Vijana Zanzibar kuajiriwa uarabuni
Written by MTANGANYAKA // 07/02/2012 // Habari // 25 Comments
Vijana Zanzibar kuajiriwa uarabuni
Imeandikwa na Khatib Suleiman, Zanzibar; Tarehe: 6th February 2012 @ 15:15 Imesomwa na watu: 157; Jumla ya maoni: 0
NCHI za Kiarabu zikiwemo Oman, Qatar pamoja na Kuwait zimekubali kutoa ajira kwa vijana
wa Zanzibar katika nchi hizo.
Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Ajira na Ushirika wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Haroun Ali Suleiman alisema hayo mwishoni mwa wiki na kueleza kuwa nchi hizo zimekubali kutoa ajira na mipango ya kusaini makubaliano hayo ipo katika hatua za mwisho.
Haroun alisema viongozi wa nchi hizo tayari wamefanya mazungumzo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kuwapatia ajira zenye maslahi bora vijana wa Zanzibar.
“Kimsingi tumekubaliana na wenzetu hawa wa nchi za Kiarabu kutupatia ajira kwa vijana wa Zanzibar ambapo makubaliano yapo katika hatua za mwisho,” alisema Haroun na kuongeza kuwa lengo la SMZ ni kuhakikisha vijana wanapata ajira lakini zenye mazingira mazuri yenye heshima.
Aidha, aliitaja mikakati mingine itakayozalisha ajira ni kuimarishwa kwa vyama vya ushirika pamoja na vyama vya kuweka na kukopa (Saccos) kwa makundi ya wanawake.
“Tayari tumeanza kusajili zaidi ya vyama vya ushirika 3,000 pamoja na Saccos ambazo matumaini yetu makubwa zitazalisha ajira kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake,” alisema Waziri huyo.




25 Comments on "Vijana Zanzibar kuajiriwa uarabuni"
GREAT MOVE. TATIZO NI WAKATI SERIKALI INAJARIBU KUTEKELEZA NIA NJEMA KAMA HII, HASARA ILIOPO NIKWAMBA PANATANZULIWA WAPIGA KURA YA MAONI WAKATI HUU WANAPOHITAJIKA NA HUKU TUKIJAZIWA WASIOHUSIKA KWA VISINGIZIO VYA KUPITIA MAOFISI YA MAIDARA YA MUUNGANO YANAYOFUNGULIWA ZANZIBAR KWA KASI ISIYO YA KAWAIDA HUKU ASILIMIA ZAIDI YA TISINI YA WAFANYAKAZI WAKE NI KUTOKA BARA. MAHOTELI YANAMILIKI ASILIMIA ZAIDI YA TISINI YA WAFANYAKAZI WAKE KUTOKA NJE YA VISIWANI.
HALI HII YAPASWA SIO KUKODOLEWA MACHO BALI KUSHUGHULIKIWA KWA VITENDO NA HATUWA YZA MARAMOJA.
YAANI TUMESIBIWA NA NINIII?. VIINIMACHO VYOTE HIVYO VYA MAWIZARA YOTE YA MUUNGANO KUWA MIKONONI MWA WABARA HUKU TUKIAMBIWA MUUNGANO, BASI HATA HUMU VISIWANI. HIVI NI KWELI HATUKUSOMA KIASI HICHOO?.
HAPA PANA AJENDA ISIYO YA SIRI TENA. PANAHITAJIKA MUAMKO WA VITENDO TENA VYA HARAKA SANNA.
kama litapita hilo basi passport zao ziwe mikononi mwao na sio kuzuwiliwa na waajiri wao.
tiketi zao ziwe tayari na gawanyiko wa likizo na sio one way. hapo ndio patakuwa na dalili njema.si hivyo yatawakuta yalio wakuta waganda kule Iraq,na wakajuta hadi kulia kama watoto na wegine kubakwa.kwa kuwa pass zao walinyangånywa wakawa hawana njia ya kukimbia mateso.
Oman na Qatar ni sawa lakini ziliobakia ni vurugu tupu. wakuwait kibao hawataki kurudi kwao,kwa kuwa hakujatulia bado
HIVYO VIKUNDI VYA USHIRIKA NI NDOTO TU
HATA HIYO MALI IKIZALISHWA HAINA SOKO
SEREKALI LA KUFANYA NI KUTAFUTA MASOKO
WAKIAMUA KUFUGA KUKU MNALIANGUSHA SOKO
KWAA KULETA KUKU WABOVU KUTOKA BRAZIL
WAKIAMUA KULIMA NDIO MATUNDA WANAPIGIWA PAKA HAKUNA AYATAKAE
@mBUNJI
Nakubaliana na wewe kabisa,KUNA MAZAO mengi na kilimo cha wanyama hapa zanzibar hawapati soko kabisa,serikali imeshindwa kuzibiti hilo.
Wazanzibari ni wafugaji wazuri wa kuku wa kula na mayai hakuna soko,kilimo cha mboga mboga hatuna soko,na mazo mengine mengine.
Tunashuhudia hayo kila siku darajani tunaona magari yanatoka bandarini eti yana mayai kutoka dar es salaam,inasikitisha,tunaona magari yamebeba kuku kutoka south africa kupeleka mahotelini,inasikitisha,mboga mboga pia hivyo hivyo.
Hiyo miradi wanayoongelea hawa ni miradi gani ya kuwanyanyua wananchi ? Naona ni kuwasumbua tu hao wenye miradi.
Tunashukuru kwa hatuwa mzuri iliyochukuliwa na SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
ILA TU WAZANZIBAR TUNAPATA TABU AU KUHISI UNYONGE TUNAPOKWENDA KWENYE BALOZI ZA TANGANYIKA (TANZANIA) KWA KUJIHISI WAGENI KWA KEJELI ZA MAOFISA WA KITANGANYIKA KAMA VILE UMEKWENDA BALOZI YA MEXICO ,HUJULIKANI HATA KIDOGO KWAVILE HATUNA WAWAKILISHI WETU, UKISEMA UMEZALIWA MKANYAGENI HUCHEKWA KWANI HAKUNA HATA OFISA MMOJA ANAPOPAJUWA WALA KUWAHI KUKUSIKIA.
TUNAOMBA GNU KUHAKIKISHA KUNA MTU WETU KILA PANAPOBALOZI HIZO KWA HAKATI HUU MPAKA TUTAPO GAWANA MBAO.
Hizo nchi tatu zote ni sawa. Na ni nzuri. Zina historia njema na Zanzibar. Na sidhani kuwa Wazanzibari watapata shida. Kwani wapo wenzao waKizanzibari. Mfano tu, wale vijana wa MIAMI wa Kuwait asili yao ni nani? Munajuwa hata kimasomaso Wakuwait ni nyimbo yao pamoja na mengine ya Kiswahili?
Mungu ayatengeneze ikiwa nia njema ipo.
@makame ame nia njema haipo kwa smz sijawahipo kuskia smz ina nia njema. Hizo kazi wanapekwa cheap labor wasio na ujuzi. Hao wote huchukuliwa kutokea makunduchi.
Ama kwa wale wafanyakazi wenye ujuzi hupewa wapemba maana wao lengo ni kuwanyima kuajiriwa na smz. Lengo pia ni kuwaondosha kiaina ktk nchi yao wanayoipenda.
@mtanganyaka
sikwambii ofisi za muungano kujazana watanganyika bali nakuapia wallah kua ofisi nyeti za smz zimejaa vichogo wa bara tena wao ndio wanaoajiri watu. Kuna vitengo special ktk smz ni kwa ajili ya kufanya ubaguzi eti mtu anataka kukuajiri anakuuliza kabila? Whats this.
Smz haijawah kuwa na nia njema na kwa hili nina uhakika hawana nia njema.
@ Makame Ame
Tunashukuru ndugu zetu wapo huko na kwa kawaida yetu husaidiana kadiri hakuna atayekufa njaa, Tunalohofiwa ukipoteza PASIPORTI yako au ukaja kuowa mwenyeji wa huko na kupata mtoto na hata PASI yako kumalizika utaona bora urudi ZANZIBAR ule hasara za tiket kuluko adhaba za Balozini.
Uwongo akiwa mtu wetu yupo pale Zimwilikujuwalo halikuli likakwisha .
Mimi siwafiki vijana wetu kwenda kuwafanya domestic slaves huko arabuni, makazi wanayopewa sio kazi ni nakama kusema ukweli jua kali na wao waarabu wanachukua zile kazi nzuri nzur na sisi wazanzibar wanakuja kutupa makazi magumu.
Jamani maisha ya nje sio maisha kwa mzanzibar mwenye kuona mbali basi ajaribu kufikiria mara mbili. Sidhani km hao waarabu wanatupenda sana kwamba watupe kazi za mana wakati wao wenyewe kazi wanazitafuta.
Hapa znz, ilipaswa sisi ndio tukaaajiri watu kutoka mataifa ya nje ili waje kufanya kazi kama hizo ambazo tunatakiwa tukazifanye huko arabuni. Lazma tuwe wakweli tunapaswa kukuza uchumi wetu kwanza kabla hatujawatoa watu wetu wakenda kupoteza muelekeo wao.
Napendekeza vijana wote walioajiriwa katika mahoteli ya kitalii ya hapa znz ambao sio wazanzibar wapelekwe huko uarabuni na wale wazanzibar ambao wanataka kupelekwa bara arabu waajiriwe kwenye mahoteli yetu ya kitalii huu ndio uzalendo.
Haiingii akilini population ya watu 2mil ya wazanzibar na bado wanahamishwa hamishwa hii inaonyesha nchi haina dira za kimaendeleo kabisa.
Chukulia mifano vijana wetu wanaishi nchi za ulaya wanafanya kazi gani? jibu ntakupa ni kwamba makazi magumu km ya cleaning, kupeba box, vitufe, na km umebahatika basi utakua bus driver au kuchinja halal chicken.
Na wengi ya watu hawa afya zao sio nzur coz kazi hizi wanazifanya kwa miaka mingi sana na mwisho hufariki dunia mifano ipo mingi. Kwa habati nchi za ulaya km UK kuna hio benefit lakini kama sio hio basi nadhani wote maisha yangewashinda na kurudi home km bado hayayajawashinda coz benefit nazo zina mattzo yake.
Kwanza SMZ tunataka ajira zetu wenyewe kwanza tuzipate ambazo ni vigumu wazanzibari kupatiwa.
Nimefanya uchunguzi wangu nafasi za ajira kwa wazanzibari hawazibati sehemu hizi.
Maoffice wakuu wa immgration wazanzibari halisi hatuwaoni.
Kuna airport mpya hiyo taminal tunataka wazanzibari waajiriwe police na immgration.
Wizara za usalama pia wazanzibari ni wachache tunaletewa wakoloni.
Bandarini pia TRA inasemekana ni wakoloni badala kuwekwa wazanzibari,kwa nini ? Halafu munajidai eti smz ipo katikakuwakomboa wananchi suala la ajira,sio kweli bali ni kujisafisha na kujifurahisha nafsi zenu.
Mengine mutamalizia.
@ embesakuwa,,,,,,,,,,,,,,,,, wacha ujinga huo zanzibar hakuna kazi kwa lukha nyengine zanzibar nzurure ,sasa vijana hawana kazi ,kazi kukaa vibaradhani na mwisho wanakuwa wala unga hivyo ndivyo unavyo taka ,serekali yenyewe ya ubaguzi ikiwa wewe sio kaka waziri basi kazi hupati na kwa watoto wa kike ladhima wainamishwe ndio apate kazi na wanayo fanya hayo ndio hao wakubwa sasa wakae ndani wamtegemee baba na mama vipi yakhe wache wende wakatafute maisha ndio ubinaadamu ikiwa elimu yako ndogo basi na kazi nzuri sahau lakini ukiitafuta elimu haikutupi sehemu yoyote ile mimi ninawajuwa wazanzibar arabuni walio soma wana kazi nzuri, amerika pia cnada pia na uk pia inatakiwa mtu uwe na malengo ndio yatakayo kusaidia, sasa hao ambao watapelekwa uarabuni hata tuseme walipwe kiwango cha chini yaani 300 dollar basi itamuinua yeye na wazee wake na mzee wake akiletewa pesa na mwanawe atashukuru si haba mwanangu anatafuta ridhki zake kwa halali bora hivyo kuliko kukaa vibaradhani kupiga sogo tu basi, na kuhusu watu wanao kwenda ulaya na kubeba box hayo ni mapendekezo ya mtu mwenyewe ukitaka box utabeba box na ukiitaka elmu pia utaipata hata ukiwa na umri gani ,lamuhimu tuwasomeshe watoto zetu wasikimbilie kubeba box , lakini useme hawa warabu hawatokupa kazi nzuri well unategemea ufike tu upewe kazi nzuri jitihada li wajada bwana fanya kazi kwa bidii utafanikiwa tu bila ya shaka , bado tu wewe na mawadho ya kuwadhalilisha ndugu zako serekali haina kazi za kuwapa wache waende wakatafute ndio maisha baba , hao hao unawaona wataonewa na waarabu basi usishangae ukaja ukamuona kapewa umeneja kila kitu kinawezekana jitihada ya mtu tu basi usikate tamaa wewe wape mawaidha madhuri kuwa wasikubali kudhulumiwa hapo sawa lakini wache wende wakataradhaki.
huyu sakua sijui hajajua dunia au vipi haeleweki kwanza Oman ni mwiko mzanzibari kufanya kazi za utmwa Qabusi hataki hilo wanapewa kazi nzuri tu wazanzibari tena nawajua wala elimu yao si kubwa na KUSEMA hapo kwetu naungana na wewe ASALAM kama si ndugu wa fulani hupati ajira na elimu yako mwanangu binafsi amefanya mtihani wa U HAMIAJI hawakumpa na amesoma mabanda yote ameambulia kusomesha sekondari skuli ya miwani na mwengine kajaribu unasi tena kapasi na hawakumchukua kwenye masomo sasa watu wafanye nini? tuna jua kama huna mtu serikali hii huna chako maelfu wanazurura na kuishia kula unga wakazidi kutia ufukara wazee wao mana hata kanga ya kusalia ukipepesa kesha iiba badala ya kusaidia wazeewao kila siku walishwe na kufukarisha wazee wao bora wende wakajitafutie riziki.hasa nataka kujua Sakua una miaka mingapi hujui dunia ?
hapa mimi sikioni cha maana kama hamuamini ngojeni watapelekwa Watanganyika, wazanzibari wataachwa hapo hapo, kwani ajira za Zanzibar ni kwa ajili ya Watanganyika na Wamakonde
Huu ni mpango maalum ndugu yangu,nguvu kazi ya vijana kuiyondoa tuletewa wageni zanzibar,kwa vile smz haiko makini kulinda maslahi ya zanzibar basi watawapa wageni vipande vya ukaazi,wewe nenda nje kafanye kazi ukirudi unaambiwa mgeni.
Wangapi wako Dar wanafanya biashara ,walienda zanzibar kuchukua vipande vya uzanzibari walikataliwa wakaambiwa eti sio wakaazi,wengine wapo znz hawakupata hadi leo.
Hapa kuna HILI wazalendo.
Unapata kazi lakini uzalendo unaupoteza na moja uzalendo huo ni haki yako ya msingi na ya watoto wako,ukienda njee ukirudi zanzibar ujue huna chako.
Ukirudi baada ya muda,wamasai ndani ya airport na rubega zao eti security ,ndio muungano huu.
Aslam aleikum,
Mimi kwa fikra zangu Mzanzibar yoyote asijaribu kwenda kufanya kazi katika nchi za kiarabu bila ya kutafakar kwa undani kabisa. Kwenye nchi za kiarabu hakuna kazi kuna utumwa na hususan ukenda kwa mkataba ukifika tu wanazuia Passport yako anaanza kutuma kama mtumwa bila mapumziko na huna pakwenda kulalamika.
Huyo haruni Ally anajua fika ni nini kinaendelea kwanye nchi za kiarabu ukichukuliwa kama mfanyakazi, kwani wanao fanyakazi nchi zile karibu %99 ni jamii ya kihindi na kifilipino na wanatumwa kama Punda na kulipwa dollar 50 kwa mwezi.
Mimi sio kama nawachukia Waarabu no lakini nayajua fika yale yanayo fanyika kule. Kama mtu anahamu ya kwenda kufanyakazi kwenye nchi zile ni bora aende kivyake bila conract yoyote atakuwa hana wa kum control.
Nasema hivi kwakuwa mimi mwenyewe nishaishi katika nchi zile na kilichonipeleka ilikuwa na njaa yangu mwenyewe na sikupelekwa na mtu ndio kwahiyo hakuna mtu aliyekuwa anaweza kunilazimisha kufanya kitu nisicho kitaka.
Lakini nilishuhudia madhila mengi wanayofanyiwa wageni hususan wale waliokwenda kwa contract kama Wahindi, Wafilipino na baadhi ya watu kutoka Africa Wa Ethopia.
Sisi wa Zanzibar tunaukataa utumwa kwahiyo kabla mtu haja amua chocho kama ana fikra ya kwenda kufanya kazi katika nchi za kiarabu ni bara afikiri mara milioni kabla hajachukuwa uamuzi badae akaja akajuta na majuto ni mjukuu.
Mtanzania yoyote asitegemee kama akipata tabu katika nchi za kigeni atapata msaada kwenye ubalozi wa kitanzania hususan akiwa Mzanaibar.
Mimi ni mgeni kwenye nchi za watu siko kwetu kutokana na hiyo hiyo kutafuta maisha niko sehemu ulifunguliwa Ubalozi wa Tanzania na Balazi akaja kuonana na sisi na akatupa mawazo mazuri tu na ikawa kila kipindi anakuja kutuuliza mawazoyetu na kutaka kujua matatizo ya Watanzania lakini utashangaa au si lakushangaza Serikali ya Tanzania ilipoona yule balozi kilasiku anapeleka Serikalini matatizo na mawazo ya Watanzania waliopo huu walimuhamisha mbio mbio.
Wakamleta Balozi mwengine nikisema sasa hivi ana miaka miwili (2) hajaja kuonana na Watanzania na wala hana habari nao na ukimpigia simu anakuambia nashuhuli nyingi.
Ni mwaka jana tu walikuja viongozi kibao wa kibongo akiwemo Mizengo Pinda na Shams Vuai lakini hata hakuwaleta kuonana na Watanzania tunaona tu kwenye magazeti kawapeleka kwake wamepiga picha na familia yake.
Kwahiyo ndugu zango Wazanzibar sivibaya kusafiri kwenda kutafuta maisha lakini fikiri kabla hujaamua niwapi unakwenda na nani anakupieka kwani badala ya furaha inaweza ikageuka kuwa pezadero (Jinamizi)
@chris lkn si itakua mtu kashapata japo kutembea huko duniani? Mie sioni tatizo mtu kama hana la kufanya hapa znz kwenda alau kutembea huko duniani.
Mtu akiona mambo magumu atawatukana watamrejesha kwao.
ninasema bilal ful kwa viongozi wa zanzibar hususan kundi la kina shamuhuna na seif idy na kila aliye kuwemo kwenye kundi hilli KWA NINI MUSIVUNJE MUUNGANO WAZANZIBAR WAKAWEZA KUPATA AJIRA UN NA MASHIRIKA YOTE YA KIMATAIFA PIA NCHI TAKUWA NA HAITEGEMEI UCHUMI WA NDANI KWA MAANA HIYO KILIMO UVUVI NA BIASHARA VINAWEZA KUTUSAIDIA WAZANZIBAR SASA TUMEKUWA KAMA WAINDONEZIA NI CHEEP LEBOUR
UKIVUNJIKA MUUNGANO WATELETWA SULTANI KUMBE SMZ WANAWAFUATA HA KINA QABOOS AU HUKU SI KUFANYWA WATUWA KWA WAZANZIBAR WAKATI WA JEMSHID WAZANZIBAR TULIKUWA TUKINYENYEKEWA SASA KUMBE TUMEGEUKA WATUMWA LOOOOO MASIKINI WALE WATOTO WASIOSOMA NA MWISHO WAKE WATALIA WENYEWEEEEE KIJOGORO WIKA NA NAMAYOO ZANZIBAR MUNAIYUMIZA NA WATU WAKE TATIZO DOGO NI MUUNGANO TU SASA MNAPELEKEKA VIJANA UTUMWANIII MAPINDUZI ITASHINDA DAIMA
@ Abaazanzibar,
Nakuunga mkono. Wakisikia kuwa zanzibar kuna nafasi za kazi arabuni, basi watajazana na watapewa vitambulisho na hao walioko huko tayari watazipata wao hizo nafasi. wamasai watabadilisha nguo na masikio watayatia nta mule kwenye matomo ili wasijulikane kuwa wao ni wamasai. Lakini wali, ugali kuita ugari tu.
Kama GNU inakusudia kuwasaidia vijana wa Kizanzibari, basi iwatafute wale vijana wasio na kazi ndiyo wawatafutie kazi huko arabuni na siyo watu waliomo katika makazi. Pili lazima wazingatie maslahi ya hao vijana huko wakati wa kutiliana mikataba na wahakikishe wanawalipa mishahara yao kila mwezi , kwani watu wengi hasa wa sri, wahindi wabengali wafilipino huwa wanalipwa mwezi mmoja kisha wanawacheleweshea miezi sita na wakidai huwambia kama hutaki kazi basi rudi kwenu. na wakiamua kuwalipa miezi ya nyuma huwafanyia varange wakalipa pungufu.
La kusikitisha ni kwamba warabu walikuja kwetu wakapewa hifadhi hata bila pasi kuwa nazo na wakifanya biashara huria na wala bila viza, wao wanatuzuilia pasi zetu hata ukiwa mwanafunzi kule.
2012 kwa 6:42 um · Jibu
A/alaikum
Kuna msemo unasema:- AKUFUKUZAYE HAKWAMBII TOKA
Sasa hizi tunazoziona ni NJAMA za ujanja ujanja zinazotaka kujaribiwa/kutumiwa ((KUPIGALANDA)) yaani kuwadondowa wale waZanzibari halisi watoke nje ya nchi, ile GAP/KITALU/NAFASI itakayokuwepo hapa Zanzibar? waitumie kwa kuwaleta ‘WAMASAI’ na WAKURYA. Hili JUNGU limepikwa rasmi kwa kisingizio cha kuwatafutia kazi waZanzibari wale waliomo ndani ya Nchi yao Zanzibar. Lakini hapo hapo viongozi wengine wanadai/wanawaomba wale waZanzibari walioko NJE YA NCHI/UGHAIBUNI warejee Zanzibar kwa ajili ya kujenga nchi yao! Jee sasa mwatugeuza sisi waZanzibari ni kama ule mchezo wa TENIS??
Mimi nahisi itakuja mikakati ya aina nyingi sana iliyofanana na ile azama yao yenye anuwani ya:- {{FUKUZA MWENYEJI, KARIBISHA WAGENI)) waZanzibari tahdharini sana, kuweni macho na tuache mchezo wa kuchezea MOTO, tutakuja lia kilio cha “KUNGUU”
SASA NATAKA KUWAPA MKASA WA “KUNGUU NA MBWA MWITU”
Kunguu anadasturi ya kuamka asubuhi mapema sana; ili eti apatiza kutafuta chakula chake kabla ya kuzagaa/kuanza ZAHMA ya ndege wengine. Siku moja alibahatika kuona simba/chui na wanawe wanakula nyama ya paa!! akafanya hila zake mpaka akapata pande/nofu zuri la nyama, akakimbia nalo na akaenda kutuwa juu ya mti mbali kidogo kutoka pale walipo simba/chui na wanawe, kwa kukhofu kujatokea ndege wataomzidi kwa nguvu, maarifa, ulaghai na ujanja!, lakini yoote hayo aliyofanya hayakuthmir/hayakuleta faida kwake, kwasababu chini ya ule mti aliotuwa palikuwa na MBWA MWITU wamekaa chonjo kudoweya kijio/chakula kwa njia ya ulaghai/ujanja au kumsaka waliomzidi wakamuuwa halafu wakajisaidia!!
Kabla ya hayo yooote kutendeka; na kwa vile ukame/njaa ilivowabana? ikawa kila mmoja anaduru huku na kule, chini na juu, kwa bahati nzuri wakamuona KUNGUU juu ya ule mti waliokaa chini yao na mdomoni mwake ameshika pande nono la nyama, wakafurahi sana na wakaingia tamaa kubwa ya kupata mlo ule. Mmoja kati ya wale MBWA MWITU akanza kufanya mzaha na MBINU ZA ULAGHAI/UJANJA na kumpa yule kunguu sifa za uwongo ili apate kufunguwa mdomo wake ili lilepande la nyama lipate kuanguka!!! Akaanza kumwambia:-
Mpenzi wetu ‘KUNGUU’ mbona leo uko kimya, jee unaumwa? hii si-tabia yako jee umenuna na sisi? *KUNGUU*= kimyaa, mbona leo hutuimbii zile nyimbo zako nzuri ambazo zinatutumbwiza na tukahisi raha na kutuondoshea wasi wasi? Hebu tuimbie japo nyimbo moja tuu!! tunakuomba kwa hisani yako? Kunguu aliposikia sifa zile na maneno yalionyorooroo, akaingia ASHKI na hisia kubwa na akanza kufunguwa mdomo wake huku akiimba!!! hapo lile nofu la nyama likamponyoka na kuangukia ndani ya mdomo wa mmoja kati ya wale mbwa mwitu!! hapo ndipo palipo anza kinyang’anyiro baina yao, kwasababu kila mmoja anataka apate yeye tuu.
Baada ya kutokea yale yalitokea, KUNGUU yule alipata huzuni kubwa sana kwa kukosa lile nofu la nyama yake na akaanza kuhaha kwa njaa, lakini hakuchoka/hakuvunjika moyo! akarudi kule alikolipata lile nofu! kwa bahati mbaya hakukutia hata ile ishara ya mifupa, kila kitu kinsoza!! Lakini liliibuka tatizo kubwa dhidda ya maisha yake pale alipokutia ndege wakubwa walikuwa na wao wamebanwa na njaa; wanatafuta chakula, kama vile KONHO, VIPANGA NA SAQR, waka-mover power na kumuuwa halafu wakamla. IKAWA KUNGUU AMEKOSA LILE NOFU LA NYAMA NA VILE VILE AKAPOTEZA MAISHA YAKE!!
Kwa hivo, mimi nahisi kuwa hawa wenzetu wanataka kutumia ujanja huu, ili wawaondoshe waZanzibari wote nchini mwao ili waikose nchi yao, uwattan wao na hatujuwi huko watakako patiwa hiyo AJIRA kuwa watafanikiwa au wataondokea patupu. ((ALLAHU A3LAM)) Kwani tatizo kama hili limeshawasibu wengi sana wale waliohajri kutokaZanzibar na kwenda nchi nyengine, hivii sasa wamebaki kuzurura zurura kama vile wanvo zurura waPalestine.
Ndugu zangu wapenzi, waZanzibar nawanasihi na nikijinasihi mwenyewe kuwa tusijefanya makosa haya, kwani faida yake ni ndogo/qalil na athari zake ni kubwa sana zisizomithali.
Kunamsemo unasemo:- ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA MGUU.
NAWAKILISHA
MCHONGOMA
Hili jambo si la kuumiza watu vichwa. Mimi sijui nia ya Harun au Serikali yake ni njema au la. Pili sijui kama hizo kazi ni za kibarua au za kiofisi. Na kama ya kibarua ni aina gani.
Ni kweli kuwa Wazanzibari hawatoweza kufanya kazi za sulubu kama wanazifanya waPakistani na waBengali na kadhalika. Kwanza ni dhoofu l hali. Siku mbili tu watapata maradhi yasiyotambulikana. Mimi nimewaona wapakistani wanabeba miznga wa AC mtu mmoja, mZanzibari gani aweza kufanya hivyo kwa nature yetu na physical make-up. Ni wachache sana. Kwa hivyo kwa kazi za kibarua take it from me wa Zanzibari hawatoweza kufanya na hawatopewa kwani hawatokuwa na market hiyo
Kazi gani za chini wanaweza kufanya? Kazi nilizoziona waZanzibari wakifanya ni kuwa wanavyowaita wenyewe ‘manaturi’ au walinzi; kwani hilo halina haja ya nguvu. Pili ni kazi kama za garage. Waliosoma kidogo wapo airport wanafanyakazi za kucheck-in abiria nakusimamia kupakia mizigo kwenye ndege. Waliosoma zaidi wanapata kazi za Flight Dispatchers na wenye degree zao wako mameneja wakubwawakubwa.
Sidhani nchi zote tatu hizo kuwa zina azma ya kumtumia mZanzibari kama slave-labourer kwani kazi hiyo kama nilivyosema hapo juu waZanzibari hatuwezi na hatuipiku market iliyopo arabuni. Warabu jambo ambalo wanalolipenda kwa Wazanzibari ni imani yao ya kidini na uaminifu wao katika kazi. Hicho ndicho walichonacho warabu juu ya waZanzibari. Sisi tu waZanzibari tunawaona Waarabu si watu kwa akili zetu zilizotekwa na kutu za Kiafro na ugozi usiomaana yoyote.
Mwarabu atakuhishimu ikiwa unajiwekea heshima yako. Ikiwa hao vijana watakwenda na shekeli za kicheckbob basi kweli warabu watawatoa thamani na kuwaona hawana maana. Na hata kuwapa sura nyengine ya waZanzibari.
Kama nilivyosema kabla, baada ya nia, itategemea kazi yenyewe na watu wenyewe. Wazanzibari wapo arabuni miaka sasa na alhamduliLlahi maisha yao wengine kuliko huyo raisi au waziri wa Zanzibar.
Mimi nnaye sahibu yangu huko arabuni kaanza kazi ya kucheck abiria airport, akawa superintendent, akawa management trainer, akawa senior manager na kupewa dhamana kubwakubwa kufika hadi yeye kuwasaidia Warabu wenyewe kupata kazi na kuwaendeleza kielimu na kikazi. Najuwa mtu huyu keshakuwa mtu mzima lakini bado wanamtaka na wanamngangania akae juu yakuwa keshafika umri wa kuretire.
Sahibu yangu huyu kaanza kazi mwaka 1978 kwa mshahara wa USD500 kwa mwezi na hivi sasa mshahara wake zaidi ya USD10,000 (elfu kumi) kwa mwaka mbali ya facilities nyengine kama matibabu bure popte aendako diniani na mengineyo. Hakufika hapo kwa bahati, bali ni kwa utendaji wake wa kazi, imani yake ya kidini, muamala wake na watu, na of course baraka na radhi za MwenyezimNgu. Ndio maana nikasema itategemea kwa mtu mwenyewe ataleta sura gani katika kufanya kazi atapokwenda arabuni.
Kwa hvyo narejea tena ikiwa azma na nia ni njema basi ahlan wa sahlan MwneyezimNgu atuwafikishe, la ikiwa si njema na kuna ubaya au shari MwenyeziMngu atukinge nazo.
samahani
paragraph ya nane isomeke hivi ‘zaidi ya USD10,000 (elfu kumi) kwa mwezi
Waarabu ni wabaguzi sana bado wana hulka za utumwa na ubwana……Kama ajira zenyewe ni utumwa basi…ingia kwenye andika poor working condition of immigrant workers in Dubai/Arabic countries………..