Habari

UNYANYASAJI WA KIJINSIA WASHAMIRI ZANZIBAR.

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakatuh!

Napenda kupanda JUKWAANI nikiwa na masikitiko makubwa juu ya vitendo vya kinyama na unyanyasaji vinavyoendelea Zanzibar, ambavyo kwa makusudi baadhi ya Waheshimiwa katika baadhi ya Wizara za SMZ wanakuwa wakiwanyanyasa dada zetu kwa namna moja au nyengine. Leo hapa nitataja Mifano miwili yaliyotokea katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Na ukitaka USHAHIDI ninao, kwa sababu yaliyowatokea wananihusu, ni ndugu zangu wa damu.

Tukianza na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali, Dada yangu mmoja ni Mwalimu katika Skuli fulani kisiwani Unguja, lakini kwa bahati mbaya alikuwa anakaa mbali na Skuli anayoifanyia kazi. Hivyo aliamua kwenda Wizarani kwenda kuomba uhamisho ili apangiwe kufanya kazi katika Skuli ya karibu na nyumbani, Lakini kilichofanyika baada ya kwenda Wizarani wenye mamlaka ya kumpa uhamisho, walimpa masharti ya kutembea naye kwanza ndipo wamtimizie ombi lake.

Mfano wa pili umejitokeza katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo, ndugu yangu amemaliza masomo yake ya afya na alikwenda hapo kwa lengo la kuomba ajira, lakini kilichomkuta huko kila mmoja ulimi ulikuwa nje kama Mbwa mwenye kiu kwa kumtamani, huku kila mmoja akimpa miadi njoo siku fulani saa ngapi ili apate muda muafaka wa kuzungumza naye na kueleza yake ya moyoni. MWISHO wa khabari natija yake nia zao wazee hao wasio na haya wala khofu kwa muumba wao hata chembe wakitaka kutembea naye, ili wamsaidie kupata ajira.

HIYO NDIO ZANZIBAR. HATUWEZI KUPIGA HATUA ZA MAENDELEO KWA MAMBO HAYA

Tagsslider
Share: