KURA YA MAONI: WALIOJIANDIKISHA NA WALIOPIGA KURA

Written by  //  04/08/2010  //  Nyaraka/Vitabu  //  8 Comments

Utangulizi:
Ufuatao ni mjadala juu ya kura nzima ya maoni ilivyokwenda, wangapi wamepiga NDIO, HAPA na waliochagua kutokupiga kura kabisa!

Waaleykum salaam

Kwa hili watu tofauti wanaweza kuwa na uchu tofauti wa kutaka kuelimika zaidi.

Kwa mfano kwa nini hawa ndugu zetu wameamua kuto piga kura

Jee hawakupata elimu ya kutosha na wanahitaji elimu zaidi ili kutambua umuhimu wa kura kama hiyo. Kwa hivyo itabidi wajulikane ili waweze kuelekezewa elimu itakikanayo. Pengine hata na wale waliopiga Hapana wanahitaji elimu zaidi kuona kama nafasi kama ile wakiipata tena huenda wakachukua msimamo mwengine.

Jee walitishwa na kuogopa au waliogopa wenyewe?

Walivunjika moyo na matokeo ya kura za nyuma?

Waliepuka kwa sababu walijua kwamba ushindi utapatikana au walikuwa na wasiwasi kwamba hapatakuwa na ushindi ?

Jee kumepitika kizungumkuti kutoka na mikono ya wale waliokuwa wa Hapana ndani au nje ya ZEC ?

Jee ZEC inaweza kusawazisha baadhi ya makosefu? Ili chaguzi zijazo ziwe bora zaidi ?

Jee ni bahati tu kwamba kuhusu Pemba ni mtindo wa asili mia 20% ndio wasiopiga kura wakati Unguja mtindo wa mtiririko umekuwa wa asili mia 30% ?

Mtu unaweza kujiuuliza kwa nini majimbo manane ya Hapana yameweza kupata idadi ya 95 elfu wakati majimbo 42 ya NDIO yamepata elfu 188 tu.

Matokeo yaliyotolewa ni ya vituo 1212 vya kupiga kura wakati vituo vyote ni 1292. Hesabu za vituo 80 zimekwenda wapi?

Baadhi yetu tulikuwa tunatarajia ushindi wa asili mia 75-80%. Kwa mujib wa jinsi maridhiano yalivyopokewa asili mia 66.4% kwetu wengine haitoshi hata kidogo.

Utafiti wa kina na waki sayansi unatakikana ili tuendeleze Demokrasia ya kuwekewa mfano hasa barani Afrika. Nyota ya Zanzibar hivi sasa inan“gara ingelikuwa vizuri kama tukaipiga polish ili in“gare zaidi. Zuri tuzidi kulizurisha na baya tulikimbie.

Naomba kutoa hoja.

Wasalaam
Yussuf

PEMBA

WALIOJIANDIKISHA

WALIOPIGAKURA

WASIOPIGAKURA

% Waliopiga kura

%WASIOPIGA

1

MKANYAGENI

6142

4623

1519

75.26864214

24.73136

2

WETE

8422

6868

1554

81.54832581

18.45167

3

MTAMBILE

6634

5305

1329

79.9668375

20.03316

4

OLE

7206

6361

845

88.27366084

11.72634

5

CHAKE

8195

6314

1881

77.04697987

22.95302

6

ZIWANI

7454

6191

1263

83.05607727

16.94392

7

WAWI

9355

7100

2255

75.89524319

24.10476

8

KIWANI

5995

4550

1445

75.89658048

24.10342

9

CHAMBANI

4835

3968

867

82.06825233

17.93175

10

KONDE

7443

5664

1779

76.09834744

23.90165

11

GANDO

6755

5545

1210

82.08734271

17.91266

12

KOJANI

7440

6485

955

87.16397849

12.83602

13

MTAMBWE

6155

5332

823

86.62875711

13.37124

14

MKOANI

6972

5014

1958

71.91623637

28.08376

15

CHONGA

7325

5533

1792

75.53583618

24.46416

16

MGOGONI

6951

5836

1115

83.95914257

16.04086

17

MICHEWENI

7988

6694

1294

83.80070105

16.1993

18

TUMBE

7692

6367

1325

82.77431097

17.22569

TOTAL PEMBA

128959

103750

25209

80.49918068

19.50082

UNGUJA

1

BUMBWINI

7170

4514

2656

62.9567643

37.04324

2

MJIMKONGWE

7495

5646

1849

75.33022015

24.66978

3

TUMBATU

9424

6689

2735

70.97835314

29.02165

4

KIKWAJUNI

7910

5549

2361

70.1517067

29.84829

5

CHUMBUNI

10379

7043

3336

67.85817516

32.14182

6

KIEMBESAMAKI

4698

2810

1888

59.81268625

40.18731

7

MAKUNDUCHI

8689

6488

2201

74.66912188

25.33088

8

FUONI

10884

6560

4324

60.27195884

39.72804

9

KOANI

12034

7898

4136

65.63071298

34.36929

10

MAGOGONI

10141

6887

3254

67.91243467

32.08757

11

CHAANI

8103

5357

2746

66.1113168

33.88868

12

DONGE

7872

4645

3227

59.00660569

40.99339

13

JANG’OMBE

9173

6431

2742

70.10792543

29.89207

14

MATEMWE

6325

3997

2328

63.19367589

36.80632

15

MTONI

9672

7164

2508

74.06947891

25.93052

16

RAHALEO

7269

4960

2309

68.23497042

31.76503

17

AMANI

7641

5405

2236

70.73681455

29.26319

18

BUBUBU

9809

6741

3068

68.72260169

31.2774

19

CHWAKA

10402

6726

3676

64.66064218

35.33936

20

DIMANI

12813

8959

3854

69.92117381

30.07883

21

DOLE

8017

5101

2916

63.627292

36.37271

22

NUNGWI

8436

5777

2659

68.48032243

31.51968

23

KITOPE

7737

4723

3014

61.04433243

38.95567

24

UZINI

8743

5902

2841

67.50543292

32.49457

25

KWAHANI

7497

4614

2883

61.54461785

38.45538

26

KWAMTIPURA

10767

7248

3519

67.31680134

32.6832

27

MAGOMENI

9912

6924

2988

69.85472155

30.14528

28

MFENESINI

7247

5670

1577

78.23927142

21.76073

29

MKWAJUNI

6769

4584

2185

67.72049047

32.27951

30

MPENDAE

9489

6781

2708

71.46169249

28.53831

31

MUYUNI

8201

6178

2023

75.33227655

24.66772

32

MWANAKWEREKWE

8062

5318

2744

65.9637807

34.03622

TOTAL UNGUJA

278780

189289

89491

67.76338661

32.23661

TOTAL ZNZ

407739

293039

114700

71.86

28.14

8 Comments on "KURA YA MAONI: WALIOJIANDIKISHA NA WALIOPIGA KURA"

  1. ibra 04/08/2010 kwa 10:21 um ·

    bwana mtowa mada umesema kuwa matokeo yaloizinishwa ni ya vituo 1212,na jumla ya vituo unasema kuwa ni 1292 hebu tuwekee wazi ili tupate kuelewa na tujuwe jinsi gani ya kuchangia ,hivyo vituo vengine vya kupigiya kura unaweza kututajia kwa majina yake ?ambavyo umesema kuwa vituo 80 matokeo yake hayaonekani ,,

  2. Yussuf Saleh 04/08/2010 kwa 10:41 um ·

    Hayo hapo chini ndio matokeo yaliyoletwa na ZEC katika mtandao wao. Sasa inaonekana wamebadilisha. Ingia kwenye mtandao.

    Zanzibar Referendum Results for Country : National

    ——————————————————————————–
    CandidateName Votes
    NDIO / YES 175476
    HAPANA / NO 90588

    ResisteredVoters 407669
    ValidVotes 266064
    InvalidVotes 8309
    TotalTurnOut 274373
    PercentTurnOut 67.00%
    PollingStationsPublished 1210 of 1292

  3. ashakh 04/08/2010 kwa 11:07 um ·

    Wazzalendo,

    Naogopa sana komputer hasa katika masuala muhimu kama. Wakati unajiribu kuganga kumbe unaharibu.

    Mwandishi katika Total yake ya waliojiandikisha kapata 407,739 wakati ZEC yakwake ni 407,669. Tayari makosa yameshatokea. Sasa tumuamini nani?

    Hili ni suala ambalo ningewaomba Wazalendo na ZEC kuwa makini sana katika data transfer. Ni kidole tu ndio kinacho bonyeza, kosa utalijuwa baadae. Ni rahisi katika hali kama hii kuandika makosa.

  4. Yussuf Saleh 04/08/2010 kwa 11:14 um ·

    Hiyo total si yangu imetiwa na mzalendo, Nambari nilizotumia mimi ni tatu tu nazo ni za vituo tu. 1292, 1212 n1 80. Hiyo jeduweli si yangu.

    Nambari za hapo juu zinatoka kwa mtanda wa ZEC zimekopiwa na kupestiwa. Hiyo ndio mibonyezo yangu.

  5. muunguja 05/08/2010 kwa 12:02 mu ·

    mimi sikuelewi mtoa mada unataka nini ushindi ni ushindi tu hata kama ni wa goli moja.usiwe greedy kiasi hicho ,binadamu wametafautiana.kuna wengine wanapenda wanawake wanene wengine wembamba.wengine wanapenda kula kunde wengine hawapendi.wengine wanapenda nyama ya bata kuliko kuku.
    uchaguzi wa marekani ulikuwa na 63% turn out.uk ulikuwa si zaidi ya 70% turn out kama sikosei.kwa ufupi hili swala si nyumbani peke yake hata kwa wenzetu vile vile.
    nyumbani siasa imebadilika tafauti na miaka ya nyuma watu inaonekana wamechoka na mashaka ya siasa.kila mtu yuko busy na kutafuta maisha.
    la mwisho naomba uondoe conspiracy theories kwasababu kwa mujibu habari cuf waliweka waangalizi wao vituo vyote na wakakubali matokeo.
    kuna baadhi ya cuf wameweka hapana na vile vile ccm kibao wameweka hapana na hao hao ccm wameweka ndio.

  6. Salim Mohamed 05/08/2010 kwa 12:10 mu ·

    Mimi kwa mawazo yangu naona hao walikua hawakupiga kura ni silaha za CCM,ambazo zitatuliza october.Niwale watu wanaochukuliwa kwa magari kutoka jimbo moja kwenda jingine,ambao hawakuchukuliwa katika kura ya maoni.na tayari wameshaandikiswa.

  7. kassim 05/08/2010 kwa 10:41 mu ·

    Muunguja hata nami najiuliza, hii kutaka kujuwa kwanini watu hawajaenda kupiga kura sijuwi ina maana gani na sijuwi ina uzito gani? Au ndio kusema watu warudiye tena hii kura ya maoni?

    Kenya ya kwao wanategemea watakao jitokeza ni 60% Jee hawa 40% ndio wawe sababu ya kuzuwiya kura ya maoni? Mtu kama umepata fursa ya kutowa maoni yako, ni vyema kwenda kutumia haki yako, vyenginevyo funga mdomo wako pale utakapo ona mambo yamekwenda vibaya. nchi kama Australia kupiga kura ni lazima, kuepusha manunguniko na kuwapa fursa watu kutowa maoni yao.

    Jambo jengie, watu wana njaa, si hasha mwengine yupo songea, mwengine kaajiriwa na mtaliana, mwengine yupo spitali, mwengine kata kuja kutoka Dar hakupata safari…

    Huu si wakati wa kutafuta choko choko. Ni wakati wa kufikiria sisi kama wananchi wa kawaida tutafanya vipi kuisaidia hii serikali yetu na serikali itawajibika vipi kuhakikisha hawawaangushi wananchi wao. Uchaguzi utakwendaje. Kwa upande wa tume wamejifunza nini kutokana na kura ya maoni jinsi walivyo weza kupiga kura kwa salama usalimini. Polisi, jeshi, valantia, mgambo… jee kweli munahitajika kwenye kupiga kura? Jawabu nadhani hapana. Kama kuwepo ni polisi na wawili watatu wanatosha… sisi tuna nidhamu kwenye mambo yetu

  8. chunaameirhaji 05/08/2010 kwa 5:16 um ·

    assalam aleykum
    tushukuru mungu uchaguzi umekwisha kwa salama, na ushindi niushindi tu.lakini ingekuwa kuwa vizuri kama wataalamu (kama wapo )wetu wakafuatilia na kufanya utafiti katika kasoro ndogo ndogo kamahizo zinazohusu jamii kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu,wenzetu wanaendelea kasababu wao hawapuuzi kitu ,kila jambo huwa wanalifanyia utafiti.kwa nini idadi kubwa ya watu hawakushiriki katika kutoa maoni yao ? au ndo kama biharusi akikaa kimya maana yake ndo kakubali???

Comments are now closed for this article.