Matangazo
Written by Stonetown (Kiongozi) // 04/07/2010 // Ujumbe maalum // 2 Comments
Assalamu alaykum,
Ili kuweza kuindesha mtandao huu kwa ufanisi zaidi, tunawaomba wale wote wanaotaka kuweka matangazo yao ya biashara kutumia kurasa maalum zilizowekwa kwa shughuli hiyo, vyenginevyo zitaondolewa.
Vile vile ili kuwezesha mtandao huu kuingiza mapato madogo ya kuindesha tunawataka watu walipie huduma hizi kwa ghrama ndogo tu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Admin





2 Comments on "Matangazo"
Mie mtazamo wangu matangazo yalio kwenye mfumo wa machapisho yaendelee kuwa ni bure tuu.Hii nadhani Taymia mara ya mwisho alielezea vizuri.Kuna sababu za msingi za kuacha matangazo yalio kwenye machapisho kuwa bila ya malipo.
1.Kuchapisha imeachwa kuwa ni uhuru wa mtumiaji, hivyo kuanza kumlipisha ni sawa na kuingilia uhuru huo.
2.Matangazo madogo madogo ni njia moja ya kuvutia wasomaji (unless waombe au watoe maoni kuwa uhuru huo wa kuchapa matangazo uondoshwe).
Kwa maoni yangu ni bora tukastick na maoni haya tuliyonayo kuwa matangazo ya special locations e.g headers,sidebars, slideshows ndio yasiwe bure.Haya yanakuwa ni matangazo ya kudumu na hayamo kwenye uhuru wa mtumiaji ni lazima uongozi ushiri kuyaweka.
Hivyo hapo hio statement ya “kuondolewa” naona itahijika kujadiliwa.
Nawasilisha…
mrfroasty
Waalekum salaam Mrfrosty,
Kwa ufupi uondolewaji niliokusudiwa mimi ni ule kupelekwa kwenye kiungo chake maalum cha matangazo. sio kuondolewa kabisa kabisa, na hata hayo mengine yaliokuwa ni ya bure kwa maoni yangu ni vyema yakawa kule kule kwenye matangazo.
Shukran