Ujumbe maalum kwa watoa maoni
Written by administrator // 21/06/2010 // Ujumbe maalum // 4 Comments
AS,
Kumejitokeza mtindo wa watu kutoa maoni kwa mashambulizi ya jamii fulani au sehemu fulani ya Zanzibar.Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa MZALENDO itachukua hatua za kinidhamu kuhakikisha kuwa wajumbe hawatoi maoni yenye kukashifu jamii fulani katika visiwa vyetu.
Hivyo uongozi utahakikisha kuwa maoni yote yenye kulenga kugombanisha jamii, kuchochea, kutusi, kukashifu na kuleta mgawanyiko miongoni mwa wazanzibari yatafutwa haraka iwezekanavyo.Tunaomba ushirikiano na watumiaji wa mtandao.
Watu wanaombwa tafadhali watoe maoni yenye hoja za nguvu na tujitahid maoni hayo yawe yameambatana au kuendana na chapisho tuu bila ya kuanza kuzungumza masuala yasiokuepo kwenye chapisho hilo.Kama unahisi maada unayotaka kuzungumzia haipo kwenye chapisho hilo, basi poteza muda kuandika chapisho jipya.Hii inasaidia kuwa kila maada imejadiliwa kwa kina na sio msongamano wa maoni yasio na muelekeo.
Kutofautiana kimawazo inakubalika, lakini kashfa na kejeli dhidi ya jamii haiwezi kufumbiwa macho.
Shukurani kwa suhirikiano wenu,
Uongozi





4 Comments on "Ujumbe maalum kwa watoa maoni"
HADHIRIN TUPO PAMOJA NA NYIYE
Assallam Allaykum ?
Tunashkuru sana kwa kukumbushana, hata mm pia kwa upande wangu naunga mkono na nasisitiza pia kua ni vizuri sana tukawa tunangea vitu vya maana na vyenye faida kwa visiwa vyetu sio kulumbana au kukashifiana na maneno au matusi, na hapo ndio wanapopataka hao wabaya wetu ili wweze kututenganisha na iwe rahisi kwao kututawala. asanteni ndugu zangu wazanzibarian, TUUNGANE KUONDOSHA DHULMA ZANZIBAR. ALLAH IBARIKI ZANZIBAR NA WATU WAKE INSHAALLAH. AMEEN.
@ Uongozi,
Nashukuru kwa mshitusho wako, hapa hapana shaka nnayejadiliwa ni mimi , lakini hebu jamani tujiulize, Abuu Said kawahi kumtukana mtu laaa, kawahi kuitukana jamii yoyote ikiwemo ile ya kipemba au kiunguja laa, hamuoni kua na mia pia ni kati yeni. Niulezu tena jamani huu mtandao wa CUF, jawabu mumesema ni mtandao wa Wazanzibari, basi jamani mukubali kua Zanzibar kuna wana CUF na wana CCM.
Hamjaanza nyie kunilabour majina yasikua na maana kama vile TOBIAS, nilikua nawo jamaa zangu kule mlimani Dar es Salaam (MSAUD) kwa wasiojua ni Muslim Students Association of University of Dar es Salaam, nilikua nawambia kua huyu Mnafiq nao walikua wakinita GOZI, sasa mkesema mkinyamaza mimi sitochoka kukushtueni ndugu zangu kua kiongozi wenu Maalim Seif ni Mnafiq na hakufaeni anakuchezeeni huyo.
Sababu za maneno hayo ni kutokana na matukio mbalimbali, kama hivi yafuatayo:-
1)Tukio la mkombozi wetu Mzee Jumbe nyote mnalijua sina haja kulichambua.
2)Mauaji ya Pemba
3)Tukio la Mtedeni uchaguzi uliopita
Jiulizeni kwa nini yeye haguswi jamani, jibu ni kua ni mtu wao wanamtumia kuwatuliza upinzani.
4) Muafaka Upepo
Hebu niambieni mumeona wapi katika hii dunia, Vi/kiongozi chama cha upinzani anamsifu mpinzani mwenziwe na kutaka apewe tena muda wa kuendelea kutuibia… au mnataka kusema hamjui kama Hapa pangu yeye na shemegi yake na wanawe na mkewe washatumaliza kila na kuchukua kila pembe ya unguja na pemba ,eti leo Maalim na Jusa na mnmsifu huyu Karume Kenge… wacheni nyie amkeni huyu ni msaliti … haya mtanikumbuka maana hapa mtaona wenyewe na mwaka huu mnapigwa tena bao na 2015 Maalim anagombania tena…
Ahsanteni
Nadhani unaruka paragraph hii :
Maoni lazima yaendane na chapisho tafadhali na si vyenginevyo.
Masuali ya mtandao ni wa CUF au CCM yameshajibiwa katika FAQ (Frequently Asked Question), tembelea kitufe cha Misaada hapo kwenye top navigation.
Kila la kheri