Update:Fotokopi Project
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 20/07/2010 // Ujumbe maalum // Zima maoni
salaam,
wana ukumbi zanzibar imepokea fedha za machapisho ya kizalendo mara mbili.Moja ilikuwa ni makala ya Ally Saleh na ile ya B.Ole. Kulitoleshwa nakala 300 na zaidi.Hizi zilisambazwa unguja zaidi lakini pia pemba. kopi zilikuwa zimebaki na hivi karibuni zilitumika katika semina ya vijana kuhusu civic education.
Pia kulitolewa pesa za kuchapisha KWA NINI UPIGE NDIO. tulichapisha kopi zaidi ya 3,000 na hizi zilisambazwa unguja na pemba. kopi hizo ziliibua msisimko mkubwa juu ya suala la kura ya maoni.
Wengine bado wanafikiri kuwa kama kuna harakati zilianza kuhusu kura ya maoni…hasa zile hoja 10 zilizokuwa zimetolewa.Kama kuna wana mtandao wowote ambao hawakuwa wamepata feedback basi hali ilkuwa ni hiyo.
Ally Saleh,




