TATIZO LA MAFUTA ZNZ AU UDHAIFU WA NAFSI?

Written by  //  26/02/2012  //  Habari  //  5 Comments

Wana-Mzalendo wengi mnaoishi nje ya Zanzibar, mnaweza kuchotwa na habari za magazeti zinazosema kuwa “Zanzibar Imekabiliwa na Tatizo la Mafuta” has petrol. Hii si kweli.

Ttaizo hasa ni udhaifu wetu Wazanzibari, udhaifu wa nafsi – ufisadi na corruption iliyojaa ndani ya serikali na watu wenyewe binafsi.

Mafuta yapo, tena mengi sana. Lakini hayatoki, na watu wa serikali, ikiwemo wizara ya mawasiliano na miundo mbinu (under Hamad Massoud CUF) wamebuni mbinu za kutoa INVOICE. Ukipewa hiyo basi utapewa mafuta shibe yako, hao ndio wale wale bin kinana bin huzaima. Watu wa serikalini kama TRA, ZRB, SMZ officials, CUF-CCM offcials n.k: makabwela hawana haki, wavuvi wanaokwneda kutarazak, kutafuta maisha – hawana haki. Wenye dala dala – ambao pato lao ni daily malipo, hawana haki.

SMZ-GNU imekaa kimya – wao wanafaidi matunda ya matatizo haya waliyoyasabisha wao, na wanazidi kutupiga msumari wa kichwa ilhali sisi tayari ‘maiti’.

Nadhani mmeisoma kauli ya Hamad Massoud juu ya kadhia hii – upuuzi mtupu, urasimu zaidi kuliko utendaji – eti serikali inabuni utaratibu mzuri w akugawa mafuta. Upiiiiiii? Mafuta hayakuwa shida, ila wao akina Hamad Massoud ndio wame-create problem hii ili wajipatie pesa kitita zaidi na zaidi – wananchi wansumbuka sana juu ya kadhia hii.

Tatizo jengine ni TRA na ZRB, wanawabana sana wanaoleta mafuta Zanzibar – sababu: mipango ya uchumi mbaya: Zanzibar imekosa njia na mbinu za kupata vyanzo vya kodi – sasa wanawabana wanaoleta mafuta. Only business inayo-flourish Zanzibar kwa sasa ni hii ya mafuta. Ile ya utalii, mataliana na wengineo investors hawalipi hata umeme na maji seuze kodi. Hii ndio SMZ-GNU rushwa juu ya rushwa, ubinafsi umejaa na roho dhaifu za viongozi.

Sababu ya 3: wanaoleta mafuta pia roho zao mbaya, wanatoa mafuta, kinamna ili kuwasumbua watu, wanawapa wanaowataka na wanataka faida kupindukia, ingawa sababu hii inatokana na sababu 2 – madhila ya TRA na ZRB.

Sababu ya 4: EWURA – hii ni taasisi ya kuratibu mambo ya nishati – taasisi ya Tanganyika, imeundwa kitapeli tapeli tu, na haina mandate hapa Zanzibar. WAO WANADAI KUWA MAFUTA YOTE YANAYOINGIA ZANZIBAR, LAZIMA YAPITIE BARA. MPO HAPO. Sasa BLW letu la wawakilishi nalo limejaa ujinga na upuuzi kwa sababu EWURA haijathibitishwa na BLW, vipi leo wawe na amri ya kutuamulia mambo ya maslahi ya kiuchumi ya hapa Zanzibar. Htautaki na hatujataka kuamka – bado tumelala na tumeganda na vitanda, salaaaaaaaa…….! amkenei jamani.

BLW ni pahala pa kwenda kupiga soga na kuchekesha watu – kijiweni tu, wale members wa BLW sijui niwaite nani, mambo kama haya ilikuwa wayashughulikie mara moja ni UAMUZI tu, sio kuunda kamati wala vikao vya kuondoa kero za muungano.

Jamani eee..Zanzibar tunaumizwa kila upande – tumepigwa nyundo moja safi sana ya kichwa na NECTA – watoto wetu wamefelishwa. Tumekaa kimya. Bahariu yetu inachukuliwa, tumekaa kimya – ila BLW wanazungumza UROJO na utumbo wao – sherehe tu. EWURA wanatoa fatwa juu ya uletaji mafuta Zanzibar – tumekaa kimya. Pesa zetu zinachukuliwa na BoT -then wansema kuwa Zanzibar sio sharehokder wa BoT – tumekaa kimya. Zanzibar haina hata mkurugenzi mmoja katika idara za BoT (benki kuu) ulizeni mtayapata zaidi, WHY. Nasikia juzi juzi ameteuliwa mmoja kama kuficha uchafu. Almuradi jjamani uonevu umekuwa mkubwa sana kupita kiasi. Mambo yetu ya nadni usiseme – imezama M.V Spice — kimya kama amekufa paka tu, wauwaji tunakula nao chips akina Jaku, Tantalun na mtoto wa kindaki ndaki Hasnu Makame na wengine wengi – kesi haisikilizwi tena – kilichobaki ni kuzungumza na majaji tu, wanapewa chao – finito! udhaifu wa roho na nafsi.

Leo Bara wanatuamuliw ampaka lita ngapi tutie ndani ya gari yako/yangu au gari ya Donge, Bumbwini, Wete-Chake, Mkoani-Chake nk. Tumefikia hapo. Bado nini tena?

Mimi nafikiri kuwa kama kweli BLW wana dhati ya nafsi na nia njema kwa Zanzibar, basi wapitishe miswada pale BLW – ya kutuamulia hatma yetu. Ila mimi siwaamini hata chembe wawakilishi wetu — awe wa CUF au CCM — wote sawa tu. Hawana mpya na ndio wanaotumaliza, bara wanachimba kaburi, wao wanachimba mwana wa ndani, na wale akina Samia, Mahadhi, Dr.Bilali, Pereira, Mohammed Seif Khatib, Mohammed Aboud — wao na wengine wanatuvisha sanda na kututia karafuu maiti na dalia na mafuta mazuri n.k.

Napenda sana kuuliza swlai hili kwenu kila mara: tufikwe na nini Zanzibar mpaka tujue kama tumefikwa na mtihani, au tuzinduke? yaliyotufika si madogo – leo bado tumelala tu.

Wallah nikuchekesheni kidogo – ile picha ya dr.bilali aliyppewa uchifu imekuwa kama wale ‘wachawi’ au ‘halloween’ au tuseme kama zile picha za wa le ZOMBIE’ na yeye kwa ujinga wake ‘anachekaaa’ anaona amefaidi. Eti huyu ni mtaalam wa ‘nuclear science’. Wacha aende mwezini na nguo zake za kaniki!!

5 Comments on "TATIZO LA MAFUTA ZNZ AU UDHAIFU WA NAFSI?"

  1. abdulmajid 26/02/2012 kwa 8:24 mu ·

    kwani kuna makampuni mangapi ya kuleta mafuta hata ifikie hali hii liter 6000 dah hatarii

  2. rivaldo 26/02/2012 kwa 10:56 mu ·

    ni masikitiko makubwa sana haya hapo zamani tukiongoza kwa kuletwa mafuta leo tipo nyuma kuliko mkia ila MATATIZO YETU WENYEWE na hii serikali yetu inayo uumiza wananchi maana haiwi wao hawapandi dalala WANA BILL YAO SHELI HAWAONI USUMBUFU WA NAMNA HIO TUNAOMIA NI WATU WA HALI YA CHINI MAANA BILA YA KUTO NGUVU ZETU HATULI WAO HATA HABARI HAWANA EWURA HAO TRA GOTI NGUMU ZRB WOTE NI WAZEMBE ITAFIKA HATA CHETI CHA NDOA ITOKE MAHAKAMA KUU BARAAAAA AU HATA KUMUINGILIA MKEO AMRI ITOKE HUKO HUKO……KAMA SERIKALI YA SOMALI KUWA IPO KENYA LAKINI INAONGOZA SOMALI NA HII YETU IPO DAR

    UKIULIZA UNAMBIWA MUUNGANO UDUMISHWE NA UENZIWE KUNA MATUNDA MENGI JUU YA MUUNGANO NI SAWA NA LIMAO CHUNGU ILA LINASIDIA KTK KUCHAPUSHA MCHUZI…..hii ndio serikali yetu bila VITA HAPA HATUNAAA KITU.

  3. kalasinga 26/02/2012 kwa 11:25 mu ·

    ndugu abdi sikuwa msomaji wa makala zako hapo nyuma na hii ni kutokana huwa hufahamiki fahamiki. ila kila siku zinavosonga naanza kuona your true color , kwa kweli wewe ni mpiganaji na huchoki nakufananisha na clay tukija mambo ya ulingoni . siamini kama hiyo bei imefika 6000 ltr.. kama kuna mtu anafuga tamaa kuwa hali ya nchi hii itabadilika amsubiri yessu teh teh teh..ONE

  4. ulogba 26/02/2012 kwa 11:49 mu ·

    Tatizo la mafuta znz linatokana na mfumo mpya wa uingizaji mafuta kutoka nje ulioanzishwa na SMT.
    Hivisasa tanzania nzima ni kampuni moja tu (ya uswis kama sikosei/kutoka ulaya) ndio inayoleta mafuta kisha kuyauzia makampuni yote ya hapa kwa pamoja na bei maalum bandari ya Dar. Katika kupakua,kampuni inayonunua mafuta mengi ndio inayoyapata mwanzo, kwa kampuni zanzibar kiasi cha mafuta ni kidogo wanayonunua,hivyo hua wa mwisho kuyapata.

    Muhimu ni kwa SMZ kukaa na SMT kuangalia tena utaratibu huo ili makampuni ya zanzibar yapewe mwanzo kwa kua kidogo then process iendelee.
    Na kwa upande wa vituo ni kua taasisi,makampuni,vigogo wana mikataba tayari ya kupatiwa mafuta,ndio maana walala hoi wanaambulia patupu na wakipata ni kwa ulanguzi sh.3000 hadi 6000/lita.

    • abdulmajid 26/02/2012 kwa 3:19 um ·

      basi kazi apo apo haya twende fikisha liter elfu kumi wabanie kila kitu tia shemere wazanzibar ifike cheti cha kuzaliwa na ndowa waje kuchukuwa na kuchapishwa bandari salamaa

Comments are now closed for this article.