Ujumbe kwa watumiaji MZALENDO

Written by  //  07/08/2010  //  Ujumbe maalum  //  9 Comments

AS,

Naona ni wekeend na hivyo hakuna harakati nyingi za kupashana habari wacha nichukue nafasi kuzungumzia mawili matatu kwa niaba ya kamati ya uongozi.Kwanza tungelipenda kutoa nasaha kwa wazalendo kuwa lengo kuu la kuandika maoni ni kutoa mawazo au fikra zako juu ya chapisho unalolisoma.Kwa maana nyengine, unachangia au kuongezea juu ya maada hio iliopo hapo.Hii unasaidia kutoa elimu kwa wasomaji, na wakati mwengine unamsaidia Mwandishi kama ni feedback.

Lazima tukubaliane baadhi ya vitu kuwa si ukweli kuwa watu wote katika jamii wanaweza kuwa na uwezo wa kuandika wakafahamika.Hivyo hapo kunahitajika watu kujifahamu uwezo wao, yaani self determination.Kuna machapisho takriban 70 katika Dustbin, na vile vile kuna watumiaji takriban 4 wamebadilishiwa account kutoka account za uandishi na kwenda account za wanachama.Kwa meneno mengine wamepokonywa haki za kuchapa Makala Zao na kuachiwa haki za kusoma na kutoa maoni pekee.

Hii ndio orodha fupi ya majina hayo:

  1. jesha kombo
  2. Kulikoni Ughaibuni
  3. makame silima
  4. Mchamba wima

Sababu kadhaa za kuwanyima haki ya uandishi wajumbe hao:

1.Jesha na mjumbe nambari 3 (Makame), nadhani ni mjumbe mmoja.Ambae uongozi ulimjadili na kuona machapisho yake hayafikii kiwango.Mara ya mwanzo tulimbadilishia account, na hatimae nadhani akafungua account nyengine ambayo pia nadhani majuzi tumeona pia anatupatia kazi kubwa ya kuhariri anachokiandika.Tunakuomba kama itawezekana usitengeneze account nyengine.

Ikiwa utahisi unaweza kuacha kuandika makala zako mwenyewe, lakini unahitaji haki za uchapishaji kwa shughuli kama za copi paste kutoka magazetini au vyanzo vyengine tafadhali wasiliana nasi tutakurudishia haki hizo za uandishi.Lakini tunakuomba usiandike makala mwenyewe, hazifahamiki.Hii inaweza kuwa lugha ya Kiswahili si fasaha, na makala zako kwa muono wetu hazijafikia malengo.

2.Kulikoni Ughaibuni:Huyu naona alibadilishiwa account kwasababu ni spam, anakuja hapa kuchapa habari ambazo hazina uhusiano wowote na Zanzibar.Mara nyingi kuhusiana na Bongo flava za Tanganyika, ambazo ziko nje ya malengo ya MZALENDO.

4.Mchamba wima:Sina data kwanini alibadilishiwa account na kuondoshewa haki za kuchapa makala

Nukuu:

Hapo tunazungumza kunyimwa haki za kuchapa makala mpya tuu.Tufahamiane kuwa uongozi nao ni binadaamu wenye familia zao na harakati zao nyengine za kimaisha.Hivyo wajumbe wanaombwa  kama mtu hana cha kukizungumza, basi afuate maelekezo ya dini yetu kukaa kimya.Asome habari na aondoke, kuanza kuchapa vitu visivyo na tija kwenye maoni au machapisho ni kupotezeana muda na kusumbua wajumbe wengine.

Unaweza jiuliza ni vipi nitajua kama maoni yangu tija au hayana.Mara nyingi maoni yenye kuelekea kwenye kejeli, dharau, malumbano na mtoa maoni mwengine n.k.Maoni ya mtindo huu mara nyingi hayana faida wala tija yoyote.

Maandishi bora ni yale ambayo mtu anapoteza muda angalau 15-30 kuandika yaliyo kichwani mwake.Kablda hajakitoa yeye mwenyewe kukirudia na kuhariri maandishi yake kabla hajayaingiza MZALENDO.Hii pia unapunguza mzigo kwa uongozi, na pia ujumbe unaotoa unafika vizuri kwa walengwa.

Katika kuchapa makala mpya, mwandishi unaweza tia Tags, Category (Migawanyo), picha kutoka katika maktaba n.k.

Kila la kheri,

Mwandishi mrfroasty kwa niaba ya UONGOZI WA MZALENDO.

9 Comments on "Ujumbe kwa watumiaji MZALENDO"

  1. mrfroasty 07/08/2010 kwa 1:59 um ·

    Mwengine ambae nimemsahau hapo ni “Kirinjiro”, tafadhali kama unafanya mzaha na lugha unayoandika ni kheri ukaacha mzaha huo.

    Kama hufanyi mzaha hicho ndio kiswahili chako, tunakuomba ukaacha kabisa kutoa maoni.Kiswahili unachoandika hakifahamiki, ni slang ambayo hatujui hata inatokea wapi.

    Kila la kheri

  2. binamu 07/08/2010 kwa 3:38 um ·

    Jengine kwa faida ya wote wenye kuutembelea huu mtandao, inapasa tuelewe na tuthamini umuhimu wa habari. Haipendezi kuona watu wanaacha kuongea mambo ya kujenga badala yake wanautumia huu ukumbi kutukanana. Ni vyema tukaufanya mtandao wetu wenye kuvutia msomaji na pia ukawa ni njia ya kufikisha ujumbe wetu hata nje kwa wale wasiotembelea mitandao.
    Tutoe maoni ya kuishauri ama serikali iliyoko madarakani au viongozi walioko madarakani na hata wanaokuja kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumechangia kuleta maendeleo ya kujenga nchi yetu badala ya kutumia muda mwingi kuzozana ama kulumbana kati yetu.
    Haya ni maoni yangu.

  3. Bosco 07/08/2010 kwa 4:43 um ·

    Ni vizuri ikiwa utaratibu wa kuwafungia watu wanaokiuka maadili utakuepo lkn nashauri haki itendeke kwa kadri iwezekanavyo ili asije kudhulumiwa mtu lkn mungu ndie mjuzi wa kuhukumu. Mrfroasty wewe ni kiongozi mkubwa wa mzalendo kusema kua mchamba wima amefungiwa account yake bila ya kujua sababu hii inatia mashaka kidogo. Kwa upande mwengine nahisi pia wapo usalama wataifa ktk watumiaji wa huu mtandao kwa hivyo uongozi na wazalendo kwa ujumla inabidi tuwe makini ili hawa usalama wasije kututoa ktk lengo letu kuu au wasije kuusambaratisha huu mtandao.

  4. ole 07/08/2010 kwa 6:08 um ·

    Ni idea nzuri, lakini mimi ninamawazo kidogo, inewezekana pengine nitaenda kinyume na malengo ya mtandao huu.Lakini hili ni pendekezo tu halihusiani chochote na uendashaji.

    Mara nyingi huwa natembelea mitandao mingi kama vile Zanzinet na issamichuzi.blogspot nimegundua kwamba issamichuzi katika blog yake kunanapatika taarifa za functions mbali zinazotokea Tanganyika.

    Jambo ambalo kwa upande wa blog yetu tunayakosa. Nadhani ni kwa sababu hapa Zanzibar hatajakuwa familia sana au hatuna mtu ambae atajitolea kuhaha kutafuta habari na picha muhimu na matokeo halisi yanayotokea.

    Hatuna budi kutafuta kijana ambae atajitolea ili aweze kusaidia katika hili , ukiwaachia WAANDISH WETU MAARUFU Ally bin saleh na Bi Salma ambao wana kazi nyingi za uandishi.

    Pia tuchukue juhudi za maksudi kuutangaza mtandao huu ili Wazanzibar wote wauelewe vizuri hapa nyumbani kwani wao ndio wadau wakubwa.

    Naamini walio nje na wao watafaidika na matokeo muhimu yatakayotokea nyumbani kuyapata kwa wakati.

  5. mrfroasty 07/08/2010 kwa 10:09 um ·

    @Bosco,

    Hakuna aliefungiwa, ni haki za uchapishaji tuu.Hajafungiwa mtu, kiilivyo blogi nyingi zimetoa haki sawa na hii ambayo tunatoa yaani kutoa maoni pekee (bila ya haki za uandishi).MZALENDO imejikita kutoa haki za uchapishaji on of the basic one.Na hii haki ya ziada ndio inayojadiliwa na kuhitaji uhakiki.Kwani huwezi kuacha makala ambazo hazina standard fulani.

    Kuhusiana na hao usalama usiwe na wasi wasi, nao pia ni wananchi wana haki ya kujisomea habari za MZALENDO.

    @Ole,

    Nadhani mawazo hayo si mageni, tatizo linarudia pale pale kuwa kushiriki kwa wazanzibari wenyewe na kujitolea.Ni wazi kamati nzima ya uongozi iko nje ya nchi, na wala hatuna channel za kupata habari za kazi kwa ukaribu.Lakini ni habari muhimu na zimepewa section maalum >> Matangazo >> Kazi.Lakini ndio hivyo tena, nadhani kuna chapisho moja tuu la kazi.

  6. mrfroasty 07/08/2010 kwa 11:40 um ·

    @Bosco

    Huyo Mchamba Wima inawezekana nae alikuwa akichapisha vitu visivyo na tija.Haiwezekani account hio ilibadilishwa kwa sababu kama hizo.

  7. jesha kombo 08/08/2010 kwa 10:20 mu ·

    Msh mrfroasty naheshimu mamuzi yako inaonekana kuna mambo huyopendi ktk uwandishi wangu kutokana na maslahi yako binafsi ulionayo upande wa Vichogo(Bara)? nilazima ujirekebishe tuko kwenye mapambano ya Uzanzibar wewe hata ujifanye mbara rangi zako hazilingani na wao. tutazungumza zaid tukiwa Park kusheza boli.

  8. jesha kombo 08/08/2010 kwa 10:27 mu ·

    Mara nyingi mrfroasty usitumie kusema jina gani na jina gani ni mtu fulani(mmoja)? anyway nitakufahamisha zaid nikiwa Park au nikikutembelea?

  9. mrfroasty 08/08/2010 kwa 10:47 mu ·

    @Jesha,

    Kwanza naomba ufahamu kuwa hayo si maamuzi yangu binafsi, ni maamuzi ya uongozi wa MZALENDO.Pili, mimi personally sina maslahi yoyote na Bara wala sijaribu kujifanya mimi ni mbara.Nimezaliwa mzanzibari natumai hadi nitakufa bado mzanzibari.Kiilivyo ni siasa tuu, haina maana ya kuwa watu waanze kuchukiana.Ni wazi wapo wazanzibari wengi wenye asili ya Bara na wengine wameowa, wamezaa na wanaishi huko Bara.

    Anyways, sababu kubwa ya makala zako kupimwa na kuwa hazijafikia standard inatokana na kiswahili chako kina lafdhi fulani na si kiswahili sanifu.Ukiachana na lugha, pia huonekani kama ni mtu mwenye uwezo wa kuandika na kufahamika (kama ilivyoelezwa hapo juu).Naomba samahani kama hizo critics zote utashindwa kuzichukuwa in positive way.

    Sasa naomba tusianze malumbano na kuanza kurushiana madongo kuwa ni mimi binafsi yangu ndio sipendi makala zako.

    Kwa kumalizia suala la kukutana park au sehemu yoyote ile badala ya hapa MZALENDO siliwafiki.Hii inatokana na privacy reasons, hivyo masuala ya social meetings kutokea MZALENDO ni ngumu.

    Kila la kheri
    mrfroasty

Comments are now closed for this article.