahahaaaaaaaaaaaa.
Alhamdulillahi Rabbi l ‘Aalamiin.
Mungu ibariki Zanzibar na watu wake.
Hongeraaaa Wazalendo.
Kwavile leoni EID, watu wafurahie bila ya kuwakera wengine. Tijipongeze kwa yale tuliyopata. Najuwa wengi wanayo yanayowakereketa, kwa leonaomba mumezee kwa huo mseto.
Tukumbuke tu kuwa hii ni hatua ya saba kufikia 10. Tualianza na hatua mpaka tumefikia hapa. Pamoja na furaha zetu tujitayarishe kuzimaliza hatua tatu zilizobakia.
Naam, siku hiyo ikafika,
Leo hakika ni siku ya kukumbukwa; natoa ombi kwa Mzalendo kuiweka katika tarehe siku hii na kila itapofika kuisheherekea kwa ukumbusho; Pia ombi hili ni kwa serikali yetu adhimu. Ni siku ambayo Zanzibar ilikuwa ikiiota, leo imetimia.
Bado safari yetu ni ndefu, na sisi tulio macho ni mwendo kwenda mbele tu; hakuna kurudi nyuma hadi taifa la Zanzibar lirudishe hadhi yake na kila kilicho chake.
Natoa pongezi za dhati kwa mashujaa wa Zanzibar Dr Amani Karume na Maalim Seif; na kwa wananchi wote waliopiga ndio, nawaambia hawatojutia uamuzi wao; na walio piga hapana ni haki yao pia nao wanakaribishwa kwa moyo safi katika Zanzibar mpya.
mbioni kutayarisha makala ya kusheherekea siku hii adhimu.
Mungu izidishie baraka Zanzibar na Wazanzibari. Amin.
tunashukuru kwa news mulotuppatia,tunaomba kila la kheri zanzibar,amin,tujiandae na kura ya maoni ya muungano sasa,mungu ibariki zanzibar mpya
hara tupu leo na mukitaka hara zaidi kwa wale waliokuwa hawajasikiya kwa mashikiyo yao basi nawaomba wende kwenye http://www.bbcswahili.com halafu wabinye ile ya juu kilopo cha sauti. mupate hara na nyinyi . hiii ni mara ya kumu na 19 narejeya kusikiliza yani inahara kweli kweli kwa shangwe iletagazwa raha kweli .
ZANZIBAR DAIMA. Hongera dr. Karume, hongera maalim seif(hafidhwahullah) hungera dr. Kikwete, hongereni wazanzibari kwa kutia kura ya ndio, hongereni wazanzibari nyote kwa ujumla. Mungu ijaalie kura hii ya maoni iwe msingi wa utatuzi wa matatizo yote ya zanzibar. Aamiin. Tumeona matokeo kwa upande wa unguja tu 56% wastani wameweka ndio jee kwa upande wa pemba pekee ni asilimia ngapi?
A.A Majimbo ambako HAPANA zimeipita NDIO NI Amani, Uzini, Chaani, Chwaka, Kwahani, Dole, Makunduchi na Muyuni.Donge ndio zimezidi.
Jabir Idrissa, Mhrr (Mwanahalisi)
Ahsanteni sanandugu wachangiaji.
mimi sina budi ila kumshukuru (ASW) kutpatia nuru hii ya kukubali Serikali ya Umoja Zanzibar hii ni alama njema Amin. Lakini nawakumbusha ndugu wazalendo wa ndani na je ya Zanzibar kwamba, tujifunge vibwe-bwe na tuendelee na safari yetu. Hii niktokana nakwamba “BADO HATUJAFIKA TUNAKOTAKA KWENDA”
1.tuanze campain zetu mpya za kura ya October, ambayo itaweza kutubadilishia itatubadilishia uongozi uliopo sasahivi. Hili DuDu linalotwa “CCM” mimi binafsi sitaki kulisikia tena katika Visiwa vyetu. Kwani limekuwepo kwa miaka 33 sasana halikutuletea muafaka wala masikilizano. Ila hasama na ufataghani miongoni mwetu.
Campaign tulizozifanya kwa kupitia Harambee za Mzalendo mpaka tukapata matokeo ya kura ya MAONI YA NDIO. Ndio hizo hizo tutakazo zitumia tena katika kipindi hichi kifupi ili tupate ushindi wa uchaguzi wa OCTOBER.
2.Kama Tunavojua michango yetu haikupotea ila imenufaisha kwakupeleka ujumbe. NGAO NDIO Hiyo hiyo na wembe ndio ule ule. Tutumie TV, Redio na magezti(Mediar Reports) kueneza habari za uchaguzi mkuu. Uchaguzi huu ndio utakaotupa hatima yetu na Identity yetu ambayo imepotea kwa muda mrefu sana. Mpaka ukaitwa ADOPTION CHILD NA WATANGANYIKA. …..AS IF WE ARE ONE OF THE SMALL REGION FROM NO WHERE; AND WE HAVE BEEN ADOPTED BY THE TANGANYIKA. ITS HORRIBLE.
3.Waznzibari kumbukeni ZEC imetoa matokeo haya kwasababu imefanya kazi na Kamati ya Watu sita ambayo walichaguliwa watu 6 kushughulikia suala ilila Kura ya Maoni tu. Na ndio maana matokeo hayakua na mizengwe yoyote ile. Sasa uchagzi mkuu wa Uraisi na Wabunge ZEC hiyo hiyo ndio inafanya kazi. Na iko peke yake, haina tena kamati yoyote ile yakuisaidia/ kuiongoza/kuiyangalia.
Wazalendo tumepatiwa Website ya ZEC, tuanzeni kuwatia presureZEC watuletee uchaguzi wa Haki na Amani. SISI Tlioko nje ndio tunaweza tukairekebisha ZEC.
alhamdulilah kwa kutukubaliya duwa zetu za ndio ningeomba tukafanya sala ya kumshukuru mungu kwa hili
naomba kuliza wazalendo inabidi hii serekali ya MAPINDUZI haitokuwepo tena ?jee kutakuwa na jina jipya?
Sasa wazalendo tumetayarisha kiburudisho gani kusherehekea ushindi huu.
Rusharoho, beni, kidumbak, msewe, taarab, au…..
Nyoyo nazo zinataka kutulizwa, angalau wale wa Copenhagen, Oslo, Amsterdam, London, Paris, Toronto, NewYork, wajione kama vile wako ngome kongwe. Wa Dubai na Mascut wao hawako mbali ni ziko nyingi tu wanaweza kujipumbaza.
kwanza ramadhani
ndugu yanfu ashakh usiwe na pupa kwanza tunaikaribisha ramadhani halafu eid halafu tutasheherea serikali sio kura ya maoni.
kumbuka znz tulilima ramadhani na inshaallah tuyavuna ramadhani inshaallah
A/A ,Namshukuru Allah kwa kutujaalia afya nzuri natusherehekee kwa aman ushindi
tulioupata iwe ndio chanzo cha taifa la ZANZIBAR.
Mimi binafsi nina mashaka na matokeo ya tume katika kura ya maoni.
Matokeo waliyoyatoa ni 66.4=NDIO na 33.6=HAPANA,sasa asilimia
ya kura zilizoharibika ziko wapi?
@ mrfroasty kuhusu asilimia, hapana tatizo kwani wametoa idadi ya watu waliojiandikisha, waliopiga kura,kura zilizoharibika,na kura halali. Kwa kutumia kura halali yaani kura zilizopigwa zilizobaki baada ya kutoa zile kura zilizoharibika ndio wamechukua percentage ya zilizosema ndio na percentage ya zilizosema hapana kwa kutumia kura halali. Mimi mashaka yangu ni kua watu wengi hasa unguja hawakupiga kura au hawa ndio mapandikizi wa kutoka bara wanasubiri uchaguzi wa october?
Kwa jumla majimbo mengi ya unguja watu waliopiga kura ni kati ya asilimia 60-65% ya wale waliojiandikisha tafauti na pemba asilimia kati ya 70-80% ya waliojiandikisha wamepiga kura. Kwa znz yote ni 70% wastan ya waliojiandikisha wamepiga kura. Kwa unguja wastan wa 56% wamesema ndio na kwa pemba wastan wa 88% wamesema ndio. Kilicho nifurahisha zaid ni kua ktk jimbo alikozaliwa maalim seif, 95.1% wamesema ndio hili ndio jimbo ambalo ndio imeshinda kwa wingi zaidi kuliko majimbo yote ya znz.
shekh Ahmed A.Rejected (spoiled)votes huwa ziondolewa katika hisabu na kubakishwa kura sahihi tu,katika kupata pacentage za mshindi na aloshindwa,Hujulikana tu ni asilimia gani katika kura zilizopigwa.Ili kuwaka hesabu sawa ya watu walojitokeza.hubakihwa hesabu ya kura sahihi tu
@Mpapani
Ulivyomfahamisha ndugu Ahmed ni sawa, lakini na mimi nahisi kama record zilizowekwa kwenye ule mtandaona wa ZEC ziko sawa, basi asilimia ya NDIO – 66% na HAPANA- 34%. Sasa sijuwi 66.4 imepatikana vipi. Mimi hesabu zangu za vidole ni kama ifuatavyo:
VALID VOTES – 266,064
YES VOTES – 175,476 / 266,064 = 65.952 (SAY 66%)
NO VOTES – 90,588 / 266,064 = 34.047 (SAY 34%)
TOTAL 100%
Any way, la muhimu ni kuwa tumeshinda kwa zaidi ya 65% ambayo binafsi nahisi ni asilimia kubwa.
Alhamdulillah, hatuna budi kumshukuru Allah kwa kutukubalia duwa zetu.
mwanzo mgumu
mimi siwalaumu sana walotia hapana hawa watakuwa ndugu zetu wa ccm ambao wanahitaji kuondolewa mawazo mapotofu waliojazwa tangu enzi za siasa chafu.
wanahitaji kuelimishwa zaid na zaid