Nyaraka za kongomano-Makala ya Prof.Mohd Adam

Written by  //  22/07/2010  //  Nyaraka/Vitabu  //  3 Comments


[ipaper id=34736057 key=key-wut1j9r6xmmt8693th1 mode=list]

3 Comments on "Nyaraka za kongomano-Makala ya Prof.Mohd Adam"

  1. zinduka 23/07/2010 kwa 10:54 mu ·

    Hii Makala ni Safi sana, Muandishi inaonyesha ni mtu aliebobea na kama nikijana basi hawa ndio wanaotakiwa kuwa Future leaders kwa Zanzibar yetu, kwani haja base kwa upande wowote wa Mielekeo ilioko Hapa Zanzibar,

    Pia heko kwa MUWAZA kwa kujitahidi kutetea Maslahi ya Visiwa vyetu, Shikeni Uzi huo huo nasisi tuko nyuma yenu.
    Ahsante.

  2. Msema Kweli 23/07/2010 kwa 12:36 um ·

    @ Zinduka.

    Naungana nawe kwa kumpongeza Dr. Mohammed Adam, na pia nakujulisha kuwa ni kijana mchapa kazi asiepoteza muda wake kwa mambo ya kipuuzi, na ndio maana akafikia alipofika. Na alipokuwa muajiriwa wa SMZ mara nyingi akikwaruzana na viongozi na mabosi wake kwasababu akiuona upuuzi anauita upuuzi (he calls a SPADE a Spade) – My kind of people.

    Hata hivyo nina wasiwasi na hicho kichwa cha habari, kwani kwa kipindi alichomaliza masomo yake ya PhD mpaka sasa, sidhai kuwa ameshafikia U-Professa. Inawezekana kuwa ni Associate Professor.

    Nitafurahi zaidi na naamini kama atakusudia, na kwa uwezo wa Allah basi atafikia u-Professor, lakini namshauri alieandika/alieweka hiyo habari bora tuwe na hadhari na kutowa informatin ambazo si sahihi.

  3. Junius 23/07/2010 kwa 5:27 um ·

    Naungana na Dr.Mo’hd Adam katika suala la kutumia fursa hii ya kuleta mshikamano zanzibar kama ni hatua zaidi ya kuirejeshea Zanzibar heshima yake ndani na nje ya muungano. Kazungumza umuhimu wa kutumia njia kama hii ya kuwashirikisha wananchi katika maamuzi makubwa ya mustakbali wa nchi yao.

    Kagusia suala la muungano ambao ni muonekana katika fikra za wazanzibar wengi umechangia kuzotesha maendeleo muhimu kwa watu wake,mfano zanzibar kukosa kushirikiana na washirika wa kimaendeleo katika nyanja ya kimataifa kwa kubanwa na muungano.

    Dr.Adam, amegusa kuwa suala la mambo ya nje ni la muungano, lakini masuala ya ushirikiano wa kimataifa kwa misada ya maendeleo yalikuja baadae. Hapa pamekuwa na mivutano kweli,kwani Zanzibar inashindwa kutafuta wahisani wa kimaendeleo wanaofanana na mila na tamaduni zake ambao wapo willing kutoa misaada bila ya masharti magumu.

    Hatua tuliyofikia ni muhimu kwa wawakilishi wetu katika vyombo vya kimaamuzi wanapokuwa huko wawe wanakuwa kitu kimoja kuhakikisha kuwa mambo kama haya yanapatiwa ufumbuzi kikatiba na sheria. Na kama kweli watashikamana kwa haki na yakini basi katiba si msahafu, mambo mengi yanaweza kurekebishwa kwa kuanzia na njia kama hizi za maoni ya wananchi moja kwa moja na kuiwezesha zanzibar kujitaftia fursa za kimaendeleo.
    MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
    J

Comments are now closed for this article.