Habari

vunjajungu yakemewa misikitini

Naaaam, Leo ikiwa ni ijumaa ya mwisho kabla ya kuingia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan. Kama ilivyokawaida khotba zote za swala ya ijumaa zinatakiwa zitolewe kuendana namatokeo.

Misikiti mingi imekemea vunjajungu bila ya kufahamu au kueleza maana yake. Huu umekuwa mtindo wa uchafuzi wa lugha unaoendelea huku wanafalsafa na wasomi wetu bila kujijuwa kufuata upotevu huu

Miongo ya karibuni imehusishwa siku ya vunjajungu na utendaji maasi mkesha wa wiku ya mwanzo ya mwezi mtukufu wa ramadhani. Hii ni kwenda kinyume na lugha fasaha iliyokusudiwa kwamba unaoposema vunjajungu maana yake ni siku ya mkesha wa ramadhani. Kama vile mkesha wa sikukuu

Nidhani ipo haja kubuni mfumo na mtindo mpya wa vipi kuipokea siku hii badala ya kuinasibisha na mambo machafu, halkadhalika tuepukane na kufuata mkumbo na kuanza kuikataa siku ya vunjajungu.

Vunjajungu sio siku chafu wala siku ya uchafu. Hii ni miongoni mwa sikubora. Hivyo tusiichafue kwa dhana, hoja, maelezo yanayopelekea kuona kama ni siku chafu.

Share: