Docs:Nyaraka nyeti za kujikumbushia yaliojiri
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 19/08/2010 // Nyaraka/Vitabu // 5 Comments
- Tanganyika Citizen Act
- Union Act
- An Act to Change the Name of United Republic of Tanganyika and Znz
Nyaraka zimeletwa kama ni ukumbusho kuwa Tanganyika ilikuwa taifa ambalo linafanana sana na nchi tunayodaiwa leo kuwa ati ndio imebadilika jina na kuitwa Tanzania.Utafiti unaendelea kuweza kupata jawabu ni kwanini wenzetu wamekuwa wakikimbia kuwa na taifa la Tanganyika..kunani hapa!
Mwandishi Lula yeye amefika hadi kusema kuwa taifa lake ni urithi wa wakoloni.Hii ni kumaanisha kuwa wengi hawataki kusikia kama Tanganyika ilikuwa ni taifa ambalo lipo limejibadili jina kiujanja na kujiita Tanzania kwa kisingizio cha Muungano.
Anyways, nyaraka hizo zinaweza saidia kuonesha picha halisi.
Ukipenda pia tunarudia hapa kukumbushana tuu kuwa nembo ya Tanganyika ndio ile tunayoambiwa leo kuwa imegeuka jina na kujitanua mipaka kwa kutumia jina la Tanzania.See foto below for clarification and compare it with the original foto from those documents.
- Nembo ya Tanganyika/Tanzania
- Nembo ya Tanganyika
Tanganyika Citizen Act:
[ipaper id=36110643 key=key-193e1uyqa8w90m0kv0fo mode=list]
Union Act:
[ipaper id=24823426 key=key-1dlp0tnzt4n91utuby5c mode=list]
An Act to Change the Name of United Republic of Tanganyika and Znz
[ipaper id=36112545 key=key-99do17m35yt5ci5vn8m mode=list]







5 Comments on "Docs:Nyaraka nyeti za kujikumbushia yaliojiri"
Salaamndugu mtoa mada,,mimi sinabudi ili kukushukuru kabisa kwakutuekea wazi hizi katiba .Mtu akitakakuzisoma vizuri inabidi Azoom (+), ndipo ataweza kusoma. Naamini hawa wana sheria, wasomi wa Tanganyika wanalijua hili lakini wanajifanya vichwa ngumu na ku-nga-ngania Muungano wa Ukoma. ambao umevikomaza Visiwa vyetu vya Unguja na Pemba kiuchumi, kimaendeleo, kijamii, kielimu,kikalture na hata kidini kwa muda wa miaka 47.
Haya : Phil-Mikael wewe unajiita msomi na umesoma mlimani hebu nenda kwenye hizi nembona na ufanye analysis ya kitaalamu. Ukesha tupatie jibu Kwenye nembo yenu ya Adam na Hawa. Ni wapi manapo re-present Visiwa vya Zanzibar na kuonesha/maanisha kwamba tumeungana na Tanganyika?
Sasa wazanzibari wanapokua na bendera yao, wimbo wa taifa lao na nembo yao ya visiwa viwili. hawakua wajinga bali walijua kwamba huu ni Muungano Batil ambao ulifanywa na Nyerere na bunge lake la Tangayika kwa kuimeza na ku-idhibiti Zanzibaer na Uchumi wake.
Wazanzibariwalijua kuna siku itafika na mambo yatakua nje, musijitie Ati mumeungana na Zanzibar kwakisingizio cha Umoja wa Africa. Mbona hamukwenda Kenya au Uganda? Na hata hao cousins zenu Warundi, wazambia waliko chini ya pua hamukutaka kuungana nao.
Ameona avuke mawimbi ya Bahari na afanye Muungano hewa. jiulizani wenyewe Nyerere alifuata nini Visiwani? Wasomi wangampi waliuwa-wa wakati wa Uongozi wake? Kwanini SH. Abeid Amani karume aliuliwa before 26/april 1972?
Wako wapi wal Waislamu waanzilishi la Taifa la Tanganyikaambao pia waliomtoa Nyerere Butiama na kumleta Dar-es salaam kumuonyesha Jiji?
Jibu Nyere he saw a good portion of Zanzibaris foregn Currence, oils & gus, turisim and above all was religion.
So when Tanganyikans News papers claim that Zanzibaris people has been educated with your kauzus money or karanga. ” How could you help someone while you can not help yourself irst”? Therefore those karangas should be enough to feed your big bellis (yourself) first before even cross the Indean Ocean & help us. This claim was absolutely rubish & you seems to be confused.
Nawasilisha
P:S
Duplicated by admin,
Duh hawa jamaa wanajifanya wanaakili sana sio, lakini mambo sasa tunaanza kuwekewa hadharani, yaani ukiusoma hata hio Articles of Union basi kipo kipengele kwamba huu mkataba ulikuwa ni wa muda tu, yaani interim period, hebu naomba hao wanasheria wetu wasome hicho kipengele cha (iii) kinasema “During the interim period the Constitution of the United Republic shall be the Constitution of Tanganyika so modified as to provide for” …
Ingawaje hapa pia kuna ujinga ulifanywa na hao Wazanzibar wakakubali katiba ya Watanganyika iwe ndio katiba halisi lakini kwa tafsiri hapa tunaona huu mkataba ulikuwa ni wa muda tu na kwa bahati mbaya huo muda wenyewe haukuoneshwa ndani ya huo mkataba. Nafikiri kwa kuwa Karume alilijuwa hilo ndio ikawa anasema Muungano ni kama koti likikubana unalivuwa tu.
Kama ule muda ulikuwa ukisubiriwa basi nahisi umeshafika na ukimaliza tu uchaguzi tunataka kura ya maoni juu ya muungano.
hii nembo ni ileile imeongezwa bendera tu duh!!
kwa wale wote wanao iita nembo ya tanyangika ni Adam na Hawa naomba wawache mana ni dhambi kuifananisha nembo ile na mtume wa M/Mungu ni vyema kuiita nyerere na maria nyerere kama wengine tunavoiita.
Halafu wanatwambia NYERERE kawaambia hakutaka ionekane Tanganyika inaimeza zanzibar ndio sababu hakuajiria serikali moja to start with. SASA angalieni uthibitisho wa lengo la NYERERE kama tunavyowakumbusha wenzetu wale walio vichwa ngumu.
Mara tu baada ya NYERERE kudhania alishamtia mbaroni KATUME kimaarifa kwavile hakusoma, ndipo alipoaanza kuimung’unyuwa ZANZIBAR taratibu kwa lengo lile lile alolikanusha KUIMEZA. Hati hiyo ni mojawapo ya hati nyingi tu za kiuhadaa hadaa, kijinga jinga, kimazabe, kilaghai, kimabavu na kila namna iliyokuwa ikikidhi utaratibu wake wa kumegua pande la ZANZIBAR. Hakika alikua kama chatu kabaka MBWA. Huwa anammeza taratibu na huku jinwa na mwili wake wote ukishindwa kujificha kwa mpanuko na mvimbo ulio dhahiri ukidhihirisha nia yake.
Lapili ni kwamba WAZANZIBARI wanapopiga kelele kuwa wanaburuzwa, huchekwa wakaonekana wapumbavu. Wakidai muungano umeendeshwa kiholela na kinyemela, huonekena akili zimepumgua.
Nembo hiyo imedhihirisha mambo mawili muhimu mno mapema katika wa ndoa ya NYERERE NA KARUME ya kuozesha NCHI.
Kwanza na la umuhimu kabisa ni pale NYEREREalipothubutu kubadilisha jina la nchi huku akitia saini yake na wadau wake kwaniaba ya RAIS NA ILHALI AKIJUWA FIKA KUWA NCHI ZIMEUNGANA KUKIWA KUMEBAKIA MARAISI WAWILI HALALI NA HIYO NI KUTOKANA NA MAKUBALIANO MAMA WALIOKUBALIANA NA MNDOA MWENZIE MASIKU MACHACHE TU YALIOPITA. Sasa angalieni pale watu, hasa jamaa zake, wanapo mpa Nyerere cheo cha ujanja. Ametaja neno RAIS bila kutaja jina. Jee kuna nchi yenye RAIS asojinaa?. Alijiona mjanja kwasababu alijuwa fika kuwa angeandika RAIS NYERERE basi KARUME angelikuja juu na MUUNGANO ungeliishia CHUMBE MITHALI YA AZIMIO LA ARUSHA. Yawezekana ujanja huo ulisaidia kumpiga KARUME chenga ya mwili. Alichokosa kukifahamu NYERERE kwa mbinu hiyo, ni kwamba hata mimi mlala hoi kisharia mpaka leo hii ningeweza kumfunga kwa kutenda usaliti. Kamuulizeni Msekwa aliyeweka saini kama karani shahidi kubadili jina lanchi. Sasa mtu mjanja hafanyi mambo yanayotowa mwanya wa kumfunga kisharia.
NA MABMO KAMA HAYO KWA BAHATI MBAYA AU NZURI, INATAGEMEA UMEELEMEA MWEGA GANI, NI MENGI MNO NDOANI, MUUNGANONI. NDIO MAMBO HAYO WAZANZIBARI HUYAPIGIA KELELE WAKAONEKANA MACHIZI. NDIO MAMBO HAYO YALIYO KERO ZA MUUNGANO. MAMBO HAYO YANATENDWA KWA MAKUSUDI, TANGU KAYAANZA NYERERE HADI KEO, NA NDIO SABABU WATAENDAJI WANAKIRI KIUJANJA UJANJA WAKIDHANI NI UJANJA. NDIO MAMBO HAYO WAZANZIBARI WAMEAMUWA KUJIAMULIA. NA KWAVILE HAIKUWA UJANJA TO START WITH NDIO MAANA ZANZIBAR HAIBURUZIKI MAHAKAMANI WALA HAITEKEKI KIJESHI.
NAUNGANA NA WATANZANIA WOTE WAPENDA AMANI BARA NA VISIWANI, LIWE LETU USHIRIKA NA KUITUNZA AMANI. AFRIKA MASHARIKI KULIKUWA NA NCHI NNE TUKIOWANA NA KUCHEKA, NA SASA ZIPO NNE NCHI, TWAPENDANA TUMEFIKA.
KAZI KWETU.
Kwa upande wangu nawasilisha ombi kwa serikali ya Zanzibar watuekee copy ambayo inaonesha kuwa huu mkataba wa Muungano ulikuwa ratified na Chombo cha kutunga Sheria cha Zanzibar cha wakati huo.
Kama hakuna copy na ikiwa huu mkataba haukuwa ratified na chombo hicho hapa Zanzibar basi tujuwe huu mkataba ulitakiwa uwe ratified na pande zote mbili na sio Tanganyika tu, kuthibitishwa na kukubaliwa na upande mmoja tu wa mkataba, huo utakuwa ni ulaghai na kututhibitishia kuwa Muungano huu ulikuwa haramu na Batil.
Tunaomba SMZ mututimizie Ombi hilo sio iwe tunabishana bila ya kuwa na ithibati ya kutosha.