Baraza la Biashara ZNZ Kujadili Soko la Pamoja

Written by  //  17/05/2010  //  Uchumi  //  2 Comments

Mh.Karume sherehe za Mapinduzi miaka 46
Na Salma Said,

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume leo anatarajiwa kufungua mkutano wa baraza la biashara la Zanzibar utakaoangalia jinsi gani Zanzibar itashiriki kwenye soko la pamoja la Afrika ya Mashariki.

Lengo la mkutano huo ni kuwaelimisha wafanyabiashara wa Zanzibar juu ya umuhimu wa kulitumia soko la pamoja na kuyapatia ufumbuzi matatizo yao watakayokabiliana nayo katika soko hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Zanzibar Katibu mtendaji wa Jumuiya hiyo Ali Haji Vuai, alisema mkutano huo utatoa fursa ya wafanyabiashara wa Zanzibar kuzungumzia kero na changamoto zao zinazowakabili.

Alisema karibuni wafanyabiashara wa Zanzibar wataingia katika soko la pamoja ambalo limeshasainiwa na utekelezaji wake utaanza hivi karibuni ambayo Zanzibar ni nchi pekee yenye visiwa itakayoingia katika shirikisho hilo.

Vuai alisema hivi sasa kilichopo ni kutoa elimu na kufanya matayarisho ya kuelimishana ili Serikali na wafanyabiashara waweze kujipanga vizuri katika kukabilina na soko hilo.
Vuai alisema katika kuwatayarisha wafanyabiashara wa Zanzibar kuingia katika soko la pamoja la jumuiya ya Afrika mashariki baraza la biashara itaendesha mkutano utakaowajumuisha zaidi ya wajumbe 300 kutoka ndani na nje ya Zanzibar ukiongozwa na mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume.

Katibu mtendaji alisema kuundwa kwa baraza la biashara Zanzibar kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuopunguza kero za wafanyabiashara ambazo zilikuwa zikiwakabili kila siku katika kazi zao.

Akitaja matatizo yaliotatulwia na baraza la biashara ambalo ni mwaka mmoja tokea liundwe ni jumla ya matatizo yapatayo 60 yanayowakwamisha wafanyabiashara wa Zanzibar yamepatiwa ufumbuzi.

Alisema baadhi ya matatizo yaliokwua hayajapatiwa ufumbuzi hayapo moja kwa moja katika mamlaka ya Zanzibar hivyo lazima pande mbili ya muuungano zikae na kuona namna gain ya kuweza kutatua ikiwemo suala la kutozwa kodi mara mbili katika bandari ya Tanzania.

Hata hivyo alisema suala hilo halimo mikononi mwa Zanzibar peke yake ndio maana likashindikana kutatuliwa lakini kupitia vikao vya kero za Muungano suala hilo limeshawasilishwa na linaendelea kuzungumzwa na mawaziri wa pande mbili za Muungano chini ya Mwenyekiti wake Makamo wa rais wa Tanzania.

Akitoa maelezo yake katika mkuutano huo, Mkurugenzi wa wizara ya biashara Zanzibar, Rashid Ali Salim alisema mkutano huo utaangalia ueleweshaji wa soko la pamoja la ndani ya Afrika Mashariki baada ya kumalizika hatua ya umoja wa forodha. ambao utekelezaji wake kamili ulianza Januari mwaka 2010.

Alisema hatua inayofuata kwa mujibu wa mkataba wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ni kuingia katika soko la pamoja iliyotiwa saini Novemba mwaka jana inatarajia kuanza mwezi Julai mwaka huu yenye lengo la kuelimisha dhana ya soko la pamoja nchini

Salim alisema suala la misamaha katika soko hilo, misamaha ya bidhaa haitaombewa kwa mtu mmoja mmoja bali itaombewa kwa wafanyabiashara wote watakaoingiza bidhaa zinazoombewa msamaha.

2 Comments on "Baraza la Biashara ZNZ Kujadili Soko la Pamoja"

  1. ole 18/05/2010 kwa 12:33 mu ·

    Haya tu tena, tuburuzwe

  2. Mznz 18/05/2010 kwa 8:23 mu ·

    Wazanzibari akili zetu hazina akili, WENGI WETU MADUNYAAA.Hivi nchi hii ilivobarikiwa neema za kila aina ndio wa kuwa hivi sisi?? ATI WABARA NDUGU ZETU, NDUGU ZETUUUU KAENI TU HIVO HIVO hapa tulipofikishwa ati bado pia kuna watu hawajashtukaa! hasa hasa ndugu zetu wa kusini na baadhi ya sehemu kaskazini huna vya kuwaambia mpka sherehe za pasaka wanashiriki na kuzifurahia,HASARA!!!

Comments are now closed for this article.