Update:Fotocopi machapisho ya kizalendo
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 10/06/2010 // Ujumbe maalum // 1 Comment
Leo nimepigisha foto kopi yale machapisho mawili ya kizalendo.kwa jumla ni kopi 300 za “Barua ya Wazi kwa Wazalendo” wote wa Kizanzibari na kopi 275 kwa chapisho la “Siasa na Migogoro Zanzibar-Fikra mpya katika zama mpya”
Tumefanikiwa kupata idadi kubwa zaidi ya kopi kwa kuwa nilipata pahala pa rahisi zaidi ambako wamechapisha kopi moja kwa shs 30 badala ya shs 50 ambayo ndio bei ya kawaida sehemu nyingi.
Tutasambaza kopi kwa maeneo. kila eneo tutawapa kopi chache na wataoingia hamu ya kusoma zaidi watatoa kopi lakini pia tunataraji kuwa kopi moja itasomwa na watu wengi.
Usambazaji utakuwa stone town na nje ya mji lakini pia tutapeleka kopi huko Pemba.
Shukuran.
Ally Saleh
Nukuu:
- Tunapenda kutoa shukurani kwa Shk Hassan kwa mchango wake mkubwa wa kufanikisha project hiyo ya fotocopi.
- Pili shukurani kwa Shk Ally ambae bila ya yeye project hii ingekuwa ni ngumu.





One Comment on "Update:Fotocopi machapisho ya kizalendo"
Nawapongeza wazalendo wote kwa mchango wenu huo katika juhudi za kusogeza mbele mabadiliko ya kweli zanzibar. Wazo langu zaidi ni vyema kopi hizo zikafika maeneo mbali zaidi ambayo mm nayachukulia kama “hayajafunuka sawasawa” kama n’gambo za mji. Ni sawa kuanza kusambaza mjini ila ilani itolewa nakala hizo zifikie watu kumi kwa kila anayeipata. Hongereni sana, najuwa huo ni mwanzo wa kuelekea kufanya makubwa zaidi.
J