Habari

Tathmini yangu, Mwaka mmoja baada ya Uchaguzi wa Zanzibar

Na Mzanzibari Halisi
Ni mwaka mmoja sasa tangu upite uchaguzi Mkuu, kwa upande wetu Zanzibar hali ni tete, maisha yamekuwa magumu kupita maelezo, hii inatokana na kwamba Serikali ambayo ipo madarakani kwa sasa haikubaliki na wananchi wengi wala haipewi mashirikiano, tunathubutu kuiita Serikali haramu ambayo inatawala kwa mabavu si kwa ridhaa ya wananchi.

Hata tujaalie kwamba ipo madarakani kihalali basi kama itakumbukwa katika kampeni za Rais aliepo madarakani Balahau Shein alisema atavigeuza visiwa vya Zanzibar kuwa kama Dubai ya Afrika Mashariki, mwaka umepita hatujaona harakati zozote za kuipeleka Zanzibar Dubai zaidi ya ugumu wa maisha na unyanyasaji wa Raia, tumeshuhudia wafanyaBiashara wamehamishwa katika Jumba la Treni lililopo Darajani Mjini Unguja, katika kipindi cha Ramadhan Kuelekea Sikukuu, kipindi ambacho kinaaminika ni cha Biashara, lakini SMZ kwa makusudi wameamua kuwahamisha wafanyaBiashara hao kwa sababu ni wapinzani kwa makusudi ili kuwatia adabu, na karibuni pia makontena yaliopo Darajani nayo yamevunjwa, kila wanapokaa wafanyaBiashara kujitaftia riziki wanawaondoa.

Uhasama, Chuki baina ya wananchi ndio yanayoikabili Zanzibar kwa sasa, na katika historia ya Wazanzibari tar 28 Octoba haitosahaulika na kuitwa JECHA DAY kwa kitendo chake cha kinyama alichowafanyia Wazanzibari kwa ajili ya kulinda ya Pishi ya mchele na maslahi yake Binafsi, kama alifanya vile kwa haki kwa nini Kibabu Jecha haonekani mitaani, anaishi kwa kulindwa, hana raha ya kuishi na kuchanganyika na jamii yake, maslahi aliyoyapata kwa kufanya utumbo huu yatamtokea puani hapa duniani na huko mbele ya safari, sisi hatumsamehe kwa alichotufanyia na ataendelea kupata laana za viumbe vyote vilivyohai mpaka mwisho wa dunia.

Napenda kuwasilisha

Tagsslider
Share: