Habari

Serikali ya SMZ na Katiba MPYA

Asalama Alaykum (naomba unitolee mada hii mzalendo- thank you)

Leo Katibu wa BLW, Bw.Yahya Khamis Hamad amekaririwa na vyombo vya habari hapa Zanzibar akisema kuwa ‘sheria mpya NO.8 ya mwaka 2012 inayounda sheria ya kuandika katiba mpya ya Tanzania itapelekwa BLW kwa kupata idhini ya baraza’.

Lakini alipoulizwa kwa nini imechelewa sana. Bw.Yahya alijibu kuwa “tokea imepitishwa sheria hiyo na kutiwa saini na President Kikwete hakukuwa na kikao chochote cha BLW kilichofanyika”.

Huu ni UWONGO usiokuw ana kichwa wala miguu. Kwa kumbukumbu zangu, sheria hii ilitiwa saini na kuwa sheria kamili na JK Feb 2012; na kikao cha mwisho cha BLW kilimalizika mwezi wa April 2012.

Kwa nini tunadanganyana kiasi hichi; kwa nini tunafanywa wajinga, wapumbavu, basi hata hizo tarehe za vikao hatuvijui?

Nakumbuka hili niliwahi kulisema kabla kuwa BLW waipitishe sheria/msawada huu kabla ya kutiwa saini na Rais JK na kuwa sheria [please refer mada zangu z ahuko nyuma].
Na Abdi Salum

Leo Yahya Khamis Hamad anageuka na anakuwa mtu mwengine kabisa kuliko yule tunayemjua miezi iliyopita. Sasa anahalalisha UOVU wa watawala na kuufanya kukubalika kama sheria.

BLW ndio wameshaambiwa waipitishe sheria hii, na hawawezi kuipinga so long w ao ni CCM na CUF — maridhiano.

Hii n dio Zanzibar. Yahya alipokuwa hajapewa fupa, alikuwa mtu wa kusimamia haki na wajibu, sasa amekuwa mtu wa kupinda kama alivyo Abubakar Khamis Bakari na Othman Masosud na wenzao kama hawa. Yaani pale wanapokuwa nje ya system wanakuwa moto, wakiingizwa ndani siku moja tu – wanakuwa baridi.

Hii ndio Zanzibar, tunajitia jiti wenyewe.

Kama kweli mchakato wa kuandika katiba mpya umeanza hivi, umejaa ufisadi, ujanja, udanganyifu, hadaa, kweli hatma yake itakuwa nzuri. Wanafilosofia wanasema kuwa ‘wrong approach brings wrong results’.

Kuanzia mswada mpaka kufikia sheria hadi kujadiliwa kwake – tayari zoezi zima limejaa mizwengwe – kweli tutapata katiba tunayoitaka, hasa Zanzibar?

Sasa uoza kama huu watausema UAMSHO, wataambiwa kuwa wao ni kama boko haram! au wanaofanana na hao. Juzi UAMSHO wameitwa majambazi – je wale walioiba pesa za EPA bank of tanzania ni nani, waliokuja kuuwa Zanzibar, pemba 2001 ni nani? waliobaka watoto wa watu hapa Zanzibar, na Piki Pemba 2005 wlaikuwa nani (mawalii? Masheikh?)

Tagsmakala
Share: