Habari

Serikali ya “Hardliners”

Ilivyoanza ndio ilivyomaliza. Serikali ya Ali Mohammes Shein inaonyesha wazi ni serikali inayojiunda ya watu wenye misimamo mikali, hawa tunawaita hardliners. Na imechukua watu kutoka utawala wa Dr.Salmin Amour. Sasa itakuwa ni misimamo mikali tu, vunja nyumba za watu, fukuza kazi, piga, n.k — hata CCM wenyewe wameshaliona hilo.

Kumteuwa mtu kama Ali Karume, Amina Salum Ali, au Castico – hawa wote ni wote wenye misimamo mikali ya kuimaliza Zanzibar. Hivi leo kama Ali Karume atakuwa Waziri, hiyo wizara itakuaje? au wafanyakazi wa hiyo wizara itakuaje? Ukiachilia aliyofanya huko nyuma ambayo hayajafutika, hata hizi tabia zake binafsi za siku hizi tu zinatosha kusema kuwa ‘hafai’ . Hivi kuna kiongozi anakwenda pub/bar mpaka asubuhi, tena takriban kila siku na mengine mengi.

Yaani ilikuwa iwe baada ya makosa yoooote hayo, wananchi angalau ilikuwa wapate kiburudisho cha kupewa serikali nzuri, yenye utawala mzuri – lakini hakuna incentive wazee, bandika bandua, likitoka hili linakuja lile.

Unaweza kuwa dikteta, lakini ukawa mzuri kwa wananchi na utoaji huduma ukawa wa kupigiwa mfano, lakini hayo yooote kwa hapa Zanzibar hayapo na hatutegemei kuwepo.Ni msuguano tu, kwa miaka mengine mitano.

Share: