Video:Harakati za waislamu – MSAUDI

Written by  //  09/08/2010  //  Vidio  //  Zima maoni

Ndugu,

Hizi ni video za muhadhara wa Sheikh Mohamed Said aliotowa kwenye Dar-es-Salaam University kwa MSAUDI. Natumai utafaidika nazo kwa kujuwa historia ya Waislamu Tanganyika. Kwahisani yako wajuilishe wengine.

Uislamu Tanganyika 1
Lecture of Mohamed Said at Dar-es-Salaam University about the role of Muslims in the struggle for the independence of Nyerere amemtaka Abdulwahid Sayks aandike historia ya mapambano ya ugombozi wa Tanganyika. Nyerere hakuyapenda yalioandikwa, kwani hayakumpa Nyerere umbele. Maandishi ya Sayks yamepuuzwa kwa muda wa kupindukia miaka 30. Hivi sasa maandishi haya yako kwa familia ya Sayks.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=TCoi9xShOxY[/youtube]

Uislamu Tanganyika 2
Mohamed Said anasema uzalendo wa Tanganyika haukuanza na Nyerere. Viongozi wa Kiislamu wameanzisha Tanganyika African Association (TAA) tokea miaka ya 1920.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=P9V9m64yvlI[/youtube]

Uislamu Tanganyika 3
Mohd Said anatuambia kwamba katika kupigania uhuru wa Tanganyika, Tanganyika Railway African Union ikiongozwa na Waislamu walifanya mgomo kwa muda wa siku 82. Huu mgomo umemtia woga Nyerere, na akakata shauri kuitia vyama vya wafanyakazi vyote chini ya mbavu zake. Juhudi zote za viongozi wa TANU na serekali ilikua kudharau Waislamu na juhudi za Waislamu katika kila lengo la nchi. Kama kua Tanganyika haina Waislamu kabisa.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=3VeQ68FgRRM[/youtube]

Uislamu Tanganyika 4
Mohd Said anatueleza kwamba gazeti la “African Events” lilizuiliwa kuuzwa Tanzania kwa sababu ya makala aliyoandika Mohamed Said kuhusu juhudi za Waislamu kupigania uhuru wa Tanganyika. Akafika kutishiwa. Zama za Nyerere Waislamu serekalini walifika kuficha majina yao ya Kislamu.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=D880RX-OC6M[/youtube]

Uislamu Tanganyika 5
Viongozi wa TANU walizungumza maandishi ya Mohamed Said na wakataka kuchukulia hatua kali. Lakini Nyerere alikataa ili asipewew Mohamed umuhimu na umaarufu.
Katika miaka ya 1950, jiji la Dar-es-Salaam lilikua na la Waislamu. Hata mabibi wa Kikristo walikua wakivaa mabuibui, kivazi cha Waislamu.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=mEc0ZnDgd0o[/youtube]

Uislamu Tanganyika 6
Mohamed Said anasimlia kwamba Nyerere aliunda kamati ya kuwajibu vitabu vya Ali Muhsin “Conflict & Harmony in Zanzibar” na cha Mohamed Said “The Life and Times of Abdulwahid Sykes”. Tuhuma kubwa ya Mohamed Said kuwa Nyerere siokuwa kaficha juhudi za Waislamu katika kupigania uhuru wa Tanganyika, bali amefanya kila juhudi kuwakandamiza Waislamu na Uislamu Tanganyika.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=I0V3w_L-XS0[/youtube]

Uislamu Tanganyika 7

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=jczuU_qws2w[/youtube]
Uislamu Tanganyika 8
Mohamed Said anaendelea kueleza. Nyerere aliogopa hili jambo la kura tatu litagawa TANU baina ya Waislamu na Wakristo. Nyerere mwisho aliweza kuifanya TANU ikubali kura tatu. Hapo ndipo Waislamu walipoteza nguvu zao. Hapo ndipo historia ya TANU ikawa ni Nyerere pekee.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=nsuizT5lOO4[/youtube]

Uislamu Tanganyika 9
Mohamed Said anasema TAA ilikuwa imejaa Waislamu. Walitaka kuleta Wakristo ili kuleta umoja wa nchi yote. Hapo ndipo Nyerere alikubaliwa kwa urahisi katika TAA. Mohamed Said anajibu masuala haya: Suala: Je Mtemvu alikuwa sahihi katika suala la kura tatu Suala: Nini hali halisi ya Waislamu? Suala: Vipi Waislamu wamevunjwa?
Suala: Vipi “East African Muslim Welfare Society” imevunjwa?
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=4AHo6BwBCcc[/youtube]

Uislamu Tanganyika 10
Mohamed Said anaendelea kujibu vipi “East African Muslim Welfare Society” imevunjwa.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=RAfXSydQUas[/youtube]

Uislamu Tanganyika 11
Mohamed Said anaendelea kueleza vipi “East Africa Muslim Welfare Society” imevunjwa.
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=13LoT3Fz8dQ[/youtube]

Comments are closed.