Ushauri:SuZa && Taasisi ya Kiswahili Zanzibar
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 04/07/2010 // Ujumbe maalum // Zima maoni
AS,
Kwa muda takriban mwaka mzima sasa mimi binafsi yangu nimekuwa ni msimamizi mkuu wa project hii ya kutafsiri na kumaintain programu ya WordPress kwa lugha ya Kiswahili.Kwa faida ya wote, programu ya WordPress ndio hii inayoendesha mtandao wa MZALENDO na mitandao mengine mingi hususan blogi.
Hii project ambayo inapatikana kwenye kiungo hiki sw.wordpress.org, ni project nzuri na yenye manufaa mingi kwa kuelimisha jamii.Binafsi yangu nimefarijika na kutumikia na kutoa mchango wangu katika project hii kwa muda wa mwaka mzima.
Maoni yangu na ushauri ni kuwa vijana wa kizanzibari hususan kamati ya wanafunzi wa SuZa kwenye department ya IT au Computer Science, wangeichukua na kuisimamia au kuwapatia wanafunzi wetu pale waweze kujipa changamoto za ulimwengu.Na pengine watajisomea mengi katika kwa kujitolea katika project hii.
Natumai kama wapo wahusika wa chuo hicho wanasoma chapisho hili wataweza kutake over project hii.MZALENDO ni moja ya website ambazo zinatumia kazi hii, hivyo tutaendelea na mimi personally bado nitaendelea kutoa mchango wangu hususan mwanzoni kutoa ushirikiano wa tools ambazo zinatumika katika project hio.
Maasalaam,
mrfroasty




