Suala kutoka kwa Mtanganyika
Written by Stonetown (Kiongozi) // 07/02/2012 // Habari // 17 Comments
Mlitaka nini exactly katika muungano? Mlitaka haki ya kupewa ardhi
bara ambayo mnanyimwa? Mlitaka haki ya kuchimba mafuta pemba ambayo
mnajua yapo muyatumie peke yenu mkanyimwa haki hiyo? Mlitaka haki ya
kutumia Sharia Law na kuhukumu kesi kwa mahakama za makadhi
mkanyimwa? Mlitaka Sultani wa Oman awe anarudi kuzuru Zanzibar wakati
fulani fulani bila Visa mkakataliwa? Au kuna hofu kuwa…. kwa kuwa
bara kuna watu wengi zaidi kuliko Zanzibar, Wabara hawa wanaweza
kuipenda sana Zanzibar wakaamua kuvuka bahari, waje wakafurika huko na
wewe ukose kabisa mahali pa kulima karafuu?
Tatizo hasa ni nini? Mnataka nini ambacho mnakosa kwa kuwa katika Muungano.
Tafadhali fafanua; nijuze nielewe tatizo hasa liko wapi. Nina hamu ya
kukuelewa.




17 Comments on "Suala kutoka kwa Mtanganyika"
salamu wazanzibar, freedom that is what we want .
@Written by Stonetown (Kiongozi)
Mh Stonetown inaonekana umekumbwa na malaria sugu?, Hapa chakujiuliza kama unataka jawabu Mh? nikujiuliza jee kuna usawa wa Muungano kati ya Zanzibar na ilokuwa Tanganyika ambayo hivi saa inajita Tanzania?. a.
b. sasa ukipata jawabu ndio unaiweka Zanzibar katika nafasi gani ya Mezani kwenye Huu Muungano, wilaya ,Mkoa au kikata, kicha utajuwa mtawala na mtawaliowa nyupi mwenye kuumia.
KUSHEREWA KUFA KWA MUUNGANO NIHASARA KWETU SIE.
Stontown kifupi nikuwa jawabu ulitakalo ni hili? KAMA HUJIJUWI WEWE NI NANI, WATU WATAKWITA KWA JINA WALITAKALO?.
kuna msemo wa kiengereza unasema (Freedom is the better than gold and Diamond) maana kuwa huru samani yake ni kuchinda zahabu au almasi, sasa chakujiuliza jee Zanzibar iko huru?.
Mtu kupigwa na wazee wake haisi kuwa kaonewa, lakini kupigwa na wazee wasio wake ndio hujihisi kuwa ameonewa.
Sasa ingekuwa imetawaliwa na Wazanzibar wenyewe hata wawe ccm/asp basi tungejuwa ni vita vya ndugu lakini tumetawaliwa na michezi isio hata na huruma kila pembe ya nchi ni kambi za kikuria na hungojea kila uchaguzi wakafanya vitimbi vyao vya kishenzi na uchafu.
nakusha ngaaaaa au ndo bunuasi?
KIANCHUNISUMBUWA MIMI KUITAKA ZANZIBAR HURU NI KILE KIKUFANYACHO WEWE KUIKANA TANGANYIKA HURU
@ MTANGANYIKA
Mh. suala lako kwa kweli lina maana kubwa sana kwa yule anayelifahamu!! Ni sawa na lile SUALA unaloweza kumuuliza MAITI kuwa UTALALA VIPI NDANI YA MWANDANI ULIKUWA NA UPANA WA DHIRA’A MOJA TUU??
NAWAKILISHA
MCHONGOMA
Ndani ya maswala yako ndio yalimo majibu yako.
@MTANGANYIKA
Laana yenu ya utapeli ndio inayotufanya tuitake Zanzibar yetu.hatuna ufinyu wa ardhi katika dunia hii
@ palepangu,
HAKIKA SIJAKUPATA ( KUFAHAMU ) VIZURI, YAANI LIGHA HAPO IMENIPIGA CHENANGA.
NAOMBA UFAFANUZI KWA FAIDA YA WENGI.
Tunataka mengi tu ambayo hatuna uhuru nayo
Tunataka uhuru wetu kamili wa kujiamulia mambo yetu bila
ya kuingiliwa na mkoloni Tanganyika
Hivi sasa hatuna uhuru huo na kila tukitaka kujikwamua
kiuchumi basi mkoloni mtanganyika atafanya juu chini ili
aitowe tonge yetu kinywani.
Kwani kuna ubaya gani wa mtu kudai anachotaka na
kumforce mtu kumpa asichokitaka?
Tatizo ni dogo kuweni na serikali yenu na sisi tuwe na
serikali yetu na ujirani mwema ubaki kama kawaida sasa
hilo mbona nyinyi hamlitaki?.
MIMI SITOI JIBU MOJA KWA MOJA KWANZA NIKUULIZENI NYINYI KWANINI MNATUNG`ANG`ANI HAMJUI HATA KUPUUZWA KWANZA DAENI TANGANYIKA YENU
KWANI WAZANZIBARI WALIIUNGANA NA NYIE SIMMEMLAGHAI KARUME MPAKA KATUFIKISHAHAPA TUNADAI ZANZIBAR YETU KWA SABABU MUUNGANO SIO HALALI
Kwani sisi tumeungana ua tulivamiwa tukawa ngawira ya Tanganyika?.Naona tumuulize aliyejeruhi kwanini kajeruhi,si sawa kumwambia majeruhi kwanini umejeruhiwa.Ushahidi wa Kihistoria na usio na shaka ni kua Tanganyika ilifanya njama za makusudi kuvamia na kuipindulia mbali serikali ya Wazanzibari na kuitokomeza nchi ya Zanzibar kwenye pori la Tanganyika.Sasa wawauliza wazanzibari wana khofu ya nini?
@stonetown
Ikiwa maoni yangu yataendelea kubaki hapa basi yanaweza kufahamika zaidi na Wazanzibari wote wa Unguja na Pemba.
1. Suala lako ni zuri sana hasa kwavile umeonyesha picha ya wana Mapinduzi na ASP. Akiwemo Bw. Thabit Kombo wa kwanza kulia. Huyu babu alikua na Uchungu wa Wazanzibar na ndie yeye aliekua akipinga Muungano na ulipokuja mpango wakuiua ASP alikataa vikali sana. Akaonekana Mzee.
Hapa tunaona MBLP na mawaziri wamechanganyika makabila tofauti, na hii ndio ZANZIBAR na WAZANZIBARI walivyo. Wazanzibari ni Mchanganyiko wa makabila na rangi tofauti. Unaweza kua na asili ya KI-BARA, Ki ARABU, Ki-HINDI, Ki ZUNGU, na hata Ki MAKONDE.
Mimi nashangaa wale Wazanzibari wanajiona kwamba wao tu ndio wana haki ya Nchi hii na watu wenye asili za RANGI hawana haki.Mfano mdogo ni huu wa BILAL GHARIb aliesema Kuvunjika kwa MUUNGANO ni KURUDISHA USULTANI.
Mtu kama huyu naejaribu kujenga CHUKI ndanio ya RAIA anahatarisha Usalama wa Nchi na anatakiwa achukuliwe hatua haraka.
2. Wanzanzibari wanachokitaka sio Ubaguzi bali nikuwa na haki sawa kama NCHI ambayo imeungana na Nchi Nyengine. Wazanzibari wanataka MUUNGANO wa KILEO Utakao Tambua Mataifa mawili kuwa na haki sawa sawa. Yaani Tanganyika na Zanzibar kuwa na Muungano wa haki.
Akina Bilali Gharibu, Samia Suluhu, SHAMSI KAMARI VUAI na wengi wanaoitwa (Ati) ni Viongozi wanaowakilisha Muungano . HUU ni Udanganyifu mtupu.
Hawa wote kwa macho ya Mzanzibari wa karne ya 21 tunawaona ni VUIBARAKA WA TANGANYIKA ambao wanashirikiana na Vibaraka WENGINE wenye asili ya KIBARA ambao wanaishi Zanzibar. Kuimaliza Nchi yetu.
3. Wazanzibari hasa wa KUTOKA KISIWA CHA UNGUJA, hawajawa tayari kuikomboa Zanzibar na Wanawasiliti nduguzao kutoka KISIWA cha PEMBA. Huu ndio ukweli mutake musitake ukweli ni huu.
Itizame MAKUNDUCHI, NUNGWI , na DUNGA Ilivojaa makanisa na WANYAMWEZI. Licha yakua TUNATAWALIWA KIJESHI bali Tunavamiwa na idadi ya Wageni Unguja ni Kubwa kuliko Pemba. Hii yote Inamaanisha kwamba Unguja Wanajali Pesa kuliko UTU na Asili zao.
AKINA SHAMSI VUAI , SAMIA Suluhu wangesoma Nyayo za Sh. Amer TAJO, Thabit Kombo na wakaacha Ujinga wakuiuza Nchi.
@ zamko
Umeongea mi sina cha kuongeza zaidi. nagonga meza tu.
Kwa niaba ya waZanzibari/Wananchi wa **JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR** tunasema/tunatowa kauli zetu THAABIT kuwa tunataka turejeshewe nchi yetu ya Zanzibar!!! ikiwa HURRU kama vile mulivoikuta kabla ya mavamizi na kabla ya hii CANCER/SARATTAN ya huu MUUNGANO FEKI!! Kwa kweli tuko HOI, hebu tuachieni wenyewe tupate fursa angalau ya kuvuta PUMZI ZENYE HEWA SAFI!!!
Tuliuondowa UKOLONI kwa matumaini ya kuwa HURU katika nchi yetu ya Zanzibar!! Lakini lengo letu LIMEBERUKA ikawa tumetekwa na kutawaliwa ni wale WAKOLONI WALIO ASHADDI na dhaifu sana kushinda hata ule UKOLONI ulioukitawa enzi hizo za UJAHILI!!
Twasema twataka nchi yetu, tutawale wenyewetu, bila ya kuingiliwa katika mambo yetu ya ndani. Na pindi tukiridhika na nyinyi? tutaweza kufanya ALAKATI baina ya nchi na nchi na kuutekeleza ujirani mwema pindi ikijiri kufanyika hayo kwa ridhaa za pande mbili.
Kuna msemo unasema kuwa:- KHIYARI YA SHINDA UTUMWA.
Sasa khiyari zetu ni KUBANDUKANA NA NYINYI, hatutaki tena kutawaliwa kwa kisingizio cha haya maradhi hatari yanayojuilikana kwa jina la MUUNGANO FEKI.
NAWAKILISHA
MCHONGOMA
ama wewe kweli mtanganyika na wala si mtanga bahari hata kiswahili hujui basihata huoni? kila tukilia yomi nana bado unauliza kafa nani.