MZALENDO.NET kufikisha mwaka mmoja

Written by  //  14/06/2010  //  Ujumbe maalum  //  10 Comments

1.0 Historia fupi

Mnamo muda kama huu katikati ya mwezi wa June 2009, mawazo ya kuanzishwa kwa jukwaa maalum kwa ajili ya habari za Zanzibar yalianzishwa.MZALENDO.NET kama mtandao mwengine wowote, ulikuwa na changamoto za hapa na pale tulianza kurusha matangazo kutoka kwenye nyumba ya mjumbe mmoja wa MZALENDO.Hatimae baada ya miezi 6 mtandao ukaanza kurusha matangazo katika computer maalum kwa ajili ya urushaji website.

1.2 Gharama za uendeshaji

Hadi sasa tunarusha matangazo kutoka US, kwa gharama za wastani wa 100-150$ kwa mwaka.Kwa mwaka wa 2010-2011 gharama zimelipiwa, hivyo mwishoni mwa mwaka 2010 fikra za kulipia mwaka 2011-2012 zitaanza.Vyanzao vikuu vya ufadhili wa gharama hizo:

  • Maktaba yetu ya video
  • Michango wa wadau na wazalendo mbali mbali
  • Wafadhili kwa njia ya matangazo

1.3 Malengo ya mtandao

Kama wengi walivyotarajia, MZALENDO.NET ni jukwaa maalum kwa ajili ya khatma na mustakbal wa taifa la Zanzibar na watu wake.Hivyo lengo letu kuu ni kupashana habari zinazohusiana na taifa la Zanzibar, kuanzia harakati za kukomboa taifa hilo kutoka kinywani mwa Tanganyika, mila na desturi za mzanzibari hadi michezo na burudani kutoka Zanzibar.Kwa mtazamo huu MZALENDO.NET inalenga kuwa ni jukwaa maalum kwa ajili ya habari zote zinazohusiana na Zanzibar, zikirepotiwa na wananchi na wazalendo mbali mbali.Mbali na kupashana habari kutoka Zanzibar, pia tumelenga kuwapatia jukuwaa wazanzibari kwa ajili ya kutoa maoni yao kuhusiana na habari hizo.

1.4 Mafanikio

Moja ya malengo ya mtandao ni kupata jukwaa linaloendeshwa na wazanzibari wenyewe wakiandika habari zao wenyewe.Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio tuliyoyapata katika kipindi cha mwaka mmoja:

i)Google Rank:Tumefanikiwa kuwa highly ranked kwenye suala zima la habari na siasa za Zanzibar.Sasa hivi imekuwa rahisi mtu kufika kwenye mtandao wetu akitafuta habari za Zanzibar.Vile vile tumeweza kuchukua nafasi ya mwanzo kwa mtu alietafuta neno “mzalendo”.Nafasi hii ilichukuliwa na website ya Kenya, ambayo sasa hivi wanachukua nafasi ya 2.

ii)Ongezeko la watembeleaji:Tumefanikiwa kuongeza watembeleaji kutoka 0 hadi 1200-1500 kwa siku.

iii)Ushirikiano na waandishi pamoja na wazalendo mbali mbali:Ni wazi tulilenga kuwapata waandishi mahiri wa kizanzibari, na tunashukuru kwa ushirikiano walio onesha katika kufanikisha project hii na kutoa elimu kwa jamii.

1.5 Matokeo ya “Golden Member Award -GMA”

Tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa wote waliochangia kwa njia moja au nyengine kufanikisha GMA kwa mwaka 2009/2010.Kura imefungwa rasmi, na MZALENDO.NET inatoa pongezi kwa wajumbe hao kwa uzalendo walioonesha pamoja na ushirikiano wao katika sector ya uandishi na elimu kwa jamii.(B.Ole tunakuomba ututumie anwani ya kutuma zawadi hiyo, email utakayo tuandikia ni lazima iwe sawa na ile uliojiandikishia uanachama hapa MZALENDO), washindi Ally Saleh na Salma Said uongozi utawasiliana nayi kwa barua-e kupata anwani ya kutuma zawadi hio.

Mpigie kura mshindi wa golden member award 2009/2010

  • Ally Saleh (60%, 130 Votes)
  • Salma Said (28%, 60 Votes)
  • B.Ole (12%, 28 Votes)

Total Voters: 216

Loading ... Loading ...

1.6 Uboreshaji

i)Video,mp3 na picha za matukio:Ni wazi uongozi takriban wote wa MZALENDO haupo Zanzibar.Kwa kweli hivi ni moja ya nguzo kuu za utoaji habari wa matukio muhimu ya Zanzibar.tungelipenda kuboresha ushirikiano tuliopata kutoka kwa wazanzibari walioko Zanzibar.Hadi sasa hatuna wazalendo waliojidhatiti na kujipanga vizuri katika suala zima la kusafirisha mafaili kutoka visiwani Zanzibar.

Video nyingi tulizozipokea zilikuwa ni kutoka kwa wadau mbali mbali wa ZAWA kutoka UK na mwisho ni video nyingi kutoka kwa MUWAZA.Lakini hadi sasa hatuna mtu ambae yuko visiwani Zanzibar anaetupatia mafaili kwa ufanisi.Hii manaake video nyingi zinatufika muda mrefu baada ya tukio, usije shangaa kuona MZALENDO.NET inachapa video ya tukio la miaka kadhaa iliopita!

Kwa suala la mp3 nyingi tumepokea kutoka kwa Shk Ally, Bi Salma na baadhi ya mp3 kutoka ZAWA, tunatoa shukurani za dhati kwa ushirikiano wenu…really appreciated.

ii)Uongozi na utendaji: Uongozi hadi sasa una wajumbe 4 Ashakh, Taymia, Stonetown na Mrfroasty.Tungelipenda kuboresha katika sector ya uongozi na uendeshaji hususan katika suala la uhakiki kwa vile tumejikita katika kuwapa wazalendo jukwaa la uandishi, hii manaake makosa ya hapa na pale yanakuwepo na uongozi unahitajika kurekebisha kwa ajili ya watumiaji wengine.Bado tunatafuta vijana wa kusaidia uendeshaji, kama utapendelea kushiriki na unahisi unaweza saidia tafadhali wasiliana na uongozi kwa admin@mzalendo.net au toa maoni yako kwenye chapisho hili.

Mwisho

Shukurani za dhati kwa wote walioshiriki na kuunga mkono harakati hizi za kizalendo…Inshallah Zanzibar itakuwa huru na kushiriki Umoja wa mataifa kama ilivyokuwa awali, Amen!

Wako,

Uongozi wa MZALENDO.net


10 Comments on "MZALENDO.NET kufikisha mwaka mmoja"

  1. mrfroasty 14/06/2010 kwa 11:18 um ·

    Moja kati ya mafanikio ambayo hayamo kwenye nyaraka hiyo ni project yetu ya fotocopi, ambayo kwa msaada wa Shk Hassan na Shk Ally tumefanikisha kusambaza kopi kwa wazanzibari wasio na huduma ya Internet.

    Tunatarajia kutoa kopi kwa makala nyengine zenye kutoa elimu kwa jamii.Binafsi yangu napendelea next project iwe ni makala ya Babu Duni kuhusiana na muungano.Hii makala kwa kweli ni muhimu na inatoa elimu kubwa kwa jamii.Lakini mjadala huo uko wazi hususan ukizingatia sasa hivi kuna mchakato mzima wa Afrika Kusini na kombe la dunia….

    Hivyo ni kheri kuacha hadi kombe la dunia limazike, tuanze kujadili next fotocopi project na kujiandaa na kura yetu ya maoni.

    Maoni, critics (both negative/positive) yanakaribishwa kwa ajili ya uboreshaji.

    Maasalaam,
    mrfroasty

  2. Administrator 15/06/2010 kwa 12:37 mu ·

    Kura ya GMA imefungwa rasmi, hivyo uongozi unapenda kuwapongeza washindi hao.Tutafanya mawasiliano, kama ijulikanavyo kuwa kuna wajumbe wengine hawakuona umuhimu wa kutumia email za ukweli.Hivyo uongozi utafanya mawasiliano na washindi hao, email ikibounce tutafanya update hapa.

    Shukurani,

  3. mkarafuu 15/06/2010 kwa 2:20 mu ·

    HONGERA MZALENDO.NET KWA KUFIKISHA MWAKA MMOJA.

    Napenda kutumia nafasi hii leo kupeleka zaidi shukrani zangu kwa muanzilishi wa mtandao huu (Mrfroasty),lakini pia sitowasahau viongozi wake wasasa,pamoja na watumiaji wa mtandao huu iwe ni wanachama au wasomi tu wa habari za mtandao huu.

    Kwani niaminivyo mimi ni ushirikiano ya hao hapo juu ndio ulotufikisha hapa leo,na bila ya hao yani viongozi wanachama na wasomi wa habari za ndani ya mtandao ndio wanao toa changamoto kubwa na upanuzi wa mawazo yetu,pale tunapo soma habari zao au maoni yao baada ya habari husika ndio kina sisi huzinduka.

    Nataka nikiri kua mimi binafsi nimepata muamko mkubwa kabisa na elimu kubwa inayo husu mambo ya Zanzibar special historia ya kweli ya zanzibar na matukio yazamani ambayo sikutegemea kama ningeyajuapo wala sikufikiria hata kuyapekua.

    Lakini nashukuru kuepo mtandao huu na naziheshimu harakati zake kwani ni fahari ilioje leo kua wazeji tuna pahala ambapo tunaweza kupata habari zituhusuzo lakini buwa zaidi tunaweza kutoa naoni kwa vile tunavyo fikiria bila ya shida yoyote kwa urahisi na salama kabisa.

    Pamoja na yote hayo kitu kilicho nipendeza ndani ya mtandao ni kutumia lugha ya Kiswahili kwa wastan wa asilimia 99%,hii nikuonyesha kua mtandao huu kweli ni wakizanzibari kwani hadi sasa Zanzibar ni nchi pekee (duniani) ambayo watu wake hawana lugha nyengine ya ukoo wala kabila bali ni Kiswahili tu,mwazo mwisho.

    Kwa maana nyengine Wazanzibari ndio waanzilishi wa Kiwahili na Mzalendo.net inaheshimu na kuendeleza Lugha hio,ambayo ni moja ya alama ya Taifa la Zanzibar.

    Imani yangu mtandao huu utaendelea na malengo yake na hautarudi nyuma kwani malengo ya mtandao huu ndio malengo ya wazanzibari walio wengi kama sio wote.

    Nachukua nafasi hii kuahidi mtandao huu kua tutakua pamoja kuhakikisha kua tunasonga mbele kufikia malengo tuyatakayo.

    EWE MWE/MUUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA UWABARIKIE WATU WAKE.(amin)
    EWE MWE/MUUNGU INUSURU ZANZIBAR NA URUDISHIE HESHIMA YAKE.(amin)
    EWE MWE/MUUNGU ILINDE ZANZIBAR NA UANGAMIZE MAADUI WAKE.(amin)
    EWE MWE/MUUNGU ITIZAME ZANZIBAR NA UPEPERUSHE FITINA ZAKE.(amin)

    Maasalam.

  4. Junius 15/06/2010 kwa 3:33 mu ·

    Kwanza nawapongeza wazalendo kwa wazo la mtandao huu ambao ninauotea mengi ya mafanikio huko mbeleni, pili nawapongeza kwa kutimiza mwaka mmoja ambao ni isabu ya miaka mingi itakayokuja kwa mtandao huu.
    Mimi binafsi yangu kama Mzanzibar, mzaliwa na kulelewa, najitolea kwa msaada wowote wa kihali na mali kadiri Mungu atakavyonijaalia kwa mtandao huu. Hivi sasa nipo masomoni nje ya nchi, lakini inshaallahu taala,nategemea kumaliza mwezi wa tisa mwaka huu, na kabla ya uchaguzi nitakuwa Zanzibar kwa uwezo wa Allah.
    Nitakuwa tayari kushiriki kwa kujitolea katika eneo lolote litakaloonekana linafaa kutoa mchango wangu nikiwa visiwani. Uongozi tunaweza kuwasiliana kwa e mail niliyojisajili humu.
    Wabillahi tawfiq
    J

  5. ashakh 15/06/2010 kwa 9:27 mu ·

    Mwanzo wa hesabu ni moja. Kutimiza mwaka mmoja kwa mzalendo ni kitu cha kujivunia. Shukran zote ziwafikie wadau (Wazalendo) walio uimarisha mtandao huu. Kuanzia na mwanzilishi mrfroasty, timu yake na wasomaji. Tunafahamu iko mitandano mingi imeanzishwa, lakini kwa kukosa nyenzo muhimu hizi haikupata haiba kama huu.

    Ipo haja kwa wazalendo kuangaza mbele (focus) mwaka unaofuata. Kwani ni kipindi muhimu kwa nchi yetu kwa vile tunatayariji kipindi cha mpito katika uongozi wa nchi yetu. Tutumie mwaka uliopita kama na mafunzo, tuanishe mapungufu, tufikirie uboreshaji.

    @mrfroasty
    Kuhusu hii project ya kuchapisha, tunamatatizo ya kutumia hii paypal. Nimezungumza na zamko, amenitumia check (bado sijaipata) ya £25 na mimi nitaweka zangu £25 baadae nitamtumia Sh Ally Saleh mojakwamoja. Natumai tutakuwa na kimtaji cha kuendeleza hiyo project.

  6. abdul 15/06/2010 kwa 9:33 mu ·

    Abdul
    mimi natoa pongezi kwa wale wote wanaosaidia kukua kwa web hii,hususan uongoziwa mzalendo.net nikiwa kijana wa kizanzibar ntajitahid kuwa pamoja nanyi kusaidia web hii ikue zaid.amin

  7. rasmi 15/06/2010 kwa 9:37 mu ·

    Hongera kwa kijana wetu mrfroasty na uongozi mzima wa Mzalendo. Imechukua kijana wetu mmoja kwa jina hilo hapo juu kuweza kutuwashia taa wengi kuweza kujua nini kilichotusibu na nini kifanyike Zanzibar ijitibu. Leo mwangaza wa nuru na neema tumeanza kuuona.

    Safari bado ni refu, wengine pengine tutaiwahi kuifikia; wengine allahu aalam; ila msingi imara umeanzishwa, Zanzibar imeamka- hakika haitolala tena.

    Kijana wetu atakumbuka wakati anaanzisha harakati hii, na karibu avunjike moyo; lakini Mola akampa subira na leo ndio hapa tulipo kuelekea Uhuru kamili.

    Mola tuwekee vijana wetu, uwaelekeze katika kheri, utuvushe na shari, Zanzibar iwe shwari.Ameen.

    I will always remain loyal and humble to my beloved motherland Zanzibar.

    Safari bado ni refu; biidhinillahi tutafika. Ameen.

  8. kindy 15/06/2010 kwa 12:15 um ·

    Hongera waandaaji na wadhamini wa mtandao huu kusema kweli kwa muda wa mwaka mmoja mumefanya kazi kubwa na munastahili sifa inshaala ndio iwe njia ya kuandaaa nchi yetu ipate mafanikiao kama haya well done keep it up the good job…………..

  9. mrfroasty 15/06/2010 kwa 7:57 um ·

    Shukurani kwa wozalendo wote ni imani yetu kuwa safari ni ndefu tuombe kheri inshallah amen…

    @Ashakh na wengine wote
    Kutakuwa na makala nzuri na muafaka kuhusiana na kura ya moani na serekali ya umoja wa kitaifa.Hii itakuwa na high priority kuchapwa fotocopi ili ujumbe uwafike wahusika (hapo priority ni kutokana na issue yenyewe ya kura ya maoni kuwa ni Julai).

    Hivyo hizo zenu inshallah zikitangulia kwa Shk Ally itakuwa jambo la maana, zitasaidia hapo kwenye fotocopi ya makala/nyaraka hio.

    Maasalaam,

  10. ashakh 16/06/2010 kwa 1:38 um ·

    @ mrfroasty, Shukran Inshaallah nitafanya hivyo na mara baada ya kukamilisha nitakujulisheni.

    Jengine kwa ajili ya historia, ningeomba kuanza kutayarisha chapisho (kitabu) maalum kwa ajili ya watoto na wajukuu wetu juu ya uanzishwaji wa mzalendo.net.

Comments are now closed for this article.