Siasa sio mradi wa biashara- Maalim Seif
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 20/02/2012 // Habari // 7 Comments
Salma Said,
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema siasa sio uwanja wa biashara bali ni fursa ya kuwatumikia wananchi, hasa katika majimbo ya uchaguzi. Alisema kwa kuzingatia kuwa kuingia katika siasa ni fursa ya kuwatumikia wananchi, viongozi wa kuchaguliwa lazima wajenge utaratibu wa kushikikiana kwa karibu katika kufanyakazi za kuwakomboa wananchi kutoka katika umasikini.
Maalim Seif alikuwa anazungumza katika sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Kuendeleza Ujasiriamali na Ajira (MKUAJI) unaodhaminiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni, Nassor Ahmed Mazrui nje kidogo kutoka mjini hapa jana.
Alisema Madiwani, Wawakilishi na Wabunge wakiendelea kufanyakazi kwa mtindo wa “kila mtu na wake” na kugeuza siasa kuwa mradi wa biashara wa kuwaneemesha, juhudi ya kuwaletea maendeleo wananchi itakwama. “Wanasiasa wote, Zanzibar tumeomba kazi kuwatumikia watu, sio matumbo yetu,” alisisitiza Maalim Seif.
Maalim Seif alisisitiza kuwa anasikitika sana anapoona Mwakilishi au Mbunge visiwani Zanzibar na Tanzania bara kwa jumla anatumia muda mwingi kwa shughuli za biashara zake na kuwasahau watu.
Alisema Madiwani, Wawakilishi na Wabunge wote wameomba fursa hiyo kwa ahadi nyingi, lakini baadhi yao wakishaingia ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Bunge wanawatelekeza watu katika majimbo yao.
Alimpongeza Mwakilishi Mazrui kwautekelezaji wa ahadi kwa kuchimba visima 11 chini ya mpango aliojiwekea wa kuwaondolea wakazi wa Jimbno la Mtoni tatizo la ukosefu wa huduma ya maji.
Pamoja na kupunguza tatizo la huduma hiyo, Kwa kushirikiana na Kituo cha Mafunzo ya Ujasiriamali Tanzania, kanda ya Zanzibar Mwakilishi huyo pia amejenga kituo cha biashara chini ya MKUAJI na kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi 36 vya ujasiriamali huko Mtoni.
Kituo hicho ambacho bado kinaendelea kujengwa, tayari ujenzi umegharimu shilingi milioni 32, na kwa mujibu Mazrui pamoja na mambo mengine kituo hicho kitatoa mafunzo juu ya uendeshaji miradi ya maendeleo, hasa inayolenga kuondoa tatizo la ajira kwa vijana




7 Comments on "Siasa sio mradi wa biashara- Maalim Seif"
Nimefurahi kumuona yule dada kushoto ya Mw. Seif. Hili ndilo katika vazi la kitamaduni la Zanzibar.
A/alaikum Wananchi wote wa JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.
Bila shaka mtindo huu aliouwanzisha Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Mh. Nassor Ahmed Al-Mazrui kwa kuwapa huduma nzuri watu wa Jimbo lake hilo; ni kitu cha kutia moyo sana, kwani hivi ndivo inavotakikana kwa kila Mwakilishi na Mbunge kutimiza ile ahdi aliyoitowa wakati wa kampeni za uchaguzi na kwaajili ya kuomba voti katika Jimbo lake husika.
Mimi nahisi ikiwa Wawakilishi na Wabunge wetu wote hapa Zanzibar, (Unguja na Pemba) wataanza kufunguwa miradi na kuwapatia huduma nzuri Wananchi kwa lengo la kustawisha na kwa kutumia anuwani ya **KILA MWAKILISHI/MBUNGE KUBORESHA JIMBO LAKE** Kwa ushindani halisi wa vitendo vyema, yaani kwa kila ‘Mwakilishi/Mbunge’ kuwa na hamu ya kutaka kumpikuwa mwenzake kwa ajili ya kuonyesha imani na mapenzi kwa watu wa hilo Jimbo lake. Hii itakuwa/itaonyesha angalau amewadumulia kidogo katika zile ahdi alizoziahidi wakati ule wa kinyanganyiro wa kutafuta ushindi. Si-hivo tuu, bali atakuwa ameshamwaga ZEGE la msingi madhbuti usiolegalega pale Jimboni pake, na itakuwa ni mfano wa MPUNGA ambao umeshaiva shambani, yeye ateremke na kisu na junia lake kwa ajili yakwenda kuvuna tuu.
Katika Nchi za Ghuba ya Kiarabu {{ARBIAN GULF}} Wizara, Makampuni na Mabenki hushindana kwa kina utowaji wa huduma nzuri kwa kila mwaka, mwenye kuibuka kuwa mshindi wa huduma nzuri hizo? hupewa ZAWADI nzito/nzuri na ya kufurahisha ni Serikali, ambayo zawadi hiyo husababisha kutia hamu na ashki kwa wale waAjriwa/wachapa kazi ili kuongeza juhudi zao!! kwa lengo la ushindi wa mwaka ujao, huku nchi ikawa inazidi kupata maendeleo mazuri na uchumi kuzidi kukuwa/kunawiri, Ajira kuongezeka na wanyonge kunufaika.
Mcheza kwao hutunzwa, kwa hivo sinabudi kumpongeza Mh.Nassor Ahmed Al-mazrui kwa juhudi na huduma nzuri aliyowafanyia Wana-waJimbo lake la Mtoni, kwa ajili ya kurahisisha matatizo na angalau kuipunguza ile shida iliyowakabili watu husika katika Jimbo hilo. Nasema HONGERA MH. NASSOR AHMED AL-MAZRUI. **KEEP IT UP**
Mwisho namuomba M/mungu ajaalie hii khatwa aliyoitekeleza Mh.Mazrui iwe nichanzo kizuri na funzo kwa WAWAKILISHI/WABUNGE wengine kuweza kufuata nyayo hizi adhim ambazo bila shaka zitaleta faida kubwa na mustaqbal mwema kwa Wananchi wa “JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR”
WABILLAHI ATTAWFIQ
MCHONGOMA
Mimi nimefurahishwa na hizo rangi (kijani na manjano). Awali nilidhani kuwa ni sherehe za CCM na nimepigwa na butwaa kuona CUF imefikia hapo – maridhiano yamekuwa kuridhia bila mipaka.
Wallah mtaniona MBAYA, na uongozi wa mzalendo unazidi kuni-frustrate eti wanaziondoa mada zangu baada ya kupata instruction kutoka kwa akina Jussa-Bimani. OK. Twende mwendo huo huo mnaoutaka.
Lakini mjue kuwa ‘talk of the town’ ni kuwa watu wengi wanamlaumu Jussa kwa maneno yake aliyoyasema kuhusu kushidnwa kwa jimbo la uzini. Mara amesema kuwa ‘hawana interest na jimbo hilo’, mara hawakushindwa, kiboko yake ni ile kuwa ‘wameshindwa uzini kwa sababi jimbo limejaa watu wa bara’ – imetafsirika kama ubaguzi. Na bara wanarejesha kadi kwa wingi sasa.
Nyie mnichukie sana mimi, lakini mjue kuwa sheria ya kuanzisha vyama vingi TZ inataka kila chama ili kiwe halali lazima kitimize idadi fulani ya wanachama kwa kila mkoa – bara na zanzibar.
Tujue kuwa uhalali wa CUF unategemea bara unless tuvunje muungano na hatujakuwa tayari kufanya hivyo. Mimi niko tayari, tayari tena sana sana hata leo sasa hivi.
Sasa one day CUF inaweza kufutwa kwa sababu itakuw ahaina uhalali kwa idadi ya wanachama.
Endeleeni kuzitoa, kuzifuta mada zangu – very good. Lakini ONE DAY mtanikumbuka na kuona ukweli wangu. CUF inazidi kudorora. Viongozi wake wanaongoza kwa sasa ni wafedhuli tu, wahuni na watu wasiojua kuongoza. Najua kuwa mzalendo inapokea instruction kwa hao – wanataka mimi ninawsifu CUF hata kama wanavuruga na kuuza nchi – sitofanya hivyo. Lakini pia nitaendelea kusema ukweli, kama ndio msingi mkuu wa uislamu.
@Bi Salma na Waandishi wenzako
samahanini sana sio kam,a ninawaona hamujui kazi zenu au wapumbavu, bali naona Uwandishi wenu wa habari unatakiwa Uwende na Wakati huu tulionao.
Nikisema hivi nakusudia kwamba Zanzibar kunamambo Mengi yanatokea kila leo.
1. Kuna yale Mazuri ambayo yanaleta matumaini na yanataka yaripotiwe ili wananchi na viongozi/ miradi inayoshughulikia shuhili hizo . wapate kukaza kamba ya uchapaji kazi. lakini Hua hamuripoti habari hizo.
2. Kuna yale Mabaya ambayo yanatokea katika Nchi yetu, na Wananchi wanataka wayasikie ili waweze kukemea na kuwashitua Viongozi/ au kikundi kinachoshuhulika na kazi hizo. vile vile hamutoi habari hizo .
3. Kuna zile habari na pirika za maendeleo ya jamii au mazingira yanatokea kila Pembe ya visiwa vyetu . yanataka yawe REVELED lakini bado hamutoi habari.
Lakini Ikitokezea Siasa, kufungua Mikutano ya CCM, CUF, Chadema munaandika habari haraka sana. Kwani habari nilazima ziwe za Siasa tuuuuu?
Hebu jaribuni kuchunguza miradi mengine ambayo inazorota , Mazingira ambayo yanachafuliwa na muandike habari hizo. Kule Nungwi kwenye fukwe kumejaa Mipira ya CONDOMS , na WINE BORTLLES, RUBISH PAPERS, na PLASTICS za COCAIN. Lakini hamuyaoni haya wala Hamuyatafuti mukayaweka kwenye Blog yakajadiliwa.
Lakini Sheni, Maalim na viongozi wengine wakitoka tu munatuletea habari mbio mbio. Kwani Habbari za Unguja ni Siasa tuu?
Munashindwa na ASHAKH ambae hana ujuzi wa habari wala Utangazaji lakini anaweza kutuletea Habari tofauti zakimaendeleo na za Ubadhirifu. Kwanini musiige mifano hiyo.
watu wamechoka na Siasa, au ndio Munaogopa ku -ikosoa SUK na Mambo mengine ?..
Mujue kwamba Msema kweli kila siku AS humlinda na tunataka Waandishi wahabari wawe Independent na Open. Sio Munabania habari ni nyinyi ndio mutakao ikomboa Nchi kwakutoogopa na kua Wazalendo.
@Zamko,
Maneno yako ni kweli, labda uwasiliane na mwandishi huyu http://othmanmapara.blogspot.com/ huenda akakugaieni habari.
Huu ni mchango wangu tu
Nafuu kufanya kazi na Seif kuliko wale majuha Hamad Rashid na JUSSA
ILA SEIF LAZIMA UKABALI MABADILIKO YA LAZIMA NDANI CUF YANAHITAJIKA
BIG UP MH.MAZRUI