Vidio

Video – Polisi akishughulikia makosa ya barabarani

Hii inatambaa uko kwenye mitandao ya kijamii, ninachotaka kukipoint hapa sio kama bodaboda au mwananchi amefanya kosa au hajafanya kosa.Suala huyu polisi yeye anatakiwa kusimamia sheria kama mwenyewe anavyotaka tuamini kuwa mtu hakuvaa helmet.

Tatizo linaloonekana hapa hatua anayoichukua kusimamia sheria, sio sahihi.Yeye ndio mstari wa mbele kuvunja sheria kwa kuanza kuadhibu wananchi kwa kujichukulia hatua mikononi mwake.

Sheria zinasemaje mtu akikamatwa na kosa la barabarani ? Na jeshi la polisi limejipanga kuchukua hatua gani kwa mfanya kazi wake huyu.Vyenginevyo napata taabu kuamini kama jeshi la polisi linatoa mafunzo sahihi ya kutetea kazi zao za kila siku.

Chengine kwa upande wa wananchi hawa, nao wataenda kuchukua hatua gani baada ya mkasa huu uliowakuta.Nauliza maswahili haya, kwasababu sijuwi kama ni ukosefu wa elimu/ufahamu wa mambo.Wananchi wengi wanadhani ni sahihi kwa polisi kuanza kupiga au kusumbua sumbua wananchi.Sheria nataka niamini zipo zinazosema mtu akivunja sheria ya barabarani atahukumiwa vipi.

Kinachotakiwa kufanyika ni wananchi wajikubalishe kuwafikisha mahakamani polisi wa aina hii.Kesi nyingi zikifunguliwa mahakamani dhidi ya jeshi la polisi pengine huko mbeleni watabadilika.Kusema wananchi wanakaa kimya, ndio mwisho mnakuja kuona kisa si kitu AK47!

Share: