TANGAZO MUHIMU: Na Tutoe Michango
Written by administrator // 09/02/2012 // Habari, Matangazo // 16 Comments
Uongozi wa zanzibaryetu kwa kushirikiana na uongozi wa mzalendo.net inawaomba wazanzibari wote ambao watakuwa tayari kutoa misaada yao ajili ya kutoa elimu ya uraia kuhusu mchakato wa katiba tunawakaribisha kutoa michango yao ili kuliwezesha baraza hilo kufikia wazanzibari wote, waliopo Unguja na Pemba, Mijini na Mashamba, michango hiyo ni kwa ajili ya kusaidia gharama mbali mbali za kuwafikia wananchi kama usafiri, vitabu vya elimu juu ya katiba, matangazo kwa vyombo vya habari. nk. Misaada hiyo kwa waliopo nje ya nchi wafikishe misaada yao kwa Jumuiya ya Wzanzibari inayoshughulikia Ustawi wa Jamii UK (ZAWA), na waliopo ndani wafikishe misaada hiyo kwetu ofisi zetu zipo Kikwajuni Welesi.Wasiliana nasi kwa njia ya barua pepe au email yetu hii ni wahamaza@gmail.com na admin@mzalendo.net na namba zetu za simu ni ni+255777477101 na +255777430022 na +447588550153
Na kwa wale wanaotaka kutoa michango yao kwa paypal wanaweza kutumia paypal ya mzalendo tunatanguliza shukrani kwenu nyote. Ukitoa msaada wako ujue umewasaidia wazanzibari wenzako katika kuleta mabadiliko katika nchi yako. Tafadhali tutumie maoni na ushauri wako na kama hujafahamu unaweza kuuliza suali ukiwa unahitaji ufafanuzi tupo tayari kwa hilo na karibuni nyote tunawakaribisha.




16 Comments on "TANGAZO MUHIMU: Na Tutoe Michango"
JEE KWA M PESA MNAPOKEA?
naomba na mi muniarifu ili niweze kutuma
sawa mambo ndio kama hayo nashukuru wana habari kwa kujitolea kuipigania nchi yetu tunaomba account number ziwekwe wazi
Katiba gani hiyo ya tanganyika?
Kiukweli siye waznz uraia hatuna na uraia wetu unajulikana ni utanganyika. Znz kuna warwanda, warundi, wacongo, wakenya, waganda, wamsumbiji na makiristo na wamaya Yani watanganyika wote hawa wanajikana ni waznz uraia WAO na wana haki ya kila kitu znz hata huyo mznZ hatambuliki uraia wake Yani mgeni yeye na hana haki hata kupiga kura
Nashagaa kusema tutoe michango kwa Katiba isiyotubusu.
Kama kuna mchango Wa kuipinga katiba ya tanganyika isiingie znz na kuwafukuza wakiristo
Waznz wana haki kubwa katika kuishi mwambao Wa Afrika mashariki kwani ni kwao. Nyerere na kenyata wameua na kuiba sehem ya znz.
WanA mapinduzi wote hawama uraia hilo jeshi la tanganyika histahili kuwepo znz kati yao kupiga watu tu pamoja na polisi kutoka tanganyika na wakiristo WAO
Yote ni ccm na smz tusichenguane nchi ishauzwa Katiba ya tanganyika
Hatutaki Katiba hatutaki muungano
Elim ndio hii
VYEMA NI KHATUA MUHIMU SANA. LAKINI SIE ZANZIBAR KATIBA YETU TUNAYO.
WAACHE WA TANGANYIKA WAJADILI KATIBA YAO.
SISI WA ZANZIBARI TUPEANA ILIMU YA VIPI KUREJESHA DOLA YETU KWA KUTUMIA BARZA LA WAKILI SHI, TAASISI ZA KIMATAIFA NA KURA YA MAONI ILI KUNGOWA UKOLONI WA TANGANYIKA ZANZIBAR . WSJIDAI KUTAKA KUTUFUNIKA GUNIYA KUTUIBIA NCHI YETU NA KUHALALISHA MUUNGANO HARAMU ( UKOLONI) KWA KUTUMIA SIE WENYEWE. ATI KATIBA YA MUNGANO. …. MKATABA WA UJIRANI MWEMA NA MAMLAKA KAMILI YA DOLA YA ZANZIBAR BAS HAKUNA JENGINE LA KUJADILIANA NAO
ZANZIBARIS AWAKE.
ACHENI VISA NANYI SI TOENI PESA ILI WATU WAELIMISWE NIMEZUNGUMZA NA DADA HUYU NA SIMU YAKE ALIYOIWEKA HAPO ANASEMA YEYE HAJAONA KAZI ILE ALIYO KUWA ANAFANYA
UJERUMANI KAZI YAKE MWENYEWE BINAFSI KAMA HI YAANI WANZANZIBAR WANATAKA
KUELIMISWA NILIIMUAMBIA KATIBA HAIFAI KWA SASA MAAMA KAJA JUU KAMA MOTO ANAYETAKA ASEMA ACHANGIE NA ASOTAKA BASI KASEMA INAMMANA SANA KWETU WATU WATASEMA YALE WANAYOYATAKA MUNATAAKA MUUNGANO BADO AU LAA SISTER HUYO ANASEMA
PEMBA WATU NDIO HASWA WASAIDIWE HIYO MICHANGOYETU UKIANGALIA NIKWELI MI SI MANIISHI KATIBA LAKINI PIA ITASAIIDIA WALE WATU KUELIMIKA AKISEMA MMOJA SI WANASIKIA WANAAKILI BASI ITAAMSHA WALOKOROMA MASALAM
@HAPA PANGU MBONA HUPATIKANI KWA SIMU ILE KAZI KUNA MTU NILIZUNGUMZA NAE
AU USHASETEL
Kwa kweli sisi huwa ni watu wazuri sana kwa kuchangia maandishi, na hasa maandishi yawe ya kumsulubu mtu. Lakini inapokuja michango ambayo aidha itahitaji mtu kutumia wakati wake au mali zake iikiwamo na fedha zake, basi utaona maneno mengi ambayo sio ya kujenga.
Hili la katiba kwa sasa ndilo lililopo, katiba kuchangia kufahamishwa Wazanzibari wenzetu katika hili ndipo kutapatikanika lile ambalo wengi wetu tunalitaka.
Sasa mawazo yangu ni kuwa kama wewe huna basi mshauri mwenzio achangie ili lengo lipate kufikiwa, lakini sio kutoa maoni yaliyo negative.
@ stone town
Mimi michango yangu yote nilikua namtumia Ashakh na anfikisha pale inapotakiwa. Hii nikwasababu Pay Pall yangu ilikua haikubali. Niko na Account ya NatWest srcurity yake ni kiboko hasa ukiwa hukai UK tena.
Lakini Ashakh hayupo hivi sasa, kama nataka kulipa kupitia check nani nimtumie ili aweze ku- Cash it?
Ikiwa nitabahatika kulipa kwa PAY PAL (kwani nitajaribu tena baada yakununua kitu kutumia Ebay UK). Jee nimlipe nani ZAWA au ??????
@ Muna
Pemba hawataki Elimu ya Katiba wala Mkata nduguyangu wee.
Wanaotaka Elimu ya Uraia , Katiba, na kuthamini Utu au Identity yao ni:
Jamaa zangu wa kisiwa cha UNGUJA , hasa Wamakunduchi, Wadonge, Mkwajuni, Dunga Matemwe, Nungwi. Hawa ndio Wanaachia Wabara (hasa Wakristo) Kuvamia Visiwa bila ya Mpango.
Ndio hao wanaowakumbatia (WAKURYA ) hasa wenye Magwanda ya Kijani (kama nzi wa Chooni). Ati wanasema ni Wenzao kwasababu wako katika chama cha CCM, wengine hata sio CCM ni Chadema lakini wakiwaona tu na Magwanda ya Kijani utawaona Wanavotafuna Vidole na Kutetemeka Miguu yao.
Wapemba Hawataki Upuuzi huu wanaghiari wafe Njaa lakini wapate Heshima yao na Wapate pakuzikana.
Jamaa zangu wa Unguja ,ndio hao wanouza Viwanja kwa Wabara hata kama ni watu wa Makanisa basi watu wa Unguja wengi wao hawajali (UTU ) wao. Ukiwatajia (Pesa) tu basi Masikio Yanawaruka kama kwamba Pesa hiyo watatumia Maisha . Mpemba hata umpe Millioni Mia kama hajui asili yako hakuuzii Kiwanja wala hukaribishwi. Wako Wajinga wachache lakini wameanza kusoma kidogo.
Sasa huyo dada anaesema kwamba Wasaidiwe watu wa Pemba kupata Elimu naona anakudanganya. Labda Wapemba uwasaidie pesa Wakanunue “MAKOO ya PWEZA”
Elimu itolewe kwa watu wa Unguja hasa hio mikoa nilioitaja, hawa ndio Wanaotaka Elimu ya Katiba. Kuna (baadhi) ya nduguzangu wa kutoka Unguja wanaishi Ulaya au wana PHd za kila aina lakini bado wanatabia za kiajabu ajabu. Nakukejeli kejeli kila kitu unachowaambia.
Tumemuona Shamuhuna na Seif Iddi alivoipeleka Bahari ya Zanzibar kwa Tanganyika kwakuahidiwa pesa na Vyeo tu. Sasahivi Chadema Wamefurahi matakwa yao yakwamba Zanzibar ni MKOA wa Tanganyika.
@Zamko njia nyepesi ni ile ya kupeleka moja kwa moja, kwa kupitia zilw bureau de Change zilizopo zanzibar.
Kama kawaida naamini wapelekaji kwa huko ulipo wapo, basi kama hamna unaweza kutumia accout ya zawa uk na ref ukishazitia andika katiba.
Ni Imani yangu kuwa Account ya Jumuiya yako uipendayo bado unayo.
kama huna basi nitaiweka hapa. Lakini kama itatumika njia ya Bureau de Change itakuwa bora zaidi, na tuma kwa JIna la Salma said ama Ally Saleh
Kama hiyo haiwezekani basi tumia PAY PAL na ref kama kawaida ni Katiba
@stone town
ahsante mkuu.
Nitatumia hizo BUREAU DE- CHANGE ya pale kwa Abdalla Mrusi. Huku kwetu Ni Shamba hakuna mtu anaepeleka pesa . Na kama wapo basi ni huko Mjini Scandanevia, Nikitaka kutuma visenti vya dagaa huko nyumbani njia ninayotumia ni Iternal Tranfer ambayo hutuma kwa Sahib yangu anaeishi Reading na yeye akazipeleka huko Kijiweni.
kwahivo nitafanya hivyo.
hao wanaopinga ndio wanohitaji kuelimiswa kwanza
hawajui kwamba mpaka leo watu wanafuata mkumbo kuna watu wanamapenzi na ccm,
kwa sababu kaahidiwa kwenda kazi za vikosi unajua znz hakuna ajira.
na sera ya ccm ni kwenda serekali moja
Asalamu Alaykum.
Bi Munna ahsante kama umenipigia simu lakini jee lengo lako lilikuwa unipigie simu halafu uwaeleze watu kuwa umeongea na mimi au lengo lilikuwa ni kutaka ufafanuzi wa suala la elimu ya katiba?
Na kama unavyosema nimeruka kwa ukali jee kulikuwa na haja ya kuandika humu mtandaoni? kwa kuzingatia mazungumzo yetu yalikuwa ni baina yangu mimi na wewe na kama mimi nimekujibu hivyo au nimekuwa mkali kama usemavyo jee ulichozungumza wewe mbona hujakiandika? nadhani heshima na nidhamu lazima iwepo kila pahala umezungumza na mtu kwa njia ya simu basi lazima uheshimu mazungumzo hayo unless mkubaliane kwamba mazungumzo hayo mnaweza kuyatoa hadharani lakini sio sahihi wala sio maadili mema wala sio busara kuongea na mwenzako kwa simu halafu ukaweka hadharani mlichozungumza. Hata hivyo nakushukuru kwa hilo,
kuhusu elimu kwa nini muwasemee watu ambao wanahitaji elimu mkaseme hawahitaji kupewa elimu wakati wao wenyewe ndio wanataka kufahamishwa suala la katiba?
aliyeuliza kuhusu kutuma fedha kwa MPESA namjibu ndio tunatumia kwa njia hiyo pia sisi tunapokea msaada wowote hata mtu akijitolea kuwalisha watu wanaokwenda kutoa elimu au kuwapatia usafiri au kutoa gharama za mafuta ya gari kuwafikisha huko katika bijiji au pia msaada wa kuchapisha hivyo vitabu yote ni misaada na yote tunapokea na namba zetu za simu ndio hizo kwa wale ambao wapo tayari kusaidia. SHUKRAN
Vishindo vyote hivi vya rasimu ya Katiba vimezuka baada ya Katiba ya Zanzibar kujitangaza kuwa ndio Grundnorm – Katiba Mama na Baba ya Zanzibar – na sio Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nia ya rasimu mpya ya Katiba ya Muungano ni kuifanyia Mapinduzi ya kikatiba Katiba ya Zanzibar ili ife, na Jamhuri ya Zanzibar na watu wake watumbukizwe ndani ya kaburi moja la halaiki la kikatiba, ili Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano isimamishwe tena kama ndio Grundnorm. Huo ndio msingi wenyewe.