UVUJAJI WA MITIHANI UKIATHIRI TANZANIA BARA MITIHANI INARUDIWA UPYA LAKINI UKIATHIRI ZANZIBAR WANAFUNZI WANAFUTIWA MATOKEO?
Written by Ahmed Omar Khamis // 09/02/2012 // Habari // 12 Comments
Katika kuthibitisha kuwa wanafunzi wa kizanzibari walikuwa wakikandamizwa na bado wanakandamizwa katika masuala ya mitihani inayosimamiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni haya yaliyotokea mwaka huu. Ni jambo la kawaida kutokea kesi za udanganyifu katika ufanyaji, na usimamizi wa mitihani ya taifa jambo ambalo huchukuliwa kama ni la kwenda kinyume na maadili na kanuni za mitihani hivyo. Linapotokea suala hili, baraza la mitihani la Taifa huwachukulia hatua wale wote waliohusika. Jambo hili si geni linaonekana kila mwaka pale baadhi ya wanafunzi kufutiwa matokeo na walimu kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili kurejesha heshima na nidhamu ya mitihani.
Hata hivyo inapobainika kuwa usambazaji, ulinzi na usimamizi wa mitihani nao ulikuwa na matatizo na hivyo kuwa miongoni mwa sababu za kuharibika kwa mitihani hiyo, baraza la mitihani huwachukulia hatua wale waliosababisha kuvuja kwa mitihani na mitihani hiyo kurejewa upya. Hatua kama hii imeshawahi kuchukuliwa kwa baadhi ya mikoa kama Dar es Salaam na mengineyo kulazimika kurejea mitihani kwa kuwa mikoa hiyo imegundulika kuvujiwa na mitihani hiyo. Halkadhalika hatua kama hiyo imeshawahi kuchukuliwa kwa Tanzania nzima katika mwaka wa 1998 kwa kurejewa upya mitihani ya kidato cha 4.
Jambo kama hilo tulilitegemea pia kutokea kwa upande wa Zanzibar ambapo inaonekana mitihani ya kidato cha 4 ya mwaka 2011 inaonekana kukabiliwa na suala kama hilo. Hii ipo wazi kwani udanganyifu katika mitihani miaka yote hikuwahi kuwa wa kiwango na wa hali kama ilivyojitokeza mwaka huu. Hivi ni kweli hata wanafunzi wangu 15 wa kidato cha 4 wa skuli yangu ambao nawaamini hata kupata daraja la kwanza nao hawakujua kitu katika mitihani hiyo? na hivyo kulazimika kukopia majibu kutoka kwa wenzao katika vyumba vya kufanyia mitihani? Hivi inaingia akilini wanafunzi wote wa skuli husika wasweze kujiamini kufanya mitihani yao na kufanya vitendo vya udanganyifu katika vyumba vya mitihani? Hivi basi inawezekanaje skuli zaidi ya 7 zilizofutiwa matokeo ziwe na wanafunzi watupu wasio na uwezo wa kufanya mitihani bila ya kukopi majibu kwa wenzao? Tusisingizie udanganyifu wa wanafunzi tu, bali na mengine ya msingi yaliyosababisha tuyaseme. Tuwe wawazi, ukweli ni kwamba baadhi ya mitihani imevuja kabla ya kufanywa jambo lililopelekea wanafunzi kujadili kwa pamoja majibu na hivyo kufanana kwa majibu yao sahihi na yasio sahihi katika mitihani hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za usahihishaji za NECTA kujitokeza kwa hali hiyo inatosha kuwa ni ushahidi wa kufanya udanganyifu.
Mimi sisitetei kuwa wanafunzi hawakudanganya, la hasha! ambacho ninahoji ni kwa nini wahukumiwe wanafunzi wakati wao walipotezwa na mitihani iliyovuja wakati wakiwa katika hofu ya mitihani? Ni kawaida mwanafunzi akiona maswali aliyopewa leo na kuwambiwa ni mvujo ameyakuta kweli katika mtihani, basi ni dhahiri hatoacha kujadili na wenzake maswali mengine atakayopewa kwa kuamini ndio atafanikiwa katika mitihani. Huu ndio msingi wa tatizo ulivyo.
Nilipokwenda mimi, Katibu Mkuu wa Vijana Taifa Mhe. Khalifa Abdala Ali kama Uongozi wa vijana wa CUF Taifa pamoja na mwakilishi wa viti Maalum na Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa CUF Mhe. Bi Zakia ili kujua sababu ya tatizo hili na kuuuliza kama Serikali ya Zanzibar imeshafuatilia, akiwa ofisini kwake Mazizini Unguja, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Abdalla Mzee (Mpangile) alijibu kuwa yaliyotendeka dhidi ya wanafunzi wetu ni haki na wao wanajiandaa kuwachukulia hatua zaidi za kinidhamu wasimamizi wa mitihani na walimu wote waliohusika na kusababisha hayo yaliyotokea. Tulipomhoji kuwa haoni kama hili jambo si la kawaida bali msingi wa tatizo ni la kuvuja mitihani, alijibu hata iweje wao kama wizara hawatauunga mkono udanganyifu kwa kuwa umetendeka kweli na NECTA imewaletea ushahidi bali watakubaliana na maamuzi ya NECTA ya kuwafutia matokeo wanafunzi akiwemo mototo wake mwenyewe aliyefanya mtihani yake katika skuli ya Laureate Internaional ya Zanzibar, skuli ambayo imefutiwa matokeo yake yote na kubakishwa matokeo ya wanafunzi watatu tu. Bwana Mpangile aliendelea kutupa maelezo kwa kutwambia kuwa watu kila jambo wanakimbilia kusema ni tatizo la muungano lna jambo hili pia watadai hivyo lakini sio kweli hili ni tatizo la wanafunzi wetu na walimu wetu.
Hata hivyo mimi binafsi na ujumbe tuliokwenda kwake hatukubaliani na hoja na misimamo ya Naibu Katibu Mkuu huyo kwani habari za kuvuja kwa mitihani zilipatikana lakini tukashangazwa na kuendelea kwa mitihani hiyo. Sasa tutegemee nini? Mi mwanafunzi yupi atakaepata jawabu sahihi na swali lake akalikuta katika mtihani asiliandike vilevile alivyolipata na kuliweka kichwani? Tuwe wawazi tatizo ni uvujaji wa mitihani uliodharauliwa kwa kuwa umeathiri zaidi Zanzibar, tusiwaonee wanafunzi. Njia pekee ni maitihani kurejewa upya kama ilivyo kawaida. Hili ni tatizo la pande mbili, NECTA ilizembea na kusababisha kuvuja kwa mitihani kwa upande mmoja na wanafunzi walikwenda na majibu yao katika chumba cha kufanyia mtihani kwa upande wa pili.
Wizara ya Elimu Zanzibar haitatenda haki kwa kukubali kufutiwa matokeo yao wanafunzi wengi kama ilivyotokea. Tunaiomba wizara iwache mzaha na siasa za kuabudu muungano, wahakikishe mitihani hii inarejewa si hivyo sisi kama viongozi wa vijana tutahamasisha maandamano Zanzibar nzima mpaka kieleweke kwani tunafahamu kuwa jambo kama hili likitokea kwa Tanzania bara mitihani hufanywa upya..




12 Comments on "UVUJAJI WA MITIHANI UKIATHIRI TANZANIA BARA MITIHANI INARUDIWA UPYA LAKINI UKIATHIRI ZANZIBAR WANAFUNZI WANAFUTIWA MATOKEO?"
Huu ukandamizaji haukuanza leo na muda mrefu. Nakumbuka Mwl Seif alipokuwa waziri wa elimu alikumbana suala hili na kwa kuwa matokeo yakija basi Wazanzibari wengi ama wanafeli kabisa au wanakuwa na daraja za mwisho (4th grade). Na wanafunzi hawa hawa wakibahatika kusoma nje wanapasi vizuri sana. Na statistic nyingi zilikuwa wanaofeli ni vijana wa kiarabu hasa. (Ubaguzi huo).
Nakumbuka, kama sikusei, Mwl. Seif aligombania mpaka ikabidi wapelekwe wanafunzi angalau 10 kili mwaka Chuo Kukuu Dar kwa kuchaguliwa na wizara ya Zanzibar. Na pia hata wanafunzi wa Form 4, SMZ ilikuwa inawachagua wale ambao wanaona matokeo yao ya mtihani unaotoka bara hayalingani ya yale matokeo yao ya kila siku, na kuwalipia tena ili wafanye mtihani kwa mara ya pili, na wengi wao kama si wote wanapasi.
Nakumbuka katika walimu wetu pale mbweni waliowahi kupelekwa Chuo Kukuu Dar walituhadiasia kuwa siku ya kujiregista pale chuoni wanafunzi wa bara wote wana Division 1 au 2 na Wazanzibari woa wamekuja ati kwa madai ya SMZ wana division 4 au wahawana kabisa (Walikuwa wanaona aibu), lakini sasa ile mitihani ya mwanzo ya majaribio pale chuoni wao (wazanzibari ndio wnaokuwa wenye result nzuri zaiadi kuliko za wabara waliokuwa na division1)
Kwa ufupi huu ubaguzi uko zamani na unajulikana na SMZ. Lakini sijui mpaka lini tuwafuata wao?
Kuna haja ya kufanaya mabadiliko ya kuwa na baraza letu wenyewe la elimu ya juu. Kwani tunao wasomi na uwezo wa kutunga mitihani yetu wenyewe.
Waliofeli Pemba Wangapi na Unguja Wamgapi, Waliopata Division IV wangapi pia. Je hawa watafanya nini Zanzibar isiyo na ajira na wengi hawana uwezo wa kwenye school binafsi zakujiendeleza? Idadi kama hiyo au zaidi itafeli tena mwakani.. Hawa vijana watamalizikia kuihama nchi, Watanganyika wataletwa… Hiyo ndio Serekali mbili kuelekea Moja. Huu mtindo upo zamannnnnnnnnnnnnniiiiiiiiiiiiiii sisi hatujakamata mita. Kufelishwa, mimi namjua mtu alipata Div 3 Pemba, kama miaka 8 iliyopita, Akafanikiwa kwenye Kusoma bara kidato cha 5 na 6 pia akafanikiwa kwenda Chuo kikuu, Amechukua first class degree pale tena kwa bwebwe. Hamuoni kama hawa jamaa wanatufelisha….Uhuru wa nchi yetu Muhimu.
ninasikitika kwa nini mtihani usirejewe pili kwanini kama uliushukia mtihani kuvuja kwa nini usisimamimshwe kwanini watu wahusika wa wizara wasichukuliwe hatuwa kwanini isiundwe tume na kushirikiana na usalama wa taifa na pilisi kuchunguza na kuwachukulia hatuwa.SASA NDUGU ZETU WATAVUTA BANGI VIJIWENI NA MASKANI KAMA BOOB MALE NA BAADA YA KUWA MACHANGU SASA WATAGEUKA SEHEWA,USHAURI WA BURE SMZ RUDISHENI BARAZA LA MINIHANI ZANZIBAR NECZA BADALA YA NECTA ,halafu kama ilivyo kawaida raisi atamuita mwanafunzi bora wa mwanzo ikulu huku wengi wakisubiri bangi na unga na umalaya mungu wavuwe vijana wa zanzibar na majanga na binu za wana IZRAILWEUSI TANGANYIKA
La muhimu ni kuwa na wizara ya elimu ya juu yetu wenyewe, baraza la mitihani letu wenyewe. Tutunge mitihani yetu wenyewe. Wasomi wapo, uwezo upo. Sijui tunaogopa nini?
Na kama woa hawatataka kutambua shahada zetu si lazima. La muhimu ni kuwa kiwango cha elimu kiwe kinakubalika kimataifa. Na hili linawezekana, ni kuungana na mabaraza ya mitihani ya kimataifa tu.
Jamani sasa tunakoelekea ni kubaya sna, swala la elimu ni suala la kitaalam sio swala la kisiasa.
Wakati unafanyika mtihani wa kidato cha 4 pepa wanafunzi wanazijadili kwenye daladala kwa fahar kubwa na baadhi ya walim wanashiriki ktk upumbavu ule. Nlipatwa na hasira lakini ilibidi nimlani shetani.
Wanafunzi hawana confidence ktk yale wanayoyafanya inakua ni akili za kuchangiwa zaid kuliko akili zao ni km sisi tuliopo hapa mzalendo. Wengi ya wanafunzi waulize bongo fleva au manchester united hapo wamekariri kila kitu. Na wanafunzi waliokua siriou na masomo yao basi na matokeo yao pia ni mazur tumewaona.
Kuna jirani yangu hapa mtoto wake wa kike kila ukimwambia ende akasome yeye 24/7 ni tamthlia za kibongo, mara tamthilia za kizungu, mtihani umefika kachanganyikiwa na kakutana na wenziwe na kujadili mvujo matokeo yake ndo km haya.
Walimu pia wanamatatizo yao, na ttzo kubwa silabasi hawamalizi na hii ni kutokana na mambo mengi ambayo wanapaswa kuyafanya ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi, nyenzo za kufundishia pia ni chache. Walimu pia maslahi yao ya fedha ni madogo kwa hio wao huandaa tuition nyingi kuliko kukusomesha darasani.
Kwa upande mwengine mttzo ya kudesa kwenye mitihani yapo mpaka vyuo vikuu, nami nakubali 100% kwamba mwanafunzi akikopia lazma afutiwe matokeo yake kwa sbb baadae mtu yule anaendlea na tabia ya kukopia kopia mpaka anaajiriwa kazini bado yeye anakopia tu na matokeo yake tunapata ma manager na makatibu wakuu hawana ubunifu wowote.
Kuna softwear ya kuzuia plagiarism ambayo pia ni muhim ktk vyuo vyetu vikuu bora ikuwepo koz naona swala hili ni ttzo kubwa sana kwa wanafunzi wetu wa vyuoni. assignment wanadesa na dissertation pia wanadesa ni maajabu kabisa.
Kuhusu kurejewa kwa mtihani inategemea na bajeti, sio rahisi kama mnavyofikiria hasa ukiangalia cost strategy hasa zinavyotaka, lakini baraza la mitihani wanaweza kuweka cost sharing ukizingatia wahanga ndio ndio wahitaji, au wende wakarejiste wawe private candidate.
There is no appeal or extra time in academic issues what student has to do is to work hard and harder and build the sense of confidence and believe that u can do something.
Hata hivyo, mwandishi umelitia swala hili kwenye kero za muungano lakini sidhani kama linafit lakini hata km zanzibar tutakua na baraza letu la mitihani basi mambo hayo hapo juu nliyoyataja basi yanatakiwa kufanyiwa utafiti na kupatiwa sustainable solutio.
Mwisho mwandishi utakuja kusema ICU ya mnazimoja imekufa kwa sbb ya muungano.
Mwandishi mbukwa-mbukwa mbukwa , taire taire muandishi taire. fanya uchunguzi zaidi
mm tatizo langu kama mtihani ulivuja kwa nn wasiwachukulie hatuwa watu wahusika kwa nini wasisimamishe mtihani kwa nini wasirejee kufanya mtihani sasa inakuwaje wawafutie matokeo kisha tanganyika hutokea hivyo sio mara moja lakini kwa nini wao hupewa wanafunzi kurejelea mtihanii
hayo unayoyasema wewe embesakua ya watoto hawataki kusoma, ni wacheza, baadhi ya walimu hawatekelezi majumkumu yao ni mambo ya kila siku. Hili ni geni kwa Zanzibar yetu. Ni uvujaji wa mitihani uliodharauliwa. Hata tukituhumu Muungano kuhusu ukandamizaji wa wanafunzi wa Zanzibar sikuanza mimi, kaanza kipenzi cha Karume, muasisi na Katibu wa Afroshirazi, Muasisi wa Mapinduzi, Rais wa Pili wa Zanzibar na Makamo wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mzee Aboud Jumbe katika kitabu chake, The Partnership: Tanfanyika and Zanzibar Union. Humo kabainisha mengi ya dharau na ukamndamizaji wa wanafunzi waislamu hususan wa kizanzibari. Wewe ni mkereketwa, muuza nchi huezi kufahamu haya lakini tutapambana na wewe na wenzako kama wewe.
pemba islamic college
high view
laurent int
bilal islamic
http://196.44.162.14/necta2011/CSEE%202011/s1291.htm
http://196.44.162.14/necta2011/CSEE%202011/s1085.htm
http://196.44.162.14/necta2011/CSEE%202011/s1366.htm
http://196.44.162.14/necta2011/CSEE%202011/s1360.htm
Hakuna haja ya kukata rufaa. Tunataka baraza la mitihani la znz. Maandamano yadai hilo.
Tunataka wawakilishi wapeleke hoja binafsi ktk blw kuunda baraza la mitihani la znz.
Wazanzibari ni ma bwege sana sio kila jambo ni la kuungana jamani. Hamuwezi kuvaliana chupi bana.
Muandishi na wazalendo naomba munijibu maswali haya jee huo mtihani unaotaka urejewe watarejea wale waliofeli tu au na wale waliofaulu vizuri au waliofaulu kiwango cha kwaida au vp?
Jee, kama aliyefaulu sasa hivi akija kufeli naye ana haki ya kushauri mtihani urejewe tena?
Jee, wale watakaorejea mtihani wakifeli au kokopia tena pia mtihani urejewe tena?
Kama wizara ya elimu inatabia ya kurejea mitihani ya waliofeli kwa kutumia gharama za walipa kodi hio ndio wazir na makatibu wakuu wote inayotakiwa kujiuzulu.
Supplimentary exams mwanafunzi anatakiwa kulipia mwenyewe gharama na sio kuleta biashara ya kitoto kila watu wakifeli warejee mitihani kwa gharama ya serikali na km mwanafunzi yupo tayar kufanya exams basi private candidate zipo nafasi tele bado hajachelewa.
Ikiwa wanafunzi wamefutiwa matokea, walimu na wasimamazi, wasahihishaji na wakuu wa maidara na mawizara watafanya nini?
Vipi jamani ile supply of chain hapa haitumiki?
Ninachosema mimi wanafunzi wetu walichonacho ni kucram majibu hivyo iawezekana mwalimu akawafundisha maswali na wao siku ya mtihani yakatokea kama yalivyo na kuyajibu kama walivyofundishwa.
Naomba nipewe maana ya kukopia ni ipi?
Ashakh mimi naamini kwa asilimia kubwa mwalimu aliwaandikia ubaoni hayo majibu.
Siyo wanafunzi wote wakihifadhi basi wanaweza kutoa kwa asilimia mia moja kile walichohifadhi, lazima vingetafautiana. Wengine wangekosea spelling wengine wangesahau baadhi ya maneno na kadhalika.
Walimu na wasimamizi ndiyo wa kutupiwa lawama kwa kiwango kikubwa kwa kuwapotosha wanafunzi. Mfano katika ile skuli moja sijui ni ya wapi wanafunzi walikuwa wamepewa kuchagua a, b, c au d lakini darasa zima likajaza o jee hii inakuwaje?
Hapa wachawi ni sisi wazazi mengine ni ya kuongezea tu.