Usalama wa watumiaji MZALENDO.NET
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 26/02/2011 // Ujumbe maalum // 5 Comments
AS,
Kwanza naomba nitoe maelezo mafupi kuhusiana na IP ndio nini.IP ni anwani ya mtumiaji wa computer katika mawasiliano ya Internet.Basically, website zote ikiwemo Google,Facebook zote hizi zinaweka records za IP za watembeleaji.
Kuna upotoshaji mkubwa wa kuwa usalama wa mtu uko hatarini kwa ajili tuu unajua IP address yake.Hii dhana ni potofu na haina ukweli wowote, ndio maana siku zote nimekuwa nikikimbia kuchokora mitambo kwa ajili ya kuficha hii.Lakini naona wazanzibari tumeshajazwa khofu na woga kila kipembe, hivyo napenda kutangaza rasmi kuwa records za IP address hazihifadhiwi na mtandao wetu wa MZALENDO.NET.Hivyo hili suala la IP kujitokeza sehemu yoyote limeondoka, kama ukiliona tena tafadhali tutumie maoni tuendeleze vita dhidi ya IP.
Information ambazo mtu anaweza kujua kutoka kwenye IP ni nchi, mtoa huduma e.g Zanlink.Hapa ataishia kujua tuu kama Internet hio mtu yuko wapi lakini si zaidi ya hapo.Tusitiane khofu zisizokuwa na kichwa wala miguu.Kuhakikisha hili tembelea website hii kujua IP yako na data utakazopata au anazoweza mtu kupata http://www.easy-hide-ip.com/
Email:
MZALENDO.NET kujiandikisha si lazima kutumia email yako unaweza kutumia mfano wowote wa email e.g mrfroasty@zanzlink.com itakubalika kabisa katika mtandao wetu.Ikihitajika kuwasiliana tutapeana maoni hapa.Maana isije kuwa nafanya under estimation za watu wana khofu kiasi gani….
Passwords:
Password jisikie huru kutumia yoyote hizi ziko encrypted with md5.Hadi sasa hakuna mtu duniani alieweza kusoma md5 encryption, hivyo ukipoteza password hakuna ujanja ni lazima utengeneze password nyengine…hata ukiwasiliana na uongozi pia nao hauna uwezo wa ku-recover password, kubwa tutalofanya ni kukutengenezea password mpya ili uweze kulogin halafu ubadilishe upendavyo.
Maasalaam,
mrfroasty-technical support





5 Comments on "Usalama wa watumiaji MZALENDO.NET"
Shukran kwa maelezo yako. Naifananisha IP kwenye computer kama vile number ya simu kwenye mawasiliano ya simu.
Shukran. Nashauri hii makala iwekwe ya kudumu (pengine inaweza kuhakikiwa) katika HELP ili watu waweze kuisoma au kama inawezekana kuwe na privacy statement ambayo hii makala itakuwa sehemu yake.
@Ashakh na wengine,
Namba ya simu ni too personal kulinganisha na IP address.IP haina madhara yoyote kwani haina information zozote za maana.Ili upate information muhimu inabidi lazima ISP (Internet Service Provider au kampuni ya Internet kwa ufupi) ahusike kutoa information hizo kuwa IP address hio ni ya mteja gani (kama itakuwa ni fixed, which hardly happen…normally zinagawiwa randomly).
Kama tujuavyo ISP hawezi kuvunja privacy za wateja wake, hufanya hivyo kwa ruhusa ya mahakama ikiwa kweli mteja huyo ni mtuhumiwa wa uhalifu tena kwa ruhusa (warant wa mahakama).Vyenginevyo kama ISP atagawa information anaweza kuingia kwenye utata.
Juu ya hapo, IP inaweza kuwa Dynamic ambayo ndio mara nyingi huwa hivyo.Yaani inabadilika au kugawiwa randomly kwa mtumiaji.Hii ndio kesi mara nyingi kuna program inayofanya kazi ya kugawa IP nayo inaitwa DHCP (Dynamic Host Configuration Protocol).Kwa hio IP yako inawezekana sio hio hio kila siku kama ilivyo nambari ya simu.
Bado hoja yangu iko pale pale kuwa IP haina uzito mkubwa kama wengi wanavyofikiria.Maana wengine hata wanafikiria ukijua IP, basi ushajua hadi nani alieko nyuma ya keyboard na anatoka nyumba gani!Hii sio kweli, wala mtu asitutishe kuwa yeye ni mtaalamu kiasi chote hicho cha kuweza kugundua wajumbe kwa kutumia IP.
Maasalaam,
mrfroasty
Ijulikane kutumia email ya kweli ina manufaa yake, hususan kwenye kutumia huduma ya password recovery endapo mtumiaji atasahau password yake unaweza kutumia huduma za kutengeneza password mpya.
Huduma hio inakutumia ujumbe wa email kukupa password mpya ili upate kulogin kwa ajili ya kutengeneza password mpya.Kwa hio hapo kuna hasara zake kama utajiunga kwa email ambayo si ya kweli.
Tumelirudia chapisho hili kukumbushana kuwa tusilaumu MZALENDO.NET ikiwa wajumbe watakutana mitaani na kupashana habari juu ya data zao private.
Ndani ya mtandao wa MZALENDO.NET hatukatazwi kujuana na kubadilishana data zetu za private.Kufanya hivyo ni kuwa mtumiaji anabeba jukumu hilo mwenyewe na anamuamini huyo anaempatia data hio.
Kiufundi ndani ya MZALENDO.NET hakuna uwezekano wa kumjua mtumiaji huyu ni nani na yuko nchi gani.Data za namna hii hazijahifadhiwa hapa katika mtandao huu.Tumefanya hivi kuepusha lawama zisizo na misingi yoyote na kujivua jukumu hili.
Ikiwa unahisi privacy yako ni muhimu na hupendelei kwa sababu moja au nyengine kujulikana.Tafadhali usijitambulishe ndani ya mtandao huu wala kumwambia mjumbe yoyote (hata uongozi) juu ya jina lako wala mahali unapoishi.
Kila la kheri
MZALENDO.NET