Habari

Takuimu ya wananchi wa Zanzibar ,imebaini kuwa Zanzibar kuna kambi nyingi za Jeshi la JWTZ kuliko Tanganyika.

IMG_8622

Takuimu ya wananchi wa Zanzibar imebaini kuwa Zanzibar kuna kambi nyingi za kijishi kuliko Tanganyika na asilimia 99% ya wanajeshi hao ni watanganyika .

Wazanzibar wanajiuliza jee kumiminwa kambi hizo kila kona mijini na mashba kupita kiasi lengo kubwa ni nini?.

Wengi wamekua wakisema hii yote ni muendelezo wa kuikalia kijeshi Zanzibar na kuleta vitisho zidi ya Wazanzibar .

Tumeshuhudia uchaguzi mkuu wa 25 october 2015 pale jeshi la JWTz kuvamia uchaguzi mkuu pale Bwawani kwa silaha za moto na kutapakaa mitani ili kulete hofu na vitisho zidi ya wananchi wa Zanzibar ndani ya ardhi yao walio zaliwa bibi na babu.

Hali hii ya JWTZ haikuishia hapo tu,tumeshuhudia mara kazaa kupita mitani wakiwa na silaha mzito na vifaa vya kijeshi bila kutowa tarifa kwa wananchi wa zanzibar na hali hii inawafanya wananchi wa zanzibar kuishi kwa hofu.

Ukisabu kambi zote za zanzibar ningapi na Tanganyika ni ngapi ?utaona Zanzibar kuna kambi nyingi za kijeshi na wanajeshi Asilimia 99 si wazanzibar.

Share: