CUF ni chama pekee kinachowakilisha utaifa

Written by  //  28/07/2010  //  Nyaraka/Vitabu  //  9 Comments

Ili kuhakikisha maisha bora ya Mzanzibari, kuishi kwa usalama na amani,kuheshimu maisha na haki za binaadam za kila Mzanzibari, kumhakikishia kila Mzanzibari haki zote za kihalali za kidemokrasia, pana wajib mkubwa sana kwa wanasiasa wote wa Kizanzibari kutizama na kulinda maslahi yaWazanzibari wote kwa jumla bila ya kujali chama wakifuatacho.

Kwa hivyo viongozi wote wa kisiasa lazima wasahau tofauti zao na kuungana na kutizama maslahi ya nchi nzima. ASP,CCM(ZNZ), Um- ma Parti, ZNP na ZPPP lazima watambuwe kwamba wanawajib mkubwa sana kwa nchi yao na vizazi vyao, na bila ya kuungana watu wataendeleakuangamizana na nchi kuselelea nyuma milele.

CUF ni chama pekee kinachowakilisha mirengo yote hiyo tofauti Zanzibar. Kwa hivyo itakuwa jambo lamaana ikiwa viongozi wa ASP, CCM (ZNZ), Umma Party, ZNP na ZPPP wote wataingia katika CUF kuendeleza maslahi ya Zanzibar na CUF wenyewe kabla hawajaungwa mkono na vyama hivyo lazima wakubali kujibadilisha jina na kujiita ZUF na wakati huo huo kuwahakikishia uongozi wa juu wakuu wa vyama vyote hivyo vitakavyojiunga nao.

Nukuu hio imetolewa kwenye kitabu hiki:
ZANZIBAR DOLA, TAIFA NA NCHI HURU
by Dr. Yussuf S. Salim

Unaweza pata kopi hapa

9 Comments on "CUF ni chama pekee kinachowakilisha utaifa"

  1. mangala 28/07/2010 kwa 11:44 mu ·

    Huyo Ami Yussufu hayo ni mawazo yake tu, mimi sikubaliana nayo. CUF inawapenzi wengi huko nyumbani Pemba lakini haiwalikishi utaifa. CUF yawakilisha wanachama wao tu. Na sasa ni wakati wa wana CUF kubadilika kama tunataka kuleta utaifa na wenzetu wa Unguja. Wana CUF tuache ubinafsi, na tushiriki katika kuleta maendeleo ya kila ntu. Iwe kama zamani, ntu nke wa Pemba aolewa na wa Unguja, ntu mume wa Pemba aowa ntu nke wa Unguja. Tuchukue yale mazuri ya zamani bila ya jazba.

  2. binamu 28/07/2010 kwa 2:26 um ·

    Sasa hapa yakhe BANKWE, naona ushabbiki na upenzi wako unatupeleka kubaya.
    Kwa maoni yako kura ya NDIO ni kuikubali CUF na kuamini kuwa ni CUF pekee ndio yenye uwezo wa kuleta mabadiliko na amani ya Zanzibar. Napenda nikuamshe kidogo kwani mwenzangu naona unaota au tuseme unaweweseka mchana, hata giza halijaingia. Znz ni ya Wa znz-bar na sio ya ya CUF au wanaCUF, na hivyo hivyo CUF peke yao hawawezi kutupeleka kule tunakokutaka, bali mshikamano na mashirikiano ya wa ZNZ-bari wawe ni wana CUF, CCM, UPDP, Chadema Jahazi au ngalawa nk, juhudi za pamoja na mashirikiano ya pamoja ndio yatayotuhakikishia ushindi, tusidanganyike, kama ambavyo katika CCM kuna nazi kavu, makoroma na matunga (lisilo dafu wala koroma) basi ni hivyo hivyo katika CUF kuna watu hata ukiambiwa ni kiongozi basi unaingiwa na kichefuchefu.
    Ni hapo sasa unapoweza kusema serikali ya umoja wa kitaifa itakuwa na maana kimaendeleo kwa sababu itabidi tuhakikishe tunachukuwa nazi kavu za CUF, za CCM na pengine vyama vyengine muradi tukiwa na majemedari stadi basi ushindi wa vita unakuwa na uhakika.
    TUSHIRIKIANE KUANZIA KATIKA HII KURA YA MAONI TUONYESHE HAJA YA KUWA WAMOJA KWA MASLAHI YA UMOJA WETU NA FAIDA YA NCHI YETU NA BAADAE KARIBUNI TUUDHIHIRISHIE ULIMWENGU KUWA YES WE CAN kwa kufanya uchaguzi ulio wa salama, haki na utaoondosha fitna kwa kumtawaza yule mwenye haki na kutawazwa, tukielewa kuwa kuharibu mfumo mzima wa uchaguzi kuanzia upigaji mpaka utangazaji wa mshindi tutakuwa hatukufanya la maana lolote katika hata hili zowezi la kura ya maoni, na naomba salamu zangu hizi ziwafikie ZEC.

  3. mtu kwao 28/07/2010 kwa 2:40 um ·

    Mbona hivyo abaa cuf gani hiyo unayoisema?angalia basi kwanza hiyo mwakilishi na mbunge wa cuf ananyo ingia barazani yuko vururu halafu ndio ataweza kuongoza nchi mwache kwanza ajishuhulikie yeye mwenyewe kwanza halafu ndio achukue nchi

  4. hokani 28/07/2010 kwa 3:41 um ·

    @mangala na @binamu,NAONA MAELEZO YENU YANAMTOSHA MUANDIKA MADA KATIKA KUFAHAMU UBAYA WA USHABIKI WAKE.HAPA NINAPATA PICHA HALISI JINSI WATU WA NAMNA HII WAKIWA PAMOJA NI NAMNA GANI YA UTUMBO WANAOZUNGUMZA.MTU AU KIKUNDI CHA WATU KUNAHITAJI KUWEPO WAKOSOWAJI.CUF BILA YA KUWEPO KWA CHAMA KINGINE KUNA HATARI YA KUWA NA KIBURI,MAANA HIYO NI HALI YA MAUMBILE YA WANAADAMU.

  5. Yussuf Saleh 28/07/2010 kwa 3:44 um ·

    Asalaam aleykum

    Ningependa kuwaarifu wasomaji wa nukuu hiyo ya “Zanzibar Dola, Taifa na Nchi Huru” kwamba kijitabu hicho kiliandikwa mwaka 1994. Umuhimu wa ujumbe huo ni kuonyesha kwamba ili kuinusuru Zanzibar palihitajika Umoja wa Wazanzibar wa namna moja au nyengine, jambo ambalo limejichomoza leo miaka sita (6) baadae yaani uwezekano wa kuleta mfumo wa SUK na sio lazim ZUF.

    Wasalaam
    Yussuf

  6. ole 28/07/2010 kwa 5:29 um ·

    A/aleykum Wazalendo.

    Shukurani sana kwa muandishi, ni mada ndogo lakini ina ujumbe mzito. Lakini mimi sitaki kupinga wala kukubali maoni ya muandishi kwa vile sina uhakika na kile hasa alichokusudia.

    Bali napenda kuchangia kwa kutoa mawazo mapya kinyume na wachingiaji wenzangu.

    Historia itabakia kuwa ni historia hatuna budi tuende na wakati. Kurudisha tena hadithi za Umma party, A.S.P, ZNPP,ni kupoteza dira na muelekeo.

    Hivi sasa Zanzibar inahitaji idea mpya na muelekeo wa kisasa, kwani vizazi vya leo vimechoshwa na mambo ya 1964.

    Hao ndio walio ifikisha ZANZIBAR HAPA ILIPO. Kwa maana hiyo let us forget about past tuanze upya kwani hata hao waasisi vyama hivyo hawapo tena duniani.

    Kwa nini tufuate mawazo yao ambayo ndio yaliotuletea matatizo yote haya tulionayo, wakati umefika wa kutoa fikra na muelekeo mpya.
    Zanzibar mpya, ari mpya.

  7. Dr.Yussuf 28/07/2010 kwa 6:29 um ·

    Asalaam aleykum

    Ningependa kuwaarifu wasomaji wa nukuu hiyo ya “Zanzibar Dola, Taifa na Nchi Huru” kwamba kijitabu hicho kiliandikwa mwaka 1994. Umuhimu wa ujumbe huo ni kuonyesha kwamba ili kuinusuru Zanzibar palihitajika Umoja wa Wazanzibar wa namna moja au nyengine, jambo ambalo limejichomoza leo miaka sita (6) baadae yaani uwezekano wa kuleta mfumo wa SUK na sio lazim ZUF.

    Wasalaam
    Yussuf

  8. ibra 28/07/2010 kwa 10:12 um ·

    ASALAM ALEYKUM

    NDUGU ZANGU NAONA HAMUJA MUELEWA MTOWA MADA, AU HATA MUKISOMA KWANZA JARIBU KUTAFAKARI ZAIDI ILI UPATE KUELEWA HATA IKIBIDI REJEA TENA HATA MARA 3 ,,, KWA UPEO WANGU MIMI KUWA NA UFAHAMU WANGU ,,,HAKUNA CHAMA CHOCHOTE CHA KISIASA TANGANYIKA NA ZANZIBAR HII KINACHO WAPIGIYA DEBE WANZANZIBAR ISIPOKUWA CUF ,NA KWELI HATA HAO WATAWALA CCM NA SEREKALI YAO HAWANA LOLOTE NA WANALO TUTETEA SISI WAZANZIBAR ,KUNA MAMBO MANGAPI YA WAZANZIBAR YANAAMULIWA BARA ?TENA MAMBO MUHIMU !LEO HII WAZANZIBAR HATUNA UTAIFA ,UNALIJUWA HILO ?UKIENDA POPOTE PALE DUNIA WEWE MZANZIBAR HAUJULIKANI!

  9. hokani 28/07/2010 kwa 11:22 um ·

    @ibra;Ndugu yangu mimi sikubaliani na yeyote anayesema kuwa vyama vya upinzani vyengine kuwa havichukui bidii au kuwapigia debe wazanzibari juu ya haki zao.Ni ukweli usiopingika kuwa kadri unavyokiona chama hakina wafuasi wengi huko bara na visiwani,basi ndivyo kinavyouchukia muungano, na muungano ndio shina la maangamizi ya wazanzibari.Sielezi haya kwa hisia tu bali kwa uzoefu wa ushiriki wa mambo haya.Tunapaswa kuwa na tahadhari katika kutetea haki yetu,maana kwa kukosa kufanya hivyo tunaweza kuwalaumu wasiohusika juu ya matatizo yetu.

Comments are now closed for this article.