Update:Mabadiliko katika mtandao
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 27/06/2010 // Ujumbe maalum // Zima maoni
AS,
MZALENDO.net imeboreshwa usiku wa leo.Kutakuwa na mabadiliko ya hapa na pale hususan kwa watunzi wa machapisho.Uboreshaji huo mwingi umetokea upande wa ndani ya MZALENDO na sio nje.
Vile vile tunaomba msaada wenu katika kuboresha sentensi na kiswahili kizima kilichotumika katika mtandao.Kwa wale wajumbe wapya, ni kuwa kamati ya ufundi ikiongozwa nami tunamaintain WordPress ya Kiswahili kwa ajili ya watu wengine wanaopendelea kuanzisha website zao kwa lugha ya Kiswahili.Hivyo mara tuu nilipomaliza kurelease WordPress3, nimefanya uboreshaji katika mtandao wa MZALENDO kutumia program mpya.
Katika mchakato huo wa kumaintain software hii katika lugha ya Kiswahili kuna makosa mengi na maneno mengi ambayo hayatambulikani katika lugha ya Kiswahili.Hivyo ukiona sentensi ina makosa au haifahamiki, tafadhali tutumie ujumbe admin@mzalendo.net.
Hii itasaidia kuboresha na kufanya Programu hii iwe inazungumza Kiswahili Fasaha zaidi.
Gr
mrfroasty-technical support




