Picha:Shein achukua fomu

Written by  //  20/08/2010  //  Habari-Picha  //  4 Comments


4 Comments on "Picha:Shein achukua fomu"

  1. Mtu-wakale 20/08/2010 kwa 9:15 um ·

    Jamani hiyo picha ya gari iliyozingirwa na ma-polisi wenye mabunduki au silaha zilizowekwa tayari tayari kwa kufetuliwa na kuangamiza watu. Hivyo hapo analindwa nani ama adui ninani.. hivyo Zanzibar ni kweli kuna amani?..

    Hakika picha hii haina tofauti na hali iliyoko Somalia kwa sasa, hapo ni katika hali ya hatari ulinzi kama vile nchi iko katika vita vya muda mrefu lakin, mapinduzi daima.

    Kusema kweli nchi zenye amani na usalama Duniani, viongozi wanaopenda raia na raia wanaopenda viongozi wao si aghlabu au ni nadra kuona ulinzi au askari kama hao hapo kwenye gari.

    Ulinzi huo kama ni wa Makamo wa Rais wa Tanzania ni hatari. Ulinzi kama huo anastahili Makamo wa Rais wa Marekani kwa kulingana na siasa za Marekani, zilivyo na kuwa raia wake wanamiliki silaha za kila namna. Zanzibar hakuna hata raia mmoja wa kawaida anaemiliki bunduki hata ya kupigia tumbili na mbwa koko labda, majambazi kutoka Tanzania Bara.

    Sababu ulinzi kama huo peke yake ni vitisho wa wananchi au tuseme kiongozi mwenyewe akiwa na ulizi wa namna hiyo huwa anaona fahari?..

  2. Hisba 20/08/2010 kwa 10:36 um ·

    Jamani, mimi bado moyo wangu nauona ni mzito kwani na yote haya yanayotokea nyumbani ya maridhiano na kura ya maoni lakini, jee CCM wako tayari kukubali watakaposhindwa? Suala hili hata maalim Haroun alilikwepa alipoulizwa na waandishi wa habari. Sheni, anaanza kulindwa kwa mashine guns. Hili ni zoezi kwani ikiwa atapelekwa ikulu kwa nguvu na ndio inavyoashiria basi hivyo ndivyo utakavyokuwa ulizi wake kwani atajua fika kuwa kaikeuka haki, na ukiikeuka haki basi M/Mungu hukukuminizia khofu katika moyo wako. Na kama atashindwa na ni muungwana kweli basi asikubali matokeo atakayopikiwa. Ndugu zangu, tuongezeni dua M/Mungu atuepushe na mtihani mkubwa ambao unaweza kutokezea. Kiti ni kitamu hata Komandoo alikiri na tunajua kuwa CCM kumwachia mpinzani kutawala ni kama kurejesha utawala wa Sultan na hilo ni gumu kwao. Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

  3. ahmed mohd 21/08/2010 kwa 12:41 mu ·

    jamani hii ni ishara ya kuwa kio ngozi huyu hakubaliki tena kabisa na ni kibaraka wa tanganyika ambae anataka kutumiwa kwa maslah ya watanganyika na ndo mana ukaona ulinzi wake kila siku unazidi kuimarishwa kama sijui kuna hali ya hatar au vipi m mungu atuepushie kibaraka huyo na waliomleta safar chukua chako mapema wakitaka wasitake watatupa nchi yetu kwani tunajua fika nchi hawato kubali kuitoa lakini litakalo kuwa na liwe safar hii tunapiga kura kwa amaan na utulivu wanzanzibar wote walio kuwa na uchungu na nchi yao hawawezi kumpa kura kibaraka huyuuu wa tanganyika atatutetea nini huyuu shein baada ya kupata urais kwa mabwana zake tanganyika walio mpa supa mtu ambae anaweza kutetea na akasema ukweli kwa sasa ni MAALIM SEIF PEKEEE HUU NDIO UKWELI SHEIN NI KIBARAKA TU.

  4. jesha kombo 21/08/2010 kwa 2:12 um ·

    Wazanzibar musiwe na wasi wasi na Sheni. Kuweni na wasi x2 na Dr Amani Karume? Sheni hapiki wala hapakuwi ikiwa Dr Amani atakuwa muungwana kuendeleza kiporo chake.Sheni hawezi kubebeshwa msalaba na Tume ya uchaguzi(ZEC)kama ikiwa Dr Amani atataka kweli tume iwe huru na mshindi kupewa haki yake basi uhakika basi inakuwa bado Dr Amani ni Rais na anazo nguvu zake. na tusijidanganye Mh Sheni hana ubavu hata kwao Mkanyakeni. huko kwao Mkanyageni watu wake hawamtaki itakuwa unguja?

Comments are now closed for this article.