People’s Bank of Zanzibar Limited to open its first branch i

Written by  //  23/07/2010  //  Uchumi  //  4 Comments

Hellen Nachilongo
The People’s Bank of Zanzibar (PBZ) is expected to open its first branch in Dar es Salaam as part of a countrywide expansion strategy.

The PBZ marketing manager Mr Rajabu Zuberi said in an interview in Dar es Salaam on Wednesday that the branch would be opened before the end of this year.

“Our strategy is to extend our services in Tanzania Mainland and to enable low income citizens to access financial services,” he told The Citizen at the ongoing entrepreneur’s exhibition in the city.

He said the minimum deposits required to open a bank account would be Sh10, 000.

Mr Zuberi said that so far the bank has financed a total of 1,500 people, including entrepreneurs and individuals to assist them run and enhance their businesses and reduce poverty in Zanzibar.

He noted that they offer loans to people who are willing to open their accounts at the PBZ, calling citizens in the Mainland to exploit this opportunity.

Currently, the institute has a total of Sh60.6 billion customer deposits, making it the biggest bank in Zanzibar.

The bank was established in 1966 as a central business bank of Zanzibar. It has three branches, two in Unguja and one in Pemba

4 Comments on "People’s Bank of Zanzibar Limited to open its first branch i"

  1. Royal Zenj 24/07/2010 kwa 2:41 mu ·

    Muda wote huo toka 1966 hamkuwahi kufungua hata kiji tawi kimoja hapo Tanganyika mlikua mnasubiri nini wajinga na wapuuzi wakubwa , wenzenu NBC wapo Zanzibar mudagani sasa au ndio mlikua mukiendesha kama inavyosomeka hiyo Bank yetu ( bank ya watu wa Zanzibar tu biashara haina hivyo .

  2. Salmin Kiluwa 24/07/2010 kwa 5:38 um ·

    Si mazuri hayo Royal Zenj. Huu si wakati wa kutukanana. Hayo ndio yaliyotufikisha tukawa na tawi moja kwa kudharauliana. Towa mawazo ya kuendeleza si kukosoa bila ya jawabu. Mimi nawapongeza PBZ na nahisi huu ni mwanzo na natumai PBZ itakuwa kwani sasa kuna wazanzibari all over the world na kama PBZ itakuwa na master plan ya kuexpand tutafurahi kutumia benk yetu yukiwa Hong Kong London Dubai kufanya biashara badala ya kubeba mapesa kwa mikoba. Haya ni mawazo kwa PBZ. Wazanzibari wananufaisha benki nyengine na itakuwa vizuri tukinufaisha vya kwetu
    Kiluwa

  3. Royal Zenj 25/07/2010 kwa 12:08 mu ·

    A/ Aleykum Salmin Kilua naomba radhi kwa hilo unajua nilipatwa na munkari kidogo , lakini jambo kama hili la kufungua tawi Dar nataka unikubalie tumechelewa sana sana mambo kama haya ndio yaliotupeleka tukafika kunyan’ganywa nchi na Tanganyika .WAZANZIBARI WANANUFAISHA BANK NYEGINE nimekukoti ndio maana nikasema tumechelewa sana kwamuda usiopungua miaka 40 PBZ na Wazanzibari tumepoteza FORTUNE zake hii sio nzuri .

    M/Mungu ibariki Zanzibar na watu wake .

  4. Heart 26/07/2010 kwa 5:58 um ·

    Nimeshawishika kuchangia kidogo mada hii. kwanza ni vizuri kuelewa kwamba katika kujinasua na kujiendeleza ama siasa ndio zilizaa mipango hii. PBZ iliwahi kufungua matawi mengi Zanzibar. Kwa mfano ukiachia yaliobakia hivi sasa ya Kwerekwe na Malindi Ungunja na Chake Chake Pemba.

    Kuliwahi kufunguliwa Matawi mengine ya Makunduchi, Chwaka ambayo sasa ni chuo cha Uongozi wa Fedha na Kivunge kisiwani Unguja. Pia kulikuwa na tawi la wete na mkoani Kisiwani Pemba. Haya yote yalikuwapo Zanzibar. Lakini pia Kuliwahi kufunguliwa Tawi moja kule Tanga mjini hata hivyo hili halikuweza kufanya kazi licha ya gharama kubwa za mtaji zilizotumika.

    Kwa kweli mpango wa kufungua tawi Dar sio mpya kwani kuliwahi kuwa na mipango hii hapo nyuma lakini PBZ haikuweza kutimiza azma yake kikamilifu kutokana na kubanwa na sheria na sera za Reserve Bank kwa wakati huo ama mipango ya siasa tu ya hapo juu.

    Kwa mtazamo wangu mimi nawaomba PBZ wakaze buti kwani muda upo na hawajachelewa ila mipango na sera nzuri ndio zitakazo wasimamisha na kuwaweka juu katika hali hii ya ushindani mkubwa usiokwepeka.

    Hata hivyo Benk kadha zimeanzishwa Zanzibar katika kipindi hiki kifupi tu na zimeanza kupiga hatua mbele na nyengine kuwa na misukosuko ya hapa na pale.

    lakini linapokuja suala la kusema “Currently, the institute has a total of Sh60.6 billion customer deposits, making it the biggest bank in Zanzibar”. Isiwe ndio kujipweteka kwani Assumption sio myopia nzuri hata kidogo katika biashara makini. Rivals wanaweza kukuangusha once wakijua udhaifu wako kama chura anavyomuelewa ndovu ama tembo na kumuweka chali.

    Kwa mfano kule UK kulikuwa na kampuni ya kuzalisha pikipiki za Trumphs, hizi Trumphs hapa Zanzbari zilikuwa maarufu kwa wale wazee wa miaka ya zamani, na kule USA ipo ya Harley-Davidson. Hizi kampuni zilijipweteka na imani yao na sifa zao za ubora na wingi wa umaarufu kwa bidha zao wakajisahau na kudharau kampuni ya Kijapani ya Honda ambayo ilikuwa ndio kwanza inaingia kwenye biashara duniani.

    Matokeo yake Trumph ilikufa na haipo tena duniani na Harley-Davidson inasuasua na kuiacha Honda kutamba duniani hadi leo bidha zao ndio numbari moja.

    Hivyo kwa mtazamo wangu huu na mfano huu sio vyema kujinasibu wakati washindani wameanza kukamata kamba yako kidogodogo. Kwa hatua muhimu harakisheni huduma zenu ziwe za kiushindani zaidi na ziwe za kupigiwa mfano zanzibar na popote pale mtakapo fungua matawi yenu. Hivyo basi boresheni huduma kwanza kabla hamjakimbiwa na hicho mnachojinasibu nacho kinanyemelewa na Rivals.

    Sisi wazanzibari tunapenda vyetu kwanza.

Comments are now closed for this article.