M.Seif akipiga kura ya NDIO
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 31/07/2010 // // 1 Comment
Maalim Seif amepiga kura yake muda mfupi ulopita na akasema “Zanzibar Daima!” alipoulizwa na waandishi wa habari ‘comments’ zake baada ya kupiga kura. Alisema ameridhika kwamba zoezi linakwenda vyema na kwamba ana matumaini kila Mzanzibari atapiga kura ya NDIO kwani hawataki kurudi kwenye migogoro iliyopita





One Comment on "M.Seif akipiga kura ya NDIO"
Naafikiana na Maalim Seif kwa kusema,ktk nyakati tulizonazo Wazanzibari hawataki kurudi kwenye migogoro iliyopita ambayo takriban ni nusu karne iliendelea kuitafuna Zanzibar na siasa zake na zaidi ikaleta mifarakano.Tunaka ujenzi wa Zanzibar mpya,yenye matumaini mapya na itakayofungua ukurasa mpya kwa wananchi wake wote kwa kukaa pamoja na kufanyakazi pamoja bila kujali tofauti zao za dini,rangi,asili au kabila.Zanzibar daima!!!