Picha:Kuna cha kuongeza hapo?
Written by administrator // 06/09/2010 // Habari-Picha // 5 Comments
- Jamani hakuna cha kuongeza hapo! Ujumbe upo wazi (tukapige kura sahihi)
- Mishahara ya vigogo!
- Ofisi zetu za Bunge
- THEN…. Tanzania Embassy in Washington
- A Class Room
- A Rural Primary School














5 Comments on "Picha:Kuna cha kuongeza hapo?"
Hizi ni shule au ni mabanda ya kufugia nguruwe!!? Kwa kweli hii ni Ari mpya nguvu mpya.
Pole sana Kikweeeeeeeeeeeeeeeeeete.
Inasikitisha tena inasikitisha sana sana kwani hapa inaonesha wazi wazi kuwa chini ya ccm na kiongozi wa nchi ni Kikwete au watu wa aina yake, hata uwape kuongoza nchi miaka milioni mia moja, kubwa ni kutoka kwenye umasikini kuelekea kwenye ufukara.
Hivi juzi katika kampeni za uchaguzi mkuu nimemsikia Kikwete, akitoa ahadi lukuki kwa wananchi. Mara meli kila penye mto na ziwa, mara maji, mara barabara na za motor way pia , shule na hospital. Jamani, miaka 5 iliyopita alikuwa wapi?..
Kwanini usirekebisha hayo yaliyomachoni unataka kuanza mapya. Hivyo nauliza kwa hawa viongozi wa Serikali ya ccm hizo ahadi wanazotoa ni za kweli au ni kejeli tu. Kili siku ahadi, hivyo mpaka lini?
Hao vijana wa skuli hapo ukiwaangalia wanatilisha huruma wakati katika ccm kuna viogozi wanaoitwa mafisadi ni mabilionea. Ari zaidi nguvu zaidi na kasi zaidi, hiyo ndio kauli mbiu ya kampeni za ccm katika uchaguzi mkuu baadae mwaka huu. Huu si umasikini ni ufukara tena wa mwisho.
kwa kweli hali hii inasktisha sana nainaumiza kichwa.
kuona viongoza tuliowapa majukumu yakutuongoza,
Halafu kuona siku baada yasiku umasikini naufukara unazidi,
baada yakupungua au kutokomea lakin chakushangaza ukiwaangalia wao vitumbo kaa mdudu chooko dooo mimi,
nahisi wanawazalendo wenzangu kwahali kama hii nikuyachapisha mabango yapictures nakuziweka hazarani ili
jamii ifahamu maana nina imani wengi wanafaham lakin kuna wale wanaodangaywa nakupigwa changa lamacho hawayaoni
wala hawamini kama kuna kama haya.
Sawa sasa mimi natoa wazo. Wazo langu ni kuwa kuanzia sasa viongozi wote wa siasa wawe wa kujitolea. Mwanasiasa sifa ya mwanzo ili akubaliwe kuwa mbunge au mwakilishi au mwenyekiti wa chama aweze kumudu kuhudhuria vikao kwa pesa zake binafsi, kama anataka kwenda UK kutangaza sera za chama chaka ajilipie mwenyewe gharama zote. Bunge na baraza la wawakilishi lifanywe kwenye skuli mojawapo itakayofanyiwa matengenezo. Balozi zote za Tanzania ziwe ni nyumba za watanzania wanaishi kwenye hizo nchi na wao wajitolee. Balozi nae ajitolee. Kwa mfano UK Elbatawi ajitolee kuwa balozi wa Tanzania, na ubalozi uwe ni nyumba yake ya council ya Barking. Atafanya shughuli zote za ubalozi lakini bila ya malipo.
ccm juu juu juu zaidi nimefurahishwa sana na maendeleo aliyotuletea ccm kwa takriban miaka 50 sasa kwa kweli ni mambo ya kufurahisha na kupigiwa mfano hasa ktk sekta ya elimu,
naw2aomba wana ccm wenzangu tuzidi kukaza kamba na kuiunga mkono serikali yetu kwa jitihata kubwa wanazotuonesha viongozi wetu kwa kweli wana ccm tutembee kifua mbele kwa maendeleo haya .
zaviongozi