Amazing Swahili girl shocks the TV presenter
Written by Stonetown (Kiongozi) // 13/02/2012 // Vidio // 23 Comments
httpv://www.youtube.com/watch?v=1WifsCB6bfM
Written by Stonetown (Kiongozi) // 13/02/2012 // Vidio // 23 Comments
httpv://www.youtube.com/watch?v=1WifsCB6bfM
23 Comments on "Amazing Swahili girl shocks the TV presenter"
ASSALAAMU ALAIKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAATUH
I WISH TO CONVEY MY SINCERE CONGRATULATIONS TO THE PARENTS OF RAFIA FOR
THEIR ENDLESS EFFORT TO ENABLE THEIR DAUGHTER SUCCESSFULLY ACHIEVE THIS
HONOUR, ESPECIALLY BEING HERE IN LONDON WITH THE DIFFICULT WESTERNISED
CULTURE AND PEER PRESSURE TO OUR CHILDREN.
MAY ALLAH BLESS YOU AND YOUR FAMILY, AND GUIDE US (JAMII IL ISLAM) TO FOLLOW
THE RIGHT PATH.
AAMEEN
MASHAALLAH
AlhamduliLlah Mwenyezi katupa mtoto kama huyu. MwenyeziMngu amfungulie kila la kheir na baraka pamoja na wazee wake. Ni fakhari kwetu kuwa na mtoto kama huyu ambaye anaonesha kuwa na mustaqbal mzuri wa dini
Saa nyengine hujiuliza kwa nini ikaandikwa ‘Amazing Swahili Girl…’ Huyu mtoto wazee wake asili ni Wazanzibari waliotoka Omani. Lakini haikuwa Muomani wala Mzanzibari. Kwa nini?
Moja ya ndugu zetu wenye asili ya kiomani juu ya kuipenda Zanzibar na kuwa na itikadi kuwa ndio kwao, hawakubaliki kuwa ni waZanzibari na utawala ulipo sasa na wanaonekana ni wageni tu. Maskin haikuweza hata kusemwa kuwa ni Muingereza…Lakini hongera chaguo ni USWAHILI ambao mtu yeyote hana uwezo wa kumnyang’anya. The best choice ‘USWAHILI’
Fakhri yetu Waswahili
A/alaikum waZalendo wote
Kwanza kabisa sinabudi kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujaalia kuwa na afya njema na kutupa mtoto mwenye bidii na anayeipenda dini yake ya kiislam. Tunamuomba M/mungu amzidishie fahamu ili azidi kuhifadhi kwa kila anachosoma na anachosomeshwa, ampe siha nzuri, maisha mema na marefu, na amjaalie mustaqbali wake uwemzuri wenye kheri na baraka pamoja na WAZAZI wake woote. Ameen.
@Makame Ame.
Maalim wangu nakuomba usisikitike sana kwa kuona huyu mtoto wetu kaitwa “SWAHILI GIRL”
Kwanza kabisa nataka kuwakumbusha kuwa hili neno “SWAHILI” ni neno lililotoka katika lugha ya kiarabu, linalotamkwa kwa lafdhi ya *SAAHIL* Mana yake ni sungosungo ya bahari, kwa hivo ninavofahamu mimi? ikiwa sikosei!! Mtu yeyote anayeishi katika sehemu hizo huweza kuitwa mswahili, akiwa muarabu, mzungu au muafrika. Kwa mtazamo wangu mimi nahisi si-jambo lakututafunisha vichwa vyetu.
NAWAKILISHA
MCHONGOMA
Ndugu yangu Mchongoma
Haijanisikitisha hata chembe huyo mtoto kuitwa Mswahili. Bakhti ni mtoto nnayemjuwa. Kwa kweli nimefurahi kuitwa Mswahili kwa kuwa hilo neno limeondoa ugozi. Hakuna wa kumnyang’anya Uswahili wake. Lakini ingesemwa Mzanzibari au Muonamani upo uwezo wa kunyang’anywa hayo…hasa huo Uzanzibari. Angekataliwa. Na si hasa hapa jamvini ingekuwa hivyo.
Tujivunie Uswahili wetu sisi Waswahili kwani ndio unaotuunganisha!
salam wazanzibar, al hamdulillah mashaallah mwenyeenzi mungu azidishie elmu na subra yeye na wazee wake, kwa kweli mtoto huyu imewaamsha watoto wetu wazidi kupigania dini yao na kuijua ijapo kuwa tunaishi katika mazingira magumu hasa ulaya na amerika ,mimi mwenyewe nimewaonyesha wanangu na wamefurahi sana , na wao pia watajitahidi na wengine pia. haya ndio maisha tunayo stahiki kuwapa watoto zetu tuendelee kuwaongoza ili wafanikiwe na dunia na akhera na baba au mama utakapo kufa ni kuuliza vipi uliposhi au vipi umeiacha familia yako na nini tutaweza kupata jibu nadhani mumenielewa shurkani kwa sote,
Hongera Rafia.inshallah utakapo tembelea Zanzibar usikose kutujuulisha ,tuna zawadi kemkem mashaalah
Allah ukuzidishie elimu ,maarifa,na tafsiri.amin
Maisha ni njia ndefu ambayo unakoenda hujuwi itakuwaje ila Mungu anajuwa. Mimi kila siku kufikiria namna gani Media inaweza kutupeleka mahali ambapo hujafikiria. Kuna watoto wengi katika Europe ambao wako very much talented kwa vitu mbali mbali kama vile mipira na kadhalika lakini inapofikia kuanza kutiwa au kufikia kwenye media exposure basi nakuwa na wasi wasi sana kutokana kuwa wengi wetu tumetafuta maisha kwa njia mbali mbali alimradi tu tunaweza kuendelea na maisha yetu nje na nyumbali (Zanzibar) na hizi media eg TV au news paper hutafuta kila habari ili kupamba magazeti yake. Jee kwa hili tumejitayarisha vipi ili kupambana na challange za baadae kwa watoto wetu naoma wana mzalendo munichangie ili tuweze kupata way forward. Nafkiri wengi watakuwa wamenielewa.
Na wapa hongera wazee wa Rafia . Na muombaMola ( s.w.t) . amfungulie kila la kheri na mafanikio katika juhui yakuijua dini yake, na awe mfano kwa watoto onamu watoto wote wa ki islamu.
Ku itwa mswahili ni fakhar kwa sababu ina juilisha culture, history , watu, na lugha. Sote tuna jivunia kama tunavyo jivunia Uzazibari wetu.
Kumbukeni kwamba muendeshaji wakipindi ali muuliza lugha gani wazungumza nyumbani na akajibu Swahili. Na hilo suala lime baaa ya kusikia fasaha yake ya lugha ya kiarabu. hiyo ni sifa ya watu wa mwambao na Zanzibar kwa kutamakan lugha nyigi wana apo amua kujifunza. Dini na ilimu nyegine hii yatoa muangaza w
inaendelea.—- yatoa muangaza wa historia yetu na culture yetu.
Congratulation RAFIA .
KEEP IT UP.
Mimi najiuliza huyu mtoto kawekwa hapa ili atoe ukumbusho au watu washangae km mtoto anasema kiarabu? Watoto km hawa mbona tunao wengi tu hapa znz au kwa sbb huyu yupo Ulaya?
Pili wazee wa huyu mtoto wanatakiwa wawe makini sana, mi wala sijui malengo yao nini kumtia huyu mtoto mdogo kwenye You Tube, mtoto bado mdogo lengo lenu nini? au watu wamuone tu?
Nashauri wazazi msiwe na tabia ya kumtia mtoto wenu ktk mambo haya bado mapema sana, mtoto km anamuelekeo mzur wa kusoma atafutiwe school akasome sio mnamkaririsha hadith na aya kisha mnaenda kumtia You Tube, what for?
Mtoto yupo stage ya kwanza hata adolescent stage hajafika munaanza kumtafutia umaarufu mwacheni kwanza akasome kwa maana ya neno kusoma kisha ndo mwenyewe atajua nini afanye insh.
Kwa upande mwengine, watu wengi tumeconcentrate na umri wa mtoto ila aliyoyasema wengi wetu aidha hatujafaham au tumeyapuuza. Na ukweli ni kwamba mtoto anatoa message kwa wanamzalendo kwamba waache ubaguzi kwa sbb Mola wetu mlezi hatizami sura zetu wala ngozi zetu ila yeye hutazama nyoyo zetu jee zipo safi?
Then, wazalendo tuwache ubaguzi na matusi na tuangalia mafunzo ya Uislam km mtoto anavyotukumbusha.
MY DEAR BRO/SISTER, @ EMBESAKUA
I AGREE WITH YOU ON YOUR LAST COMMENT BUT MAY NOT AGREE ON THE FIRST.
AM NOT THE PARENT OF RAFIA BUT AM THE ONE WHO PUT THIS CLIP HERE.
MY INTENTIONS WERE:-
• TO MOTIVATE OUR FELLOW PARENTS AND MAKE AN EFFORT TO SEND OUR CHILDREN TO MADRASSA.
• TO USE RAFIA AS A ROLE MODEL TO OTHER CHILDREN LIVING IN THIS WESTERN WORLD – 90% WHO ARE ON YOU TUBE ARE TEENAGERS.
• TO OPEN DOORS FOR SUCH A SUCCESS – FOR FURTHER STUDIES IN INTERNATIONAL ISLAMIC INSTITUTES
I AM NOT AWARE OF ANY HADITH OR AYAT THAT SAYS ITS WRONG TO PRAISE OR PUBLICISE A SUCCESS. INFACT I CAN REMEMBER THAT THERE WAS A HADITH THAT, PROPHET MOHAMMAD (SAW), HE CONDUCTED QURAN COMPETITION AND PRAISED UBAID BIN QAAD AS THE BEST RECITORS DURING HIS TIME (OR YOU MAY CORRECT ME).
WE KNOW THEY ARE OTHERS WHO MAY HAVE MORE TALENTS THAN RAFIA, BUT IN THIS INSTANCE, WASWAHILI WASEMA “MCHEZA KWAO HUTUZWA”, THEREFORE, IT IS OUR DUTY TO NURTURE AND DEVELOP SUCH TALENTS IF WE CAN.
IT IS SO SAD THAT WE HAVE SUCH NARROW MINDED PEOPLE IN OUR SOCIETY, NOW THAT WE HAVE VAST INFORMATION AVAILABLE ON LINE, WHY DON’T WE USE OUR TIME MORE EFFICIENTLY TO EXPLORE BETTER AND USEFUL INFORMATION AND BE OPEN TO WHAT IS HAPPENING IN THE WORLD.
LET US NOT EVER COMPARE THE ISLAMIC EDUCATION IN ZANZIBAR AND IN LONDON, WHERE WE HAVE VERY FEW MADRASSAS, AND HAVE TO TAKE AND COLLECT THE CHILDREN TO MADRASSA EVERY DAY AND TO SCHOOLS, HOSPITALS, ETC. WE HAVE TO BE WITH THE CHILDREN 24-7. APART FROM ALL THE CONSTRAINTS, DISTANCE, BUSES, PEER PRESSURE, SNOW, APPOINTMENTS, SCHOOL ACTIVITIES, AND WE HAVE SEVERAL CHILDREN TO LOOK AFTER.
LET US BE OPEN, CELEBRATE OUR SUCCESSES AND USE OUR FAILURES AS EXPERIENCES OR HURDLES THAT WE NEED TO JUMP AND GET OVER THEM IN LIFE.
Assalaam alaikum wanaukumbi . Ndugu embesakua hivi sasa tunaishi au tumo katika nyakati za teknolojia ya internet nk na sio nyakati zile za dark ages ambapo ilikuwa tunu kuwa na TV , simu ya mkononi n.k. Ukisikiliza kipengele cha mwanzo huyu binti anasema ikiwa utafanya jema kwa nia safi ya Allah basi utapata thawabu nyingi pasi na mfano na ukiwa utafanya jema hata liwe kubwa kiasi gani kwa nia ya kujionesha basi kwa allah huna kitu . Tumpongeze huyu aliemrecord huyu bint na kumuweka hapa kwenye mzalendo na you tube ili watoto wenzake wafate mfano wake . ni watoto wangapi wanapotea huku ulaya na hata hapo znz . Maudhui hapa ni kufundisha wala sio kumpatia huyu mtoto umaarufu . Ndugu embesakua je unae mtoto aliefikia stage kama ya huyu au zaidi yake . kwa znz ni rahisi kufanya haya lakini ukiishi nchi za western au European ni mtihani ulioje Inshallah Allah atuongoze katika njia iliyonyooka Amin
Mbali ya objective kufikiwa ya kuiweka hii clip hapa jamvini. Dua ngapi kaombewa huyu mtoto. Hili ni dogo? Ninaamini sote tuliomuombea pamoja na wazazi wake na sisi wenyewe tuliomba kwa moyo na nia safi. hilo si jambo dogo kwa MwenyeziMngu. Kwani jamani hatujui kwamba Mngu hufurahi mja wake anapomuomba?
Zikiwa zipo nyengine za wengine ziwekwe tushajiishe watoto wetu. Mimi nakumbuka nilipokuwa mdogo wazee wangu wakinishajiisha kusoma Quran kwa tajweed mbele ya watu kwenye mahafla kemkem. Na kweli imenisaidia, tena sana. Na pengine kungekuwa na YouTube waqti huo wazee wangu wasingesita kufanya hivyo.
Tushajiishe watoto wetu katika dini khususan elimu ya TAWHEED (kama katika mfano huu), kwani ndio ufunguo wa kumjuwa Mwenyewe SWT
Embesakua nani aliyekuambia wazee wa huyu mtoto Rafia ndio aliyo tuma hii video kwenye YOUTUBE? Kama huna cha kusema ni kheri ukanyamaza kimnya. Hapa UK kila siku jumuiya za Ki-Islamu zinajitahidi kufanya mshindano kwa watoto wao na Rafia amekwenda hapo unapo muona kwa kazi hiyo na hiyo ikarushwa na Islamic Channel ya UK. Kwasababu ya watu kuwa na mapenzi ya dini yao na kutokana na mazingira ya hapa UK kutokezea mtoto mdogo wa miaka minane akazungumza kama vile amezaliwa Oman basi ilikuwa na fahari kubwa kwa sisi waswahili ehee nasema waswahili wote wa afrika mashariki mpaka burundi ambao ndio tuko pamoja kwenye harakati zetu za dini.
Kama Zanzibar wapo wengi pia ni fahari yetu na tunajivunia kwa hilo na tunaomba wasiwe wachache hao wote ni ndugi zetu jirani zetu wahisani zetu kwa hiyo bado tunajivunia lakini kwa mtoto Rafia anastahili sifa yake kwa hapo alipo kuweza kuhitimu na akawa anaendelea vizuri na masomo yake ya dini na dunia.
Embesakua pale tunapo ona ndugi zetu wadodo hasa wakike wanaharibika sisi wengine inatuuma sana japo kuwa wengine si ndugi zetu wa damu lakini ni ndugi zetu katika uislamu. Inatusikitisha leo Zanzibar kuona mabaradhuli baada ya kupungua iimekuwa wanazidi. Pombe kila kona. Leo ktukisikia kuna sober house na vijana wanapata matibabu basi tunafurahia kwasababu wote ni ndugi zetu… kwa hiyo kaka baadhi ya wakati usukurupuke kuanza kushutumu kwa kitu usicho kijuwa.
a/a @ Kassem
basi inatosha wala usireje tena maneno yako ni makali
amesha fahamu huyo mlengwa, naomba tafadhali .
KAMSHUU.
@ Zanzibarone
“LET US BE OPEN, CELEBRATE OUR SUCCESSES AND USE OUR FAILURES AS EXPERIENCES OR HURDLES THAT WE NEED TO JUMP AND GET OVER THEM IN LIFE.”
Kwa mtazamo wangu finyu ni kwamba success bado she has long way to go brother mwacheni mtoto apate taaluma kwanza. Umaarufu baadae
Nakubaliana na baadhi ya maelezo yako ya awali juu ya lengo la kumotivate wazee wengine kwamba wapeleke watoto wao madrasa ila ningependa kukushauri utafute njia nyengine mbadala.
Fikiria kwamba unaishi nchi za kikafiri ambazo ndio maadui no 1 ya uislam sasa wewe unaonyesha success hao maadai umewatizama vp?
@ Kassem
Nakubaliana na maoni yako lakini ujue kwamba watoto wenye mattzo ktk sio nchi za ulaya tu bali dunia nzima ni watoto ambao wapo kwenye adolscent period na (nakusudia watoto ambao wapo ktk kubadilika kimaumbile). Watoto wengi km huyu Rafia wengi hujasikia kua na tabia ya utovu wa nidham ila ni tabia za kawaida za kitoto.
Lakini watoto wengi ambao hutia aibu wazee wao na uislam kwa ujumla ni wale ambao wameshajitambua. Tunawajua watoto wengi ambao awali walikua wameshika dini sana lakini baade walikuja kuiwacha. Binafsi nawajua watoto walikua namsingi mzur wa dini lakini hivi ninavyotoa maelezo ni kwamba wengine ni wanamuziki, na wangine ni miss, na wengine ni maluuni ni wakawaida, huo ndo msiba, Mungu atunusuru
Mtoto anapobalika kimaumbile basi anakutana na vitimbi vya kila aina, na ktk hayo mashule yenu huko ulaya walimu badala ya kuwafundisha watoto mambo ya kheri ndo kwanza wanawafundisha mambo ya kijitu kizima. Hili wazee walitizama vp?
Ungekua umeshawahi kufundisha wanafunzi basi ungejua nimekusudia nini ktk maelezo yangu, lakini nadhani utanielewa. Time will tell
@ Mbonji
Nakubaliana na wewe kwamba technologia imeongezeka na watu wanatakiwa kuchukua juhudi ili kuenda sambamba na tech. Ila kwa mtazamo wangu tech itumike wakati muafaka, kuna mambo mengine hata tech haihitajiki kutumiwa.
Wasomi wengi walitutangulia ambao ndio tunatumia ideas zao walifanikiwa kusoma bila ya hata hicho unachokiita tech hakijuulikani.
@ Makame Ame
Nakubali kwamba mtoto ameombewa dua nyingi sana hata mimi namtakia kila la kheri ktk maisha yake. Ila tunaweza kuomba dua mara 100 lakini km vyakula vyetu na vivywaji vyetu vinapatikana kwa pato la haramu basi dua hata hapo nje haitoki seuze kufika mbingu ya kwanza.
Chakula cha haramu kinaathiri miili yetu km chakula na kinywaji cha halali kinavyoathiri miili yetu. Damu yetu huo ipo kiharam haram tu then na kila kinachofata ni haramu tupu. Mungu atunusur
Maoni
Niliyosema ni ushauri tu ila mnaweza kuwaweka watoto wenu ktk You Tube km mnavyopenda.
Wabillah Tawfiq
ASSALAAMU ALAIKUM MY DEAR BRO EMBESAKUA,
JIHAAD IS TO FIGHT WITH YOUR HEART, PLS LET US NOT ENCOURAGE ILL FEELINGS OR NEGATIVE ATTITUDES IN LIFE. POSITIVENESS AND NURTURING GOOD DEVELOPMENTS WILL TAKE US FAR AND HAPPY HERE AND HEREAFTER.
Assalaamu alaykum
Alhamdulillah, kwa hapa UK mtoto kama Rafia ni hatuwa kubwa tumefika na ni fakhari kwa jamii yetu ya hapa na pia ni changamoto kwa watoto na wazazi wengine.
Hapo miaka ya awali kiwango cha kusoma Quran kwa watoto kilikuwa chini sana. Madrasah nyingi za hapa UK zikachukuwa juhudi ya kuiweka kiwango cha usomaji kwenye standard inayokubalika na hata nakumbuka katika mwaka 2007 mie binafsi kama ni mwalimu niishajiishwa sana na kuona kanda za watoto za mashindano ya kuhifadhi Quran ya Zanzibar na nikatamani na sisi huku tukafuata nyayo za ndugu zetu wa huko.
Nilipowaonyesha kanda ile wanafunzi wetu wakafurahi na wengine wakaingiwa na hamu ya kuhifadhi lakini ilipokuja part ya tashjii’ wakashangazwa na wakavunjika moyo na wakasema ati haiwezekani kwa watoto wa hapa kwani kule Zanzibar wanayo time ya kutosha.
Hatukuanza kuwahifadhisha watoto moja kwa moja ila tulianza kuweka kiwango cha usomaji juu katika madaris zetu za UK na Alhamdulillah madaris kadhaa zilikubali kuweka sawa usomaji wa Quran na hata zile madaris za ndani ya nyumba na baadhi ya wazazi waliingiwa na hamu ya kutekeleza jambo hilo na mmoja katika ya hao wazazi ni wazazi wa Rafia ambao kazi kubwa wanaifanya mpaka Rafia kufikia hapa. Allah awalipe kheri.
Mwishoni mwa mwaka jana tulianzisha watoto kuhifadhi kwa njia tashjii’ na Alhamdulillah tumeshaanza kupata watoto kama hao kwenye nchi kama hii.
Kamati ya mashindano ya Kuhifadhi Quran ya Zanzibar imetukubalia kupeleka watoto 2013 wa juzuu kumi na kuendelea. Mpaka sasa tunao watoto wanaotimiza juzuu kumi ambao ni watoto wa jamii yetu na wanaishi katika nchi kama hii ya misukosuko. Tunategemea watoto hawa kuwa maimamu wetu inshaallah siku za mbeleni.
Pia hatuwa zinaendelea kuchukuliwa za kuwaendeleza watoto wetu katika dini tartib tartib mpaka tutafika inshaallah. Kama tulivyoshajiishwa na kanda ya mashindano ya kuhifadhi Quran ya Zanzibar basi na clip kama hizi za Rafia zitawaamsha na wengine watakaochukuwa hatuwa ya kuifanyia kazi Quran na dini ya Kiislamu Bi-idhniLLah.
Wabillahit Tawfiyq
@Makame Ame
:kaka hata kama huyu mtoto anatoka Makka kama wazee wake wametoka East cost of Africa husana zanzibar huyo ni mswahili tu.Wazanzibari wangapi wenye asili ya kiarabu waliohamia Oman wanaitwa waswahili hata kama kabila lao ni Busaid.
@Embesakua
kaka kambare mkunje bado mbichi,Huyu mtoto sifa zote zimwedee yeye na wazee wake kwasababu bila ya wazee asingelifika hapo
@ Jazz na Embesakua
Sadaqta. Nimefahamu na bora kwangu kukubali kutoelewana kwa hili.
Assalam alaykum
Embesakua usemayo ni sawa. Mimi nimesoma na watoto ambao walikuwa tokea wadodo washapiga hatua nzuri kwenye mambo ya dini. Lakini shetani ndio shetani hutumiakila njia kupambana na yule ambaye yupo karibu na mola wake.. Toto likisha kuwa tundu hana haja nalo anajuwa atajimaliza mwenyewe.. Hata hivyo mimi nikiona mtu ambao namjuwa alikuwa kwenye amali njema ikisha shetani akamzidi akapotoka si mcheki bali husikitishwa sana sana.
Ukitembelea facebook ukaziona family nyengine za kiislam na watoto na hizo picha walizo ziweka wallah utatamani kulia. Kuna wengine hawana msingi mzuri wa dini lakini wengine ni watu waliosomeshwa na wakalelewa vizuri lakini ulimbukeni ndio tatizo. Anataka na yeye ajulikane kavaa.