Habari

Tathmini Ya awali ya Waathirika wa Mvua Zanzibar

Tathmini ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba hadi sasa imeathiri Nyumba 325 Mkoa Kusini Pemba, Nyumba 667 kuhamwa ndani ya Mkoa Mjini Magharibi pamoja na kubomoka kwa miundombinu ya Bara bara na baadhi ya Madaraja hasa Kisiwani Pemba.

Akitoa Taarifa za awali za athari ya mvua zilizojitokeza kwa mwaka wa 2017 tokea kuanza kwa msimu wa Mvua za Masika, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Ali Juma Hamad alisema athari ya Mvua hizo zimesababisha maporomoko ya ardhi yaliyosababisha kufukia kwa baadhi ya Nyumba na Bara bara.

Bw. Ali alisema athari kubwa ya uharibifu wa miundombinu ya Bara bara na nyumba kutokana na mvua hizo hasa katika Mkoa wa Kusini Pemba na kusababisha kifo cha Mtoto Mmoja Ramadhan Mohamed baada ya kuangukiwa na ukuta wa Madrasa Chanjani Chake Chake Pemba.

FB

Share: