Video: ZEC – matokeo ya uchaguzi 1995 – (hesabu za Bwawani
Written by administrator // 04/06/2010 // Vidio // 14 Comments
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=hZpNrZieoFQ[/youtube]
Assalaam alaykum,
Sh. wangu hii documentary inanikumbusha machungu sikuhiyo home kulikuwa kumeshaandaliwa Biriyani ya nguvu lakini amini Mungu haikuliwa na wala hakikuonekana tena kama ni chakula kizuri kwa ajili ya siku ya furaha.
Unaweza ukatuwekea mzalendo net watu wakajikumbusha.
Ahsante.
Taymia




14 Comments on "Video: ZEC – matokeo ya uchaguzi 1995 – (hesabu za Bwawani"
Hii video inanitia uchungu sana na inanikumbusha mbali tokeo hili ambalo Tume ilifeli kuonesha uaminifu na uadilifu kwa Wananchi wake wa Zanzibar.
Angalia Bwana Ali Ameri anavyojikanganya. Siku moja kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, alikiri kuwa hakukuwepo na uchaguzi wa haki na huru, na alikazania kurejewa kwa uchaguzi.
Pili angalieni Bwana Zuberi anavyojikanganya, anataja kura zilizoharibika zaidi ya 4000 kisha anasema Maalim Seif amepata asilimia 49.8 na Dr Salmin amepata alisimia 50.2 Jee asilimia ya kura zilizoharibika mbona haionekani hapa?
Nafikiri wana Statistic na Mathematic wanaelewa
Hata hivyo shukran kwa kuiweka hii video kwani tunazidi kujikumbusha na kusoma our mistakes from the past
Hawa ndio wanafiki waliobakia. Siri imefichuka mwaka huu2010 pale Salim Juma Othman akiwa na akili timmu aliposema kwamba matokeo alipelekewa Nyerere Bara, na yeye alikuwemo katika kusindikiza msafara pale uwanja wa ndege Kiembe samaki ambapo palikuwa hapana umeme ndipo walipowasha taa za gari zao ili kuisaidia ndege iruke.
Mambo mengi yanafanyika Zanzibar. Upumbavu wao Wazanzibara.
YAANI HUYU MWENYEKITI ANAONA HAYA HATA KUIANGALIYA SCREEN ZA MOVING CAMERA ZA WAANDISHI WA HABARI, HALAFU YAANI HIVYO ANAVYODODOSA UTAFIKIRI HIYO ANAYOSOMA SIO LUGHA YAKE MAMA, PIA AMESHINDWA HATA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
LAKINI NDIO HIVYO TENA UJANJA KUPATA KUWAHI HAKUNA MAANA. BAADA YA MATOKEO HAYA TU UFSKA ULIOFANYIKA ZENJ HUWEZI KUAMINI KAMA NI KISIWA CHENYE WAISLAM.
HALAFU NASIKIA ATI HUYU MZEE HICHI KIPINDI CHA KARIBUNI ALIWAHI KUPELEKWA MENTAL SIJUWI KAMA KWELI AU VIPI WANAOJUWA MUTATUSAIDIA NA KAMA KWELI VIPI AMESHAPOWA?, NA HUYO ALIYEMTANGAZA MSHINDI ANAHANGAIKA NA ULIMWENGU KUTIBU MACHO, HIYO NDIO DHULMA, NA DHULMA HAIDUMU NA IKIDUMU BASI HUDAMIRISHA TU.
TUOMBE DUWA HUU WA MARA HII YASITOKEZEE KAMA HAYA.
Mnh ama kweli haya matokeo ni ya kupika. Na bado kidogo tu yaungue. 49.8% na 50.2% ni ushidi wa chini ya 0.5% ambao kwa macho tu inaonyesha mshindi aliyetangazwa hakushinda na si wa kiwango cha mtu kuitwa mshindi kwa ajili ya kuongoza nchi.
Hapa tunaweza kujifunza mwenendo wa tume hii ya uchaguzi. Tukumbuke kuwa matokeo ya Idris Abdulwakil pia yaliwafadhaisha tume kiasi cha kutangaza mara mbili na bado hakufika asilimia ya ushindi.
Kwa mtazamo wangu kuna mambo mawili ya kujifunza kutoka katika matokeo haya mawili. La kwanza ni upendeleo wa wazi wa tume ya uchaguzi wa kulazimisha lazima mtu fulani ashinde ambao sifikirii kuwa utakuwa umeondoka.
Video hii ni ushahidi wa wazi kuwa CCM walishaangushwa katika uchaguzi huo na ndio maana Ali Ameir aliyakataa matokeo hayo hata kabla ya kutangazwa.
Ama la pili ambalo ni muhimu zaidi kwa wakati huu ni kuhusu ujumbe ambao tume unautoa kwa wananchi kuwa kutokana na hali ya kisiasa ilivyo basi serikali ya umoja wa kitaifa ndiyo itakayoondoa matatizo yetu.
Jamani tume kwanini munapindisha haki kwa batili? Uongo siku zote hausimami, leo tumeyaona. Na mtakayoyafanya mwaka huu bila shaka tutayajua tu, its just a matter of time! Na huenda Sir God akawabainisha na mapema mara hii.
Kueka sawa maoni ya Shy, tume imetoa taarifa ifuatayo:
Hapo manaake ni kweli hakuna kura ilioharibika na mahesabu hayako sawa kwenye hizo asilimia.
Marekebisho ya kihesabu ilitakiwa iwe kama ifuatavyo:
…Natumai kosa hilo litakuwa wazi kwa wale watu wa BAM
Nukuu:
**Hapo kuna mchakato mzima wa kisheria ili uwe rais ni lazima ushinde kwa asilimia zaidi ya 50.Hivyo makosa haya yana “motive” au namna, si bure.
@ Mrfroasty
Hiyo aslimia 50 au zaidi ya ushindi inahesabiwa kutoka wapi? Kati ya kura zilizowakubali wagombea au kura zote zilizopigwa?
Naomba ufafanuzi.
@depsis
Bahati mbaya sijasomea sheria upeo wangu wa kisheria ni mbovu.Hivyo natumia akili ya kuzaliwa tuu, nafikiri ni kura zilizopigwa yaani 333,899
Depsis,
Sir God ndie nani tena? Pls tufafanulie.
Sasa tukishayajua yatayofanywa na Tume itakua nini? Kwakweli Zanzibar hatuna Tume wala nini. Ilobaki ni kusindikizana tuu. Tuende tukapige kura tumsindikize Rais wa CCM atangazwe na hiyo inayojiita Tume. Sisi tubaki kulalamika mitaani. Maana hata tukipeleka malalamiko yetu UN hawana maana. Hivyo kweli hawayajui yanayofanyika Zenj. Lakini kwasababu wameyaridhia.
Allah atuletee viongozi waadilifu wanaompenda yeye naye akawapenda Amin.
Shukran
A.ALAIKUM
DAH MIMI NIMEISHIWA NGUVU TENA,HAPO JUU HIZO KURA ZIGEUZENI
SALMINI :48
SEIF : 49.5
ZILIZO HARIBIKA :1.5
HIVI NDINYO ILIVYOKUWA…
DAH HUYU MWENYEWEKITI NIKIMUANGALIA NATAMANI NIMTOE ROHO…MNAFIKI MKUBWA PAMOJA NA TUME.
NA TUME YA MARA HII ITANYA KULIKO MWAKA 95,TUJIANDAENDI MKAO WA KULA,MWAKA HUU WAKITUFANYIA UPUMBAVU HUU NAJITOA MUHANGA KATIKA TUME YOOTE KUITEKETEZA.
MZALENDO AHSANTE SANA KWA KUTUKUMBUSHIA TENA KILIO HIKI. PAIN START AGAIN.
AH NIMESAHAU KURA YAKE MOJA SALMINI : 1% ALIPATA 49
mimi nauliza swala moja tu.jee uchaguzi wa 2000 na 2005 pia nao cuf alizulumiwa kura naona sioni malalamiko au mlishindwa kihalali?
@Muunguja,
2000 na 2005 nadhani itakuwa ni nje ya maada, kwani video inazungumzia 1995.Au unasemaje mkuu?
Maasalaam,
mrfroasty
najua kwamba mada inazungumzia uchaguzi wa 1995 lakini niliuliza swala linalohusiana na uchaguzi vile vile.mimi nataka kujua tu kwamba chaguzi za 2000 na 2005 ilikuwa the some story kama 1995 au vipi mimi nataka munielimishe tu kwasababu sikuwepo nyumbani kipindi hicho.
2000 mie nilikuwepo Zanzibar, ni uchaguzi uliojaa udanganyifu.Nadhani ulikuwa much worse kuliko huo wa 95.Kwani kuna visanduku vya kura kwenye majimbo vilichuliwa na majeshi ya Tanganyika na kwenda sehemu ambazo mawakala wa upinzani hawakuwa na access.
2005 nadhani ni halikadhalika….kwa kweli mimi kama mwananchi sina imani na ZEC.Kuna msemo unasema ikiwa chombo cha uchaguzi hakiko huru, vipi uchaguzi wake utakuwa huru?
Kwa maana hiyo hapo ni paukwa pakawa tuu…hali ya kutoaminiana imeota mizizi na tunaelekea pabaya zaidi kila siku zikenda.Ni aibu tupu kuona maamuzi ya wananchi hayaheshimiwi, na badala yake kuna watu wanajiona wao ndio wana mapinduzi …hivyo wana haki miliki ya kuongoza dhidi ya wengine.
Maasalaam,
mrfroasty