Kamati ya Sheria haijaridhishwa na CAG

Written by  //  25/06/2010  //  Uchumi  //  Zima maoni

na Mauwa Mohammed, Zanzibar

MWENYEKITI wa kamati ya Katiba Sheria na Utawala Bora, Haji Mkema Haji, amesema kamati yake haikuridhishwa na kiwango cha mapato kilichokusanywa na ofisi ya Mdhibiti Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG) katika mwaka 2009/2010.

Hayo alielezwa katika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi wakati akiwasilisha hotuba ya Kamati ya Katiba na Sheria juu ya mapato na matumizi ya mwaka 2010/2011.

Mkema alifahamisha kuwa ofisi hiyo ilikadiriwa kukusanya sh 4,000,000, hadi kufikia Machi 2010 ambapo ilikusanya sh 2,500,000 kutokana na makusanyo hayo kuwa madogo, kamati ya katiba sheria na utawala bora imeiomba ofisi hiyo kuyachukulia hatua mashirika yote ambayo hayakutoa ada za uchunguzi wa hesabu.

Hatua hiyo imekuja baada ya kugundua kuwa mashirika haya hayalipi ada hizo sio kama hayana uwezo wa kufanya hivyo bali yanafanya hivyo kwa kuonyesha dharau mbele ya Serikali.

“Mheshimiwa Spika kama yapo mashirika ambayo hayana uwezo wa kulipia ada hiyo kamati yetu inashauri mashirika hayo yafutiwe usajili kwani ni vyema kuwa na mashirika kidogo ambayo yanaleta tija kuliko kuwa na utitiri wa mashirika ambayo hayana faida yeyote,” alisema Mkema
Naye kwa upande wake Waziiri Kivuli wa Wizara ya Nchi ofisi ya rais Katiba na utawala Bora, Haji Faki Shaali, alisema ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar ina malalamiko ya mishara duni, hali inayosababisha wanasheria wengi kuhama na kutafuta maslahi upande mwingine.

Shaali alisema ofisi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kuhamwa na wanaheria wazoefu kutokana na kutozingatia kiwango katika upandishwaji wa vyeo.

Katika hotuba hiyo, Waziri huyo kivuli aligusia mamlaka ya kupambana na rushwa na kuliomba Baraza la Wawakilishi kutoidhinisha sh milioni 13,000.41 ambazo zinaombwa kwa ajili ya mamlaka ya kupambana na rushwa na kusimamia maadili ya viongozi kwa vile hapana tena azma ya kuundwa mamlaka hiyo.

tzdaima

Comments are closed.