Habari

SMZ iko wapi au iko likizo?

Pamoja na kuwa ukitenda kharamu moja, mema elfu moja yanayofuata yatakuwa kharamu. Kuna kila sababu ya kujuwa hii SMZ ipo au iko likizo?

Tokea kufanyika sherehe za mapinduzi January 12, ambapo huadhimishwa kwa kufungua miradi na shughuli za maendeleo, hatujasikia tena mambo yanafantika.

Serikali na watendaji wake wako kimya kama vile hii ni nyumba yao. Mawaziri wako kimya, Makatibu na wakurugenzi husikii wakisema au hata kufanya mipango yao.

Hata pale inaposemwa unaona kauli zilizojaa usanii mtupu, kiasi kila mtu anaona hapo ni kuondoshwa njiani. Kiasi kwamba kila mtu anatilia walakini

Hata kama imeingia kiukharamu bado inawajibika kuwatendea na kuwatimizia wananchi wake mahitaji yao. Kuna jengo la uwanja wa ndege tunataka kujuwa khatma yake. Kuna sector nzima ya afya na elimu hazina mabadiliko yoyote.

Sasa hivi msimu wa mvua unaendelea, wakulima wanahitaji mbegu, vifaa na mambo mengine ya kuendeleza kilimo.

Share: